Lipumba amtaka Rais Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Rais John Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake, kwa kuwa amejivisha joho la kuwa Rais wa wanyonge.

Profesa Lipumba amelieleza gazeti la Mwananchi kuwa Rais Magufuli amejipambanua kuwa kiongozi anayeguswa na matatizo ya wanyonge, hapendi makuu, anahimiza ukusanyaji wa mapato ya Serikali na matumizi mazuri ya fedha za umma, lakini watanzania hawajui mshahara wake ni kiasi gani

Profesa huyo aliyejikita katika masuala ya uchumi, alirejea mijadala mbalimbali iliyowahi kuibuliwa kuhusu mshahara wa Rais, ikiwamo ule uliyowahi kuibuliwa mwaka 2013 na Zitto Kabwe, wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kuwa Rais analipwa Sh32 milioni kwa mwezi.

Pia alirejea taarifa iliyochapishwa na Mwananchi, Julai 27, 2015, iliyoandikwa kutoka katika mtandao wa African Review kuwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete ni wa nne miongoni mwa marais wa Afrika kwa kupata mshahara mkubwa wa dola za Marekani 192,000 kwa mwaka sawa na dola 16,000 kwa mwezi, ambayo ni sawa na Sh32 milioni kwa mwezi. Hadi jana jioni, dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na Sh2,187.

“Taarifa ya Ikulu ilikanusha vikali habari zilizochapishwa na Mwananchi. Ikulu ilieleza kuwa habari hizo siyo za kweli. Hata hivyo, haikueleza mshahara wa Rais na marupurupu yake ni kiasi gani?

Pia, katika mjadala wa mshahara wa Rais, Naibu Spika wa Bunge lililopita ambaye ndiye Spika wa sasa, Job Ndugai alinukuliwa akieleza kuwa mshahara wa mtu ni siri yake.

Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma wa wakati huo, Celina Kombani (kwa sasa ni marehemu) alisema kuwa ni kosa kutangaza mshahara wa Rais.

“…Kwa hivi sasa Rais Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake na kama mapato yake ni Sh32 milioni kwa mwezi, basi ajitolee alau nusu ya mapato hayo kuchangia elimu na afya ya wanyonge. Hatua hii itaimarisha taswira inayojengeka barani Afrika kuwa yeye ni Rais wa wanyonge,” amesema Lipumba.

Wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam wiki iliyopita, Rais Magufuli aliwataka mawaziri, naibu mawaziri na makatibu wakuu wachangie Sh1 milioni katika mishahara yao kuchangia elimu.

Pia Rais alieleza kuwa yeye mwenyewe, makamu wake na waziri mkuu watachangia Sh6 milioni kila mmoja, ili zifike Sh100 milioni kusaidia changamoto za elimu bure Mkoa wa Dar es Salaam.

Kutokana na tangazo hilo, Profesa Lipumba alisema, “Ikiwa Sh6 milioni zitakatwa katika mshahara wake wa mwezi mmoja ni wazi mshahara wake na ule wa makamu wake na waziri mkuu ni zaidi ya Sh6 milioni kwa mwezi.

“Mishahara na marupurupu ya viongozi wa Tanzania hayako wazi. Watanzania hawajui kila mwezi Rais, Makamu wa Rais na viongozi wakuu wa Serikali wanalipwa kiasi gani? Malipo ya wabunge pia hayako wazi?” alihoji.

Profesa Lipumba ambaye amewahi kuwa msaidizi wa Rais katika masuala ya uchumi kati ya mwaka 1991 na 1993, alisema kwa kuwa Rais Magufuli amejivisha joho la kuwa Rais wa wanyonge, anawajibika kuwaeleza Watanzania mshahara na marupurupu yake.

“Ikiwa mshahara ni mkubwa sana achukue hatua za kuupunguza kama alivyofanya Mwalimu Nyerere mwaka 1965.”

Hata hivyo, alisema kifungu cha Katiba cha 43 (2) kinaeleza kuwa mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba.

Profesa Lipumba alisema Rais Magufuli akitaka kupunguza mshahara wake itabidi kwanza abadilishe kifungu hicho cha Katiba.

“Anaweza kujitolea mchango wa kudumu utakaokatwa kutoka kwenye mshahara wake kusaidia sekta ya afya au elimu,”alisema.

Profesa Lipumba ambaye ni mshauri wa Benki ya Dunia (WB) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika masuala ya uchumi, alisema ili kuimarisha utawala bora ni muhimu uongozi ulio madarakani utumie mamlaka waliopewa kwa manufaa ya Taifa.

“Mishahara na marupurupu ya viongozi yawe wazi na yaamuliwe na kupangwa na taasisi iliyo huru. Kuweka utaratibu ulio wazi wa kuamua mishahara na marupurupu ya viongozi wa umma wakiwamo Rais na makamu wake, mawaziri, wabunge, majaji, makatibu wakuu na viongozi wengine,”alisema.

Alisema ni muhimu katika ujenzi wa utawala bora, uwajibikaji na uwazi wa viongozi wa umma kwa wananchi wanao waongoza.

“ Inasemekana mshahara wa mbunge katika Bunge lililopita ulikuwa Sh3.4 milioni kila mwezi.Pia mbunge alilipwa Sh8.2 milioni, nyingine kama posho ya jimbo, gharama za ofisi, mafuta, malipo ya wasaidizi wake na dereva.

“Vile Vile, mbunge anapohudhuria kikao cha Bunge alilipwa posho ya Sh80,000 za kujikimu, Sh50,000 za mafuta ya gari na Sh200,00 za kuhudhuria kikao cha Bunge, jumla ni Sh330,000 kwa siku.

“Posho ya siku moja ya mbunge ni zaidi ya mara mbili ya kima cha chini cha mshahara wa Serikali kwa mwezi mzima ambacho ni Sh150,000. Mishahara inakatwa kodi, marupurupu hayakatwi kodi,”alisema.
 
Mhhhh Magu akitaja mshahara wake imani yangu kwake itaongezeka maradufu , kama nehemia msechu wa NHC anapata mshahara wa zaidi ya mil.35 kwa mwezi , Rais Magu atakuwa mara kumi ya huo mshahara
 
Kila Rais ana mshahara wake kwa mfano Uhuru analipwa $13,000 kwa mwezi na Rais wa Ethiopia ni $3700 kwa mwezi, Zambia $ 4600, Mugabe $9000 na Zuma analamba $22500 kwa mwezi.

Hakuna cha kushangaa kama majukumu yake ni makubwa na anafanya kazi ili taifa lisonge mbele we don't mind hata akichukua mshahara zaidi ya Zuma ni sawa tu.

Boris Johnson ( London Mayor) anakula mshahara zaidi ya Putin na Obama combined jiulize kwa nini
 
Basi uwekwe wazi ili watu wajue mshahara wa raisi kwa mwezi ni kiasi gani. Tunapaswa kujua kipato chake. Nakubaliana na Prof. Lipumba kuwa JPM amejipambanua kuwa kiongozi wa wanyonge, basi aseme analipwa kiasi gani, na kama kweli ni mnyonge katika kundi la wanyonge, atumie kiasi fulani kuisaidia jamii kubwa ya wanyonge....
I doubt if that will happen though...
 
To be honest sijui ni nani anae idhinisha mshahara wa Rais wetu, maana America ni congress ndio linapanga.

Sasa ina maana Magu anajipangia? Mpaka mshahara wake uwe siri hivyo? Mbona maraisi duniani mshahara wao sio siri
 
Tunahitaji kuwa na salaries commission kwa mishahara yote inayotoka hazina.
Iwe mwiko watu kujipangia mishahara. Commission iwepo kikatiba na iwe na watu wenye weledi wa hali ya juu kama akina Warioba.

Mkuu wa shirika la umma anapeka bodi ya shirika kufanya mkutano Dubai. Hao ndiyo baadaye waithinishe mshahara wake. Hapo ni majipu tu.
 
Basi uwekwe wazi ili watu wajue mshahara wa raisi kwa mwezi ni kiasi gani. Tunapaswa kujua kipato chake. Nakubaliana na Prof. Lipumba kuwa JPM amejipambanua kuwa kiongozi wa wanyonge, basi aseme analipwa kiasi gani, na kama kweli ni mnyonge katika kundi la wanyonge, atumie kiasi fulani kuisaidia jamii kubwa ya wanyonge....
I doubt if that will happen though...
Hebu mwacheni kumuonea baba wa watu kazi anayofanya abatakiwa actually oengezwe mshahara wake mara mia kama sio Elfu. Wapinzani wameanza kukosa hoja wanaenda mambo ya kipuuzi. Mbona hamjasema mpaka sasa ameokoa kiasi gani. kwani aliekuwa anakula na mshahara juu anapata mbona hamjasema kitu. hebu muache kumuonea. Amejitolea elimu yake, akili zake, mwili wake , muda wake wooote bado na hicho kidogo mnataka kumdhulumu shame on You. Sasa wewe Kaka yangu Lipumba uko upinzani kwa ajili ya nana? Matajiri? I thought ni kwa ajili ya wanyonge hebu sema mpaka sasa umekwishajitolea kiasi gani. Ila jinsi navyompenda Magufuli hababaishwi na wanafiki kama kina Lipum,ba Shame on him. Na ninyi mnaochjangia kwenye Thread hii mmekwishajitolea kiasi gani kwa wanyonge Shame on YOUUUU!
 
Nchi imejaa wapumbavi wengi mno, sijawahi kuona. Kwanza ujuwe huyu sio "baba wa watu", ni raisi wa JMT. Lakini pia jaribu kuwa na exposure kidogo mkuu, ulichoandika ni upupu.
 
Nchi imejaa wapumbavi wengi mno, sijawahi kuona. Kwanza ujuwe huyu sio "baba wa watu", ni raisi wa JMT. Lakini pia jaribu kuwa na exposure kidogo mkuu, ulichoandika ni upupu.
Wewe mwenye exposure mbona ndio umeandika Upupu squred?!?! Leave him alone. Kila mtu anapata mshahara kutoka na na kazi yake na ana haki ya kusema au kutosema hebu kwa kuanzia weka mshahara wako hapa kama ni kitu rahisi . Ni rahisi kusema kuliko kutenda. Basi utaanza ooh yeye ni Rais tunastahilim kujua. Rfere katiba ya Tanzania ya 1977 naamini ndiyo inayotumika kuna vutu vya kibinafsia. Rais ni mtanzania na analindwa na katiba ya Tanzania kama Mtanzania Yeyote!!! na Ana hakui kama Mtanzania yoyote!!!!
 
Hebu mwacheni kumuonea baba wa watu kazi anayofanya abatakiwa actually oengezwe mshahara wake mara mia kama sio Elfu. Wapinzani wameanza kukosa hoja wanaenda mambo ya kipuuzi. Mbona hamjasema mpaka sasa ameokoa kiasi gani. kwani aliekuwa anakula na mshahara juu anapata mbona hamjasema kitu. hebu muache kumuonea. Amejitolea elimu yake, akili zake, mwili wake , muda wake wooote bado na hicho kidogo mnataka kumdhulumu shame on You. Sasa wewe Kaka yangu Lipumba uko upinzani kwa ajili ya nana? Matajiri? I thought ni kwa ajili ya wanyonge hebu sema mpaka sasa umekwishajitolea kiasi gani. Ila jinsi navyompenda Magufuli hababaishwi na wanafiki kama kina Lipum,ba Shame on him. Na ninyi mnaochjangia kwenye Thread hii mmekwishajitolea kiasi gani kwa wanyonge Shame on YOUUUU!
Na bado amejitolea maisha yake, kwa kweli hata tukimwachia ufunguo wa hazina ni sawa tu.
Unafikiri atakomba zote kama wengine?
 
  • Thanks
Reactions: R.B
h

Hebu waleleze jamani maana hata kutafsiri picha tu wanashindwa!
Mtu akikosa hoja anahangaika kuuliza mambo yasio na msingi, mshahara wake wanaujua vizuri wanajitoa ufahamu tu.

Tony Blair former PM ni advisor tu wa JP Morgan anakula $1.5m kwa mwezi. Kila mtu na majukumu

Hivi Lipumba angekuwa personal adviser na akawa anamshauri yote hayo angetegemea kupata mshahara kiasi gani? Najiuliza tu
 
HAKIPUNGUZIWA MAJUKUMU; TUTAMPUNGUZIA MSHAHARA,

RAISI WETU ANAMJUKUMU MENGI NA MAKUBWA
 
Back
Top Bottom