Lipumba amshukia kama Mwewe Maalim Seif

Lipumba amshukia kama Mwewe Maalim Seif

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,632
Reaction score
62,515
Kwa ufupi
Profesa Lipumba amelaumu uamuzi wa CUF kutoshiriki uchaguzi wa marudio kuwa sababu ya kukidhoofisha chama hicho.

Zanzibar. Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama hicho hakina nguvu kama awali kutokana na kutoshiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar.

Akizungumza leo Februari 24, 2018 katika mkutano wa ndani na wananchama wa CUF kwenye ukumbi wa Makonyo Chake Chake Pemba, Profesa Lipumba amesema uamuzi huo wa kutoshiriki uchaguzi uliobarikiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ndio tatizo la CUF kutokuwa na nguvu.

Amesema chama hicho kimekosa nguvu kwa kuwa hakimo tena katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar.

Wakati Lipumba akieleza hayo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar upande unaomuunga mkono Maalim Seif, Nassor Ahmed Mazrui amesema hawatambui ziara hiyo kwa maelezo kuwa Profesa Lipumba si kiongozi wao.

“Chama kinawataka wanachama, viongozi na wapenzi wa CUF waliopo Pemba na Unguja kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao za maisha ya kawaida na kupuuza kabisa ujio huo wa Profesa Lipumba,” amesema Mazrui.

Katika maelezo yake Profesa Lipumba amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikuwa ni fursa kubwa kwa CUF katika kupiga hatua za maendeleo kwa jamii na Taifa, kwamba kutokuwemo ni sawa na kuwakosesha haki wananchi wanaokiunga mkono chama hicho.

“Wawakilishi wangapi tumekosa kwa kugomea uchaguzi hili nataka lieleweke kuwa mtu akifanya jambo lazima aangalie maslahi ya mbali badala ya kuangalia maslahi ya karibu,” amesema.

Amesema kutokana na CUF kutokuwemo katika SUK, chama tawala kinaweza kubadili hata Katiba kwa urahisi.

Januari 28, 2016 Baraza Kuu la Uongozi la CUF lilitangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi (ZEC), likitoa hoja 12 zilizosababisha kufikia uamuzi huo.

Uchaguzi huo wa marudio wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ulifanyika Machi 20, 2016.

Uamuzi wa CUF kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo ulitokana na mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais, wawakilishi na madiwani uliofanyika Oktoba 25, 2015 kwa maelezo kuwa sheria na kanuni zilikiukwa na baadaye kutangaza Machi 20, 2016 kuwa siku ya kupiga kura upya.

Chanzo: Mwananchi
 
Lipumba kiufupi hajielewi. Hivi huwa anafikiria kweli mambo anayofanya? Ukiona hukubaliki, jitoe. Ila anakomaa tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
( )

Salam Wakuu!
Kila mtu mwenye uhai ameumbiwa "mshipa wa hofu/aibu " ndani yake. Hali hii ndio hutufanya mtu yeyote mwenye akili timamu kumuheshimu huyu au yule. Ndiyo hutufanya pia kutaka kutenda mambo ya staha bila kulaumiwa na mtu yeyote. Vilevile, hofu/aibu hiyo hutuweka kuwa WATII kwa MUNGU aliyetuumba, hata kumfanya Yeye awe Juu zaidi na sisi tuwe wanyenyekevu mbele yake. Lakini, ukiona aibu/hofu hiyo haipo ndani ya mtu, ujue either Kalogwa, Anamtindio wa ubongo, or ameamua kujitoa ufahamu!
Tafakari haya:
Mzee Lipumba alishavuliwa uanachama na chama alichokuwa(CUF). Akalia-lia kwa Msajili wa Vyama akarejeshewa uenyekiti kwa mtutu, na sasa anatambulika "mw/kiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa"(yaani atambuliwi na wanachama halali).
Tumeshuhudia (ndani ya wiki moja(16-23/2/2018)) mauaji na majeraha makubwa ya WaTz wasio na hatia yaliyotokana na "maamuzi ya kikatili" yasiyojali UTU. Huku wahanga wakubwa wakiwa ni wapenzi/Viongozi hasa kambi ya Upinzani(CHADEMA). Watanganyika wanataka kuaminishwa kuwa "mauaji na mateso" ni jambo la kawaida!

Tuliambiwa hakuna kufanya mikutano ya Siasa hadi 2020! Sasa, Je, amri hiyo haifanyi kazi kwa Lipumba??? Lipumba (na genge lake) wamekuwa wakipewa na escort ya Police ktk kukamilisha Hujuma zao. Focus yao kubwa ni kuua CUF +UKAWA kwa kutumiwa na CCM nyuma ya pazia la Msajili wa Vyama! Wanalazimisha kufanya "mikutano ya siasa" Pemba ilhali hawana kibali halali cha CUF Yenyewe! Je, wanataka yanayotokea Tanganyika na Pemba yatokee??

Tumeshuhudia akina Z.Z.Kabwe wakikamakwa na kuwekwa maabusu eti kwa kutembelea tu kata wanazoziongoza(ACT), kweli??? Mh. Mbowe hawawezi kumruhusu hata afanye mikutano ktk kata moja tu hapo Dar. but "Lipumba " anapwiyanga tu! Je, si kuwachokoza wananchi?? Wanawatakia nini wananchi wa Pemba?? Taarifa zilishapekwa Police kwamba hawautambui ujio wa Lipumba kwa title ya M/kiti CUF but Police wanamkingia kifua???

Tumezigundua hila za Lipumba na genge lake. Uovu wanaotaka kuuendeleza kwa kivuli cha CCM kwa mabavu na dhihaka haziwezi kuvumiliwa. Mtu mmoja (Lipumba) hawezi kuwafanya Watanzania woote ni MAZIZANIA, la hasha!! Mwisho wa ubaya, aibu!
 
Yeye Lipumba ndie anaekidhoofisha chama kwa sababu ni pandikizi.Kwanza chama kikidhoofu yeye Lipumba itakuwa faida kwake kwa sababu yeye yupo maalum kwa ajili ya kuua vyama.Kama chama kikidhoofika itakuwa vizuri kwa Lipumba kwani kikidhoofika baadae kitakufa na hapo Lipumba kazi yake itakuwa imekwisha atabaki kungoja kupewa kazi nyingine.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kunawakati mtu huwa hafiti tena mahali fulani,au kwa sababu ya umri au mabadiliko ya nyakati,siasa za enzi zile ni tofauti kwa sasa,watz kwa sasa sio Wa enzi zile,lipumba kwa sasa haendani Na mahitaji ya watz,ila kwa sababu siasa ni hobi kwake,ndio maana analazimisha Ku maintain career, bt he is no longer fit for nowdays tz politics.
 
Hivi Lipumba na white hair nani ana umri mkubwa?
 
Lipumba ni mateka.. Huyu Profesa aonewe huruma ametekwa na ikiwezekana jumuiya ya kimataifa imsaidie..

Lipumba tulikwambia lakini urafiki na hao jamaa sio mzuri ona sasa umekuwa mtumwa jamaa yangu na uprofesa wako..
 
lipumba kaishusha cuf toka kura 70000 hadi buku eti kiongozi

kiongozi gani huwezi kuwashawishi hata watu 2000 ??
Mbona umefika mbali huko sana. Kashindwa kushawishi hata jimboni alikozaliwa.
By the way, huo mchaguzi mdogo alioshiriki yeye kapata kura ngapi?. Kama anakiri kama Uamuzi wa Maalim umekidhoofisha chama basi huko ni kukiri kwamba yeye hana nguvu mbele ya Maalim
 
Si ameshiriki uchaguzi Longido Songea na Kinondoni?. Atupe yaliyojiri aone wanaomtumia wanavyomsaidia..
 
Kwa kweli inachosha kusoma Habari za Lipumba
 
Ameongelea hayo akiwa Pemba kweli? Lipumba anauwezo wakukanyaga Pemba kweli kipindi hiki?
 
( )

Salam Wakuu!
Kila mtu mwenye uhai ameumbiwa "mshipa wa hofu/aibu " ndani yake. Hali hii ndio hutufanya mtu yeyote mwenye akili timamu kumuheshimu huyu au yule. Ndiyo hutufanya pia kutaka kutenda mambo ya staha bila kulaumiwa na mtu yeyote. Vilevile, hofu/aibu hiyo hutuweka kuwa WATII kwa MUNGU aliyetuumba, hata kumfanya Yeye awe Juu zaidi na sisi tuwe wanyenyekevu mbele yake. Lakini, ukiona aibu/hofu hiyo haipo ndani ya mtu, ujue either Kalogwa, Anamtindio wa ubongo, or ameamua kujitoa ufahamu!
Tafakari haya:
Mzee Lipumba alishavuliwa uanachama na chama alichokuwa(CUF). Akalia-lia kwa Msajili wa Vyama akarejeshewa uenyekiti kwa mtutu, na sasa anatambulika "mw/kiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa"(yaani atambuliwi na wanachama halali).
Tumeshuhudia (ndani ya wiki moja(16-23/2/2018)) mauaji na majeraha makubwa ya WaTz wasio na hatia yaliyotokana na "maamuzi ya kikatili" yasiyojali UTU. Huku wahanga wakubwa wakiwa ni wapenzi/Viongozi hasa kambi ya Upinzani(CHADEMA). Watanganyika wanataka kuaminishwa kuwa "mauaji na mateso" ni jambo la kawaida!

Tuliambiwa hakuna kufanya mikutano ya Siasa hadi 2020! Sasa, Je, amri hiyo haifanyi kazi kwa Lipumba??? Lipumba (na genge lake) wamekuwa wakipewa na escort ya Police ktk kukamilisha Hujuma zao. Focus yao kubwa ni kuua CUF +UKAWA kwa kutumiwa na CCM nyuma ya pazia la Msajili wa Vyama! Wanalazimisha kufanya "mikutano ya siasa" Pemba ilhali hawana kibali halali cha CUF Yenyewe! Je, wanataka yanayotokea Tanganyika na Pemba yatokee??

Tumeshuhudia akina Z.Z.Kabwe wakikamakwa na kuwekwa maabusu eti kwa kutembelea tu kata wanazoziongoza(ACT), kweli??? Mh. Mbowe hawawezi kumruhusu hata afanye mikutano ktk kata moja tu hapo Dar. but "Lipumba " anapwiyanga tu! Je, si kuwachokoza wananchi?? Wanawatakia nini wananchi wa Pemba?? Taarifa zilishapekwa Police kwamba hawautambui ujio wa Lipumba kwa title ya M/kiti CUF but Police wanamkingia kifua???

Tumezigundua hila za Lipumba na genge lake. Uovu wanaotaka kuuendeleza kwa kivuli cha CCM kwa mabavu na dhihaka haziwezi kuvumiliwa. Mtu mmoja (Lipumba) hawezi kuwafanya Watanzania woote ni MAZIZANIA, la hasha!! Mwisho wa ubaya, aibu!

Mkuu usingekuwa na mihemko ungeona ya kwamba Lipumba alikuwa anafanya mkutano ea ndani na si wa hadhara.
Kwa kadri nifahamuvyo mikutano ya ndani inaendelea kwa vyama vyote
Hivyo sio kwamba Lipumba ameruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa hadharsni.Usipotoshe umma.
 
Back
Top Bottom