Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010

Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Shauri yake na alalamike, si walifanya njama kumtoa Mh. Lwakatare (Chadema) cuf ili waweze kumsaidia etc as Rwakatale angepinga wasifanye hivyo.

Na ndio maana CCM bado wanamsakama wanajua ni vitu fulani anavyo ambavyo ni tishio kwao

Eti huyu analalama now, wakati wanawalamba miguu mbona hakutoa siri?
 
zinedine umeongea jambo kama msomi kama mwanafalsafa...hzi kampen za kidin hazitoisaidia nchi hii hata siku moja.hakuna rais atakayeongoza nchi hii kwa kutumia dini moja....kama mtu atafaa achaguliwe kwa uwezo wake.kikwete alichaguliwa na wakristo weng sana 2005 lakin pia walikuwepo wagombea wakristo hawakuchaguliwa coz wananch waliamin kikwete angeisaidia nchi.aliposhindwa watu wakahama si kwa sabab slaa ni mkristo ila kwa kuwa walidhan labda angekuwa na jipya .ila kikwete akaambiwa wabaya wake wakristo....akaruhusu udin.na kama kuna mkristo anamchukia kikwete sabab ya din huyu ni mpumbavu na haujui ukristo.matatizo tuliyonayo ni yetu wot
 
duuuh kwel kabisaa mana hii ni hatari kama profesa anaongea hayo hamna haja elimu, au ndo wale maprofesa wakukariri na kufoji research?
 
Nilidhani ni habari za
kupikwa, kumbe jamaa wana hadi video?




Kama kweli CCM ina nia ya dhati ya kupambana na udini, basi tunataka
Professor Lipumba akamatwe na kushitakiwa kwa kuchochea udini. Na baada
ya hapo, Kikwete ajiuzuru kutokana na kupatikana kwa ushahidi usio na
chenga kwamba yeye ndiye muasisi wa udini. Na kwamba ndiye chanzo cha
machafuko na mauaji yanayoendelea nchini.
pumba!,kanawe uso urud tena
 
Nadhani waislam wangelimuuliza suala moja la msingi.Ikiwa tulilifanya mbinu "wezeshi" kumuwezesha muislam mwenzetu ashinde na akashinda lakini hakuna alichosaidia katika uislamu zaidi ya kuongezeka kwa mazila, Je bado kuna haja ya kumsaidia muislamu mwingine uchaguzi ujao ashinde? kwanini sisi kama waislam tusichague yeyeote katika watanzania anayeonekana anatetea maslahi ya Raslimali za nchi bila kuangalia dini yake? Sijui angelijibu nini hapa Lipumba. Lakini kwa upande mwingine waislamu tujiulize sana kwamba kama mlichagua kwa hisia za dini, basi ni kosa kubwa mmefanya kwa sababu hata kama tutamchagua Basaleh, as long as haendi kuongoza nchi kwa kutumia quran, basi tufahamu kuwa kumchagua kwetu ni bure. Na iwapo tunajua kuwa atakayechaguliwa ataenda kuongoza nchi kwa Katiba, basi mchagueni yeyote bila kujali dini yake madhali atatetea vema katiba na raslimali zilizopo. Ni ujinga kuwaza kumchagua mtu kwa dini yake katika nchi ya Tanzania kwa vile haiwezekani kuongoza kwa maslahi ya dini moja. Sote waislam kwa wakristo tuna matatizo yaleyale; Barabara tunapita sote, umeme tunakatiwa sote, vyakula vinapanda kwa sote; polisi wanatuonea sote, sasa dini ya nini hapa katika kuchagua? Aidha, ni kweli kuwa tabaka la waislam kuna mapungufu yaliyotokana na masuala mengi ambayo yalikwishajadiliwa humu jukwaani, lakini ni masuala ambayo kama waislamu tunaweza kuya-raise na kuyabainisha kama sehemu ya watanzania kuwa kuna "imbalances" hivyo kuiomba serikali itakayokuepo madarakani kuyashughulikia. Na kwavile matatizo yaliyopo yana nia ya kutatua madhaifu ya kiuchumi na kijamii katika tabaka la waislamu, ni wazi kuwa hakuna Kiongozi atakayekataa hata kama atakuwa mkristo; tena nionavyo mimi huyu kiongozi wa madhehebu ya kikristo atakuwa rahisi kushughulikia kwa kuwa pamoja na mambo mengine atataka kuprove kwamba kuwa kwake ikulu hakumaanishi kwamba hawezi kutatua matatizo ya waislamu na katika kufanya hili litaondoa "wingu" lililopo. Nimalizie kwa kusema ndugu zangu waislam. Katika hii dunia na Tanzania ikiwepo, ni vigumu sana kuishi dini moja pekee na iwapo tunataka kiongozi wa kweli kwa hapa duniani wa kuongoza serikali zinazotumia katiba, tuachane na hisia za kidini. Tutaendelea kuchagua viongozi kwa hisia za kidini huko misikitini na makanisani. Nchi hii haijawahi kuongozwa na chama kingine zaidi ya CCM, lakini imeongozwa na waislam wawili (Mwinyi na Kikwete) na hao wawili hawakuweza kutatua matatizo ya waislamu hali inayodhihirisha kuwa kutatua matatizo ya waislamu hakuhitaji muislamu Ikulu bali chama kipya zaidi ya CCM. Atakayeweza kutatua matatizo ya waislam ni Chama kingine cha Siasa, sio CCM tena. hivyo shime waislamu kiondoeni CCM na wifi yake haraka. Njia kwa sasa iko nyeupe wanamuziki ndio hao wanajionyesha muelekeo wao, ni jukumu lenu na nyie masheikh na maustadh onyesheni muelekeo wenu, kitendo cha kuona kwamba chama flani ni cha dini fulani hivyo hamuwezi kujidhihirisha nacho, kitawafanya muwe nje ya system na kweli kitaendelea kuwa na idadi kubwa ya watu wa dini tofauti, si kwamba wamekusudia bali ninyi waislamu wenyewe hamtaki kujiunga nacho kwa hisia tu. Kwa mfano mi ningetarajia mtu kama Sheikh Basaleh "akijivua shati" na kutangaza nia kugombea Ubunge Ilala, si angeweza kwenda kusaidiana na Msigwa kule bungeni. Msigwa akitoa mathayo 2:40, Basaleh anakazia kwa Quran 3:20-mamboa yangeenda sawa tu na umoja utarejea nchi hii, hakutakuwa na ujinga wa nani achinje wala nini. Zingatieni haya ndugu zanguni.

Ama kwa hakika umefanya uchambuzi yakinifu, nafurahi sana watu wenye mtazamo chanya kama huu wako, huu ni wakati wa kuabgalia maalahi ya taifa kwa ujumla na sio tabaka la dini, kwani haina faida yoyote zaidi ya madhara yaliyojitokeza na pengine yakaendelea kujitokeza
 
SiHasa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Amakweli nimeamini

Kumbe imani hupofusha kabisa Elimu, maono na weledi wa mtu.

Kwa maelezo haya hakuna tofauti kati ya Prof maji marefu na prof Lipumba.

Lipumba amegeuka kuwa pumba na kudhihiliha Jini imani inavoweza mpoteza mtu kabisa.

Je kwa muktada huu huyu Lipumba anafaa kuwa kiongozi wa nchi? Hafai hata kuwa kiongozi wa nyumba kumi maana

ataendekeza udini na kuwagawa wananchi - Huyu ni adui mkubwa wa umoja na mhikamano kwa watanzania.
 
Haya ni mambo mazito na hatari kuliko yale ya Mtwara, ni makubwa kuliko comments za watu hapa.
Kwa nchi zilizopiga hatua katika maendeleo ya kijamii na ustaarabu, kwa kauli hii Kikwete angekuwa in the Hotel Turnel mida hii.
Uchunguzi ungefanyika na kama ingegundulika angelazimishwa kujiuzulu.
Ninaamini kwa kuwa Nchimbi ni 'mtu makini' na 'anayechukia chochezi'
basi lazima atamkamata Lipumba na kumuwerka ndani kwa mahojiano zaidi.

images

Huyu ni mtaalamu wa mengi hata
Upresident wangu bila yeye ungeota mbawa
atawasaidieni mengi tu.
​




  1. Kwa hali ilivyo siri sasa ziko wazi njenje juu ya mwafaka ambao ndio njia mmojawapo iliomsafishia Kikwete kuendelea kuwepo Magogoni.
  2. Nafasi ile ya kwenda kufanya kazi Umoja iliratibiwa na Kikwete kama shukrani kwa kazi ya kujazia kura kwenye kibaba chake.
  3. Huu ni uthibitisho wazi kwamba Ibrahim Lipumba ni mdini sana, na inabidi kuwa makini sana maana ameshaanza siasa za misikitini.
 
Hivi huu msikiti wa Idrissa hauna uongozi kabisa?

Hatuwezi kuleta mambo ya siasa kwenye majumba yetu ya ibada!

Ingawa kuna vilaza wanadhani uislamu pia ni siasa, kuchagua viongozi kipindi kile sio sawa na sasa.

Kuna haja ya sheria kuboreshwa zaidi, na kuweka kipengere cha KUZUIA wana siasa kufanya siasa ndani ya majumba ya ibada.
 
Huyu Lipumba anataka kuiharibu nchi kwa misingi ya udini, matatizo yaliyopo katika taifa hili ni ya watabzania wote na wala sio ya dini fulani. Kama aliuza kura zake kwa maslahi ya udini wake na bado hakikufanikisha chochote inamaana gani ya kuendelea kua na msimamo wa udini, amesahau kwamba hii nchi inaongozwa na katiba na sio Quran. Kama anaipenda sana imani yake awe Sheikh basi ili atetee haki yake kwani sifa za kua raisi wa Tanzania hana tena kila siku anaongea pumba tu kama lilivyojina lake
 
Kama haya yaliyo andikwa na Tanzaniadaima ni kweli na kweli tupu isiyo kuwa na chembe ya shaka ndani yake basi kuanzia leo Lipumba hastahili kuwa mwenyekiti wa chama chochote cha siasaa na ni muda muafaka yeye na jk kuwajibishwa kwa kuwa na mpango ambao nia yake ulikuwa ni kulimega taifa katika misingi ya imani za kidini.

Mivutano na vurugu za kidini tunazo shuhudia leo zina chanzo, kwa hili la Lipumba linatosha kuwa moja ya kigezo cha chanzo cha yeye na chama chake kuwa sehemu ya raisi kuchaguliwa na baadhi ya waislamu kwa misingi ya kidini. Hili pekee linatosha kumuwajibisha Lipumba kwa kuwa mgombea ambaye alivunja katiba ya jamhuri inayo weka wazi kuwa nchi haina dini.

Lakini kubwa la kujifunza ni kwamba Lipumba na baadhi ya viongozi wa kidini wanatakiwa kujua kuwa kuna watanzania waislamu wengi ambao hawapendi kuona nchi au viongozi wa nchi wakipatikana kwa vigezo vya misingi ya kidini na hawapendi na wamechukizwa na namna uchaguzi wa 2010 ulivyo kuwa na chembechembe za udini ndani yake.

Itoshe tu kusema kuwa hii ni aiibu kubwa kwa Lipumba, CUF na hata aliyekuwa mgombea wa CCM ambaye alisaidiwa kwa misingi ya kidini na si uwezo wa kuongoza.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Nilishtuka sana nilipoisoma hii habari lakini chini nilipoangalia chanzo cha habari hiyo nimegundua ni siasa zetu za maji taka zinaendelea kufanyakazi. Ngoja tusubirie reaction ya CCM na episode 2 ya Bukoba Boy si walisema zipo 4 eenh? Nafurahia uamuzi wangu wa kutokupoteza muda wangu na siasa za Wadanganyika.
 
Jamani sidhani jama nitakaa kumuamini tena huyu jamaa sina imani naye tena siasa za udini zitatuharibia amani yetu.
 
Tumsubiri Salva atoe povu ama Waziri wa Habari alifungie Tanzania Daima. Maana ndio wamezoea kufanya hivyo.

Saa ingine siamini kuwa Lipumba amefunguka kiasi hiki bila hata hofu. Bila shaka G.Lema yupo sahihi, acha tusubiri ushahidi wake bungeni
 
LIPUMBA hana tofauti na mganga anae tumia maji kupiga ramli huku mteja wake akimshuhudia bila hata yoga wa kujua kuwa anadanganywa kwakeli LIPUMBA amechemsha hizi sio zama za ramli kwa maji anataka atufumbe macho kuhusu gesi ya Mtara na inavyo onyesha ametumwapia kama alivyotumwa 2010 na mwambia mteja wake kashituka majihayawezi piga ramli
 
Tangu lini tanzania daima likaaminika? Tangu lini tz daima likaandika habari ya kweli? Ama kweli wajinga ndio waliwao
 
Ukristo ndani ya chadema ndio utakizika hiki chama. Huwezi ujashinda Taifa hili bila kuungwa mkono na waislam waliowengi kuliko wote Tanzania. Nashauri chadema wamuweke slaa kugombea halafu aone kura za waislaam zitaenda kwa nani.
Upo waraka wa kanisa ambao ulisomwa makanisa yote Tanzania tarehe 30/10/2010 . siku ya jumapili wakiwataka waumini wote waichague chadema kwa madai wti ccm imeshindwa kuulinda mtaguso wa VATICAN .waraja ule watu waliupata na kuutoa copy hata mi ninao. sasa umesomwa karibu miskiti yote Tanzania ili waonyesha waislaam mipango ya wakristo na chama chao cha chadema. waislaam hawakufanya kosa waliwanyima kura cdm.na naamini mwaka 2015 slaa atakuwa mshindi wa Tatu maana chama kimezidi kupitea. kimebaki kwenye mitandao ya kijamii lkn wananchi wameshajua chuki za kanisa na chadema dhidi ya waislaam. rusubiri 2015.
 
wanasiasa msipoangalia nchi hii mtaizamisha kauli ya Lipumba inadhiirisha wazi kuwa huenda anaanza au wameanza kumtumia ccm kwy vita yao ya kisiasa dhidi ya cdm. inasikitisha kwani nakumbuka mwaka 2005 Lipumba alikuwa akipambana na CCM kuwashawishi watu kuwa cuf si chama cha kiislamu bali ni cha watanzania wote kitu ambacho binafsi ninakiamini lakini leo anakubali kutumiwa na ccm ni ajabu na kweli

Mkuu Politiki,njaa mbaya sana,halafu huyo ndo anataka kuongoza nchi.....!Kule Zenji,2010 Maalim alishinda lakini tuseme sijui njaa,kukosa uzalendo etc,akapokea kitita then akakubali kua Makamu.Hao kina Jusa na Rostam ndo waliofanikisha mpango huo kufanyika,halafu hao CUF wanajiita wapinzani na wataka mabadiliko shenz.i kabisa hao!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom