Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010

Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.

matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
7,224
Reaction score
3,960
Kwa VIDEO, tembelea

VIDEO: Prof. Lipumba akiri kumsaidia Rais Kikwete katika Uchaguzi 2010




​

LIPUMBA AIBUA JAMBO ZITO - AKIRI KUMNUSURU KIKWETE UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na "kumnusuru" Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita.

Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa.

Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa kiimani, Profesa Lipumba alianza kwa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, na ushindani mkali wa kisiasa uliokuwapo.

Alisema hawaoni matunda ya jitihada walizofanya kumnusuru Rais Kikwete asishindwe, kwani hata chini ya uongozi wake, Waislamu wameendelea kutothaminiwa.

"Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi. Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo katika mtihani mgumu zaidi," alisema.

Katika hali ambayo inasemekana ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana kwa mbinu, huku wengine wakiituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ilimnusuru mgombea wa CCM, kauli hii ya Profesa Lipumba inadokeza kwamba anajua mkakati zaidi wa kazi ya Tume ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema "wenzetu wameanza kujipanga" kuelekea 2015.

"Kwahiyo kama Waislamu tunataka kupata haki zetu, kama tunataka kuishi kama raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu, lazima tujipange kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga kwa sababu wenzetu wameanza kujipanga, vinginevyo tutaendelea kubaki maskini na raia wa daraja la nne katika nchi yetu wenyewe.

"Mwaka 2010 wakati mshindi wa uchaguzi wa rais alipotangazwa, mimi nilikwenda kwenye hafla ya kutangazwa matokeo, na nilikwenda makusudi tu, siyo kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila nilikwenda makusudi kwa kujua hali ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo.

"Huku nilikutana na Sheikh Basaleh. Nilipokutana naye, alinipongeza; sijui kama yeye anakumbuka, akaniambia ‘umeweka mbele imani yako na umekuwa mwelewa wa mambo.'"

Hata hivyo, licha ya Profesa Lipumba kuwaambia Waislamu wajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu, hakusema wajipange kupitia chama kipi.

Lakini alisisitiza kwamba uchaguzi ujao ni zaidi ya siasa au rais yupi anafaa, bali maslahi, hasa ya rasilimali nyeti zinazopatikana katika ukanda wa Pwani ya Mashariki, eneo ambalo alisema linakaliwa zaidi na watu wenye imani ya Kiislamu.

Katika moja ya kauli zake, Profesa Lipumba alisema kwamba kuna chama kimoja kinataka kuchukua madaraka ya nchi, lakini kinasaidiwa na mataifa ya magharibi, yasiyoenzi wala kuthamini imani ya Kiislamu.

Kwa muda sasa, zimekuwapo tetesi kwamba CCM imekuwa inafanya siasa za udini dhidi ya vyama vya upinzani, hasa inapoona maslahi yake yapo hatarini.

Mwaka 2010 makada kadhaa wa CCM walitumia mitandao ya simu kuchonga (spoofing) ujumbe wa simu ulioshambulia mgombea mmoja wa upinzani, ukimhusisha na imani yake.

Kauli ya Lipumba imethibitisha pia minong'ono iliyokuwapo muda mrefu kuwa baadhi ya kura za Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais Kikwete.

Katika uchaguzi huo, Lipumba alitangazwa kushika namba ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.

Alipoulizwa kuhusu ziara yake msikitini na kauli aliyotoa, Profesa Lipumba alikiri kwamba alikwenda kuzungumzia hali ya kisiasa nchini.
CHANZO: Tanzania Daima - Mei 26, 2013
 
Last edited by a moderator:
wanasiasa msipoangalia nchi hii mtaizamisha kauli ya Lipumba inadhiirisha wazi kuwa huenda anaanza au wameanza kumtumia ccm kwy vita yao ya kisiasa dhidi ya CHADEMA. inasikitisha kwani nakumbuka mwaka 2005 Lipumba alikuwa akipambana na CCM kuwashawishi watu kuwa CUF si chama cha kiislamu bali ni cha Watanzania wote kitu ambacho binafsi ninakiamini lakini leo anakubali kutumiwa na CCM ni ajabu na kweli
 
Hili suala la udini sijui kama litaisha hapa nchini. Maana ni kama vile kuna watu wamechanjiwa kwamba kila wanachofikiria, kiwe kwenye context ya udini. Hivi Mhe. Lema ule ushahidi wake kuhusu udini wa Mhe. Rais uliishia wapi? Zile siku alizopewa hazijaisha? Tungependa tuuone au tusikie ni nini hasa ukweli wa haya mambo.
 

Kweli Katiba ya NCHI HII inaruhusu MGOMBEA URAIS kwenda MSIKITINI Mara kwa Mara kiasi hichi; Na kuongelea Mambo ya KISIASA? Na pia KUONGELEA chama pinzani kuwa kina pendwa na NCHI za MAGHARIBI lakini Prof. LIPUMBA amesahau alikuwa NEW YORK UN nchi ya MAGHARIBI akifanya kazi ya MUDA wa MIEZI 6 wakati ni Mwenyekiti wa CUF; Lakini MBONA hasemi kuwa na yeye anapendwa na nchi za MAGHARIBI? ndiko anakopata PESA za kununua NYUMBA na MAGARI yake; Sasa MBONA hajawahi kusema amepata kazi SAUD ARABIA?

Kwanini Tunawadanganya Wananchi wa Tanganyika? Nape Nnauye alikuwa Ujerumani kwa Mwaliko wa chama cha SDP kwani huko sio NCHI ya MAGHARIBI? kwanini Tunawadanganya wananchi wetu tunawapa habari tofauti MISIKITINI?

Sasa ni kura ngapi hizo KIKWETE alibeba toka kwa PROF LIPUMBA na kumfanya RAIS???
 
Nilidhani ni habari za kupikwa, kumbe jamaa wana hadi video?


Kwa mujibu wa video ya tukio hilo, ambayo gazeti hili lina nakala yake, Profesa Lipumba alikaribishwa kuzungumza na waumini hao mara baada ya utangulizi uliotolewa na Imamu wa msikiti huo, Sheikh Ali Basaleh, aliyemtaka awaeleze Waislamu hali ya kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kama kweli CCM ina nia ya dhati ya kupambana na udini, basi tunataka Professor Lipumba akamatwe na kushitakiwa kwa kuchochea udini. Na baada ya hapo, Kikwete ajiuzuru kutokana na kupatikana kwa ushahidi usio na chenga kwamba yeye ndiye muasisi wa udini. Na kwamba ndiye chanzo cha machafuko na mauaji yanayoendelea nchini.
 
Hatimaye mambo sasa hadharani juu ya siri ya 'USHINDI' wake Rais Kikwete ambao hadi leo hakuna anayejua kwamba alishinda kwa kura ngapi hasa.
 
Nadhani waislam wangelimuuliza suala moja la msingi.Ikiwa tulilifanya mbinu "wezeshi" kumuwezesha muislam mwenzetu ashinde na akashinda lakini hakuna alichosaidia katika uislamu zaidi ya kuongezeka kwa mazila, Je bado kuna haja ya kumsaidia muislamu mwingine uchaguzi ujao ashinde? kwanini sisi kama waislam tusichague yeyeote katika watanzania anayeonekana anatetea maslahi ya Raslimali za nchi bila kuangalia dini yake? Sijui angelijibu nini hapa Lipumba. Lakini kwa upande mwingine waislamu tujiulize sana kwamba kama mlichagua kwa hisia za dini, basi ni kosa kubwa mmefanya kwa sababu hata kama tutamchagua Basaleh, as long as haendi kuongoza nchi kwa kutumia quran, basi tufahamu kuwa kumchagua kwetu ni bure. Na iwapo tunajua kuwa atakayechaguliwa ataenda kuongoza nchi kwa Katiba, basi mchagueni yeyote bila kujali dini yake madhali atatetea vema katiba na raslimali zilizopo.

Ni ujinga kuwaza kumchagua mtu kwa dini yake katika nchi ya Tanzania kwa vile haiwezekani kuongoza kwa maslahi ya dini moja. Sote waislam kwa wakristo tuna matatizo yaleyale; Barabara tunapita sote, umeme tunakatiwa sote, vyakula vinapanda kwa sote; polisi wanatuonea sote, sasa dini ya nini hapa katika kuchagua? Aidha, ni kweli kuwa tabaka la waislam kuna mapungufu yaliyotokana na masuala mengi ambayo yalikwishajadiliwa humu jukwaani, lakini ni masuala ambayo kama waislamu tunaweza kuya-raise na kuyabainisha kama sehemu ya watanzania kuwa kuna "imbalances" hivyo kuiomba serikali itakayokuepo madarakani kuyashughulikia. Na kwavile matatizo yaliyopo yana nia ya kutatua madhaifu ya kiuchumi na kijamii katika tabaka la waislamu, ni wazi kuwa hakuna Kiongozi atakayekataa hata kama atakuwa mkristo; tena nionavyo mimi huyu kiongozi wa madhehebu ya kikristo atakuwa rahisi kushughulikia kwa kuwa pamoja na mambo mengine atataka kuprove kwamba kuwa kwake ikulu hakumaanishi kwamba hawezi kutatua matatizo ya waislamu na katika kufanya hili litaondoa "wingu" lililopo.

Nimalizie kwa kusema ndugu zangu waislam. Katika hii dunia na Tanzania ikiwepo, ni vigumu sana kuishi dini moja pekee na iwapo tunataka kiongozi wa kweli kwa hapa duniani wa kuongoza serikali zinazotumia katiba, tuachane na hisia za kidini. Tutaendelea kuchagua viongozi kwa hisia za kidini huko misikitini na makanisani. Nchi hii haijawahi kuongozwa na chama kingine zaidi ya CCM, lakini imeongozwa na waislam wawili (Mwinyi na Kikwete) na hao wawili hawakuweza kutatua matatizo ya waislamu hali inayodhihirisha kuwa kutatua matatizo ya waislamu hakuhitaji muislamu Ikulu bali chama kipya zaidi ya CCM. Atakayeweza kutatua matatizo ya waislam ni Chama kingine cha Siasa, sio CCM tena.

Hivyo shime waislamu kiondoeni CCM na wifi yake haraka. Njia kwa sasa iko nyeupe wanamuziki ndio hao wanajionyesha muelekeo wao, ni jukumu lenu na nyie masheikh na maustadh onyesheni muelekeo wenu, kitendo cha kuona kwamba chama flani ni cha dini fulani hivyo hamuwezi kujidhihirisha nacho, kitawafanya muwe nje ya system na kweli kitaendelea kuwa na idadi kubwa ya watu wa dini tofauti, si kwamba wamekusudia bali ninyi waislamu wenyewe hamtaki kujiunga nacho kwa hisia tu. Kwa mfano mi ningetarajia mtu kama Sheikh Basaleh "akijivua shati" na kutangaza nia kugombea Ubunge Ilala, si angeweza kwenda kusaidiana na Msigwa kule bungeni. Msigwa akitoa mathayo 2:XX, Basaleh anakazia kwa Quran 3:XXX-mambo yangeenda sawa tu na umoja utarejea nchi hii, hakutakuwa na ujinga wa nani achinje wala nini. Zingatieni haya ndugu zanguni.
 
Nchi hii inaweza kuwa na matatizo makubwa sana kuliko watu wanavyofkiria. Nilijua tu kuwa CUF kuna siku itasema jambo kuhusu udini. Ndio mana nasema hivi, Zito amuunge mkono Dr. Slaa mwaka 2015 ili mwaka 2020 apite kiulaini. Bila hivyo nchi itaharibika hii. Inaharibika kwa sababu waislamu inakuwa rahisi kutumiwa kisiasa, na hii inatokana na ukweli kwamba uislamu uko interested kwa nationalism
 
Anatafuta huruma ya waislamu, CUF haina nguvu tena, miaka yote yeye ndie mgombea wa uraisi! Ivi mtu Kama huyu akishinda uraisi sijui itakuwaje! Hakuna watu wadhalimu Kama wanasiasa, they're willing to do anything for political gain.
 
Kama kweli Lipumba aliyasema haya anatakiwa ajiuzulu Uenyekiti wa CUF mara moja...!!!!

Mkuu-MM/K,

Anayoyasema Lipumba ndiyo tuliyoyaona. Issue ilikuwa nani ayadhibitishe. Kama kweli tunayo dola imara hapa ndipo pakuanzia kuliponya taifa. Kuna kitu Mungu anaenda kukifanya Tanzania: wanasiasa wanajiweka wazi na wenye udini pia. Hii ni hatua nzuri yakujua tatizo linalotafuna taifa.
 

Kweli Katiba ya NCHI HII inaruhusu MGOMBEA URAIS kwenda MSIKITINI Mara kwa Mara kiasi hichi; Na kuongelea Mambo ya KISIASA? Na pia KUONGELEA chama pinzani kuwa kina pendwa na NCHI za MAGHARIBI lakini Prof. LIPUMBA amesahau alikuwa NEW YORK UN nchi ya MAGHARIBI akifanya kazi ya MUDA wa MIEZI 6 wakati ni Mwenyekiti wa CUF; Lakini MBONA hasemi kuwa na yeye anapendwa na nchi za MAGHARIBI? ndiko anakopata PESA za kununua NYUMBA na MAGARI yake; Sasa MBONA hajawahi kusema amepata kazi SAUD ARABIA?

Kwanini Tunawadanganya Wananchi wa Tanganyika? Nape Nnauye alikuwa Ujerumani kwa Mwaliko wa chama cha SDP kwani huko sio NCHI ya MAGHARIBI? kwanini Tunawadanganya wananchi wetu tunawapa habari tofauti MISIKITINI?

Sasa ni kura ngapi hizo KIKWETE alibeba toka kwa PROF LIPUMBA na kumfanya RAIS???

Umesikika mkuu.
 
Huyu jamaa Sijui alipata vp u profesa wake Hana tofauti na dr Maji marefu....

CCM-B sasa wanajiumbua wenyewe kwamba waho ndio waanzilishi na wasambazaji wa UDINI. CUF na Lipumba ni manyang'au ! Pamoja na u-profesa, bado kichwa ni ZERO kama CHURA Muhongo

CCM na CUF wameumbuka sasa. Hii ni Aibu, Ikulu waje wakikibujikwa na mapovu mdomoni. Tulijua Dhaifu aliiba kura. 2015 Kihama kinawanyemelea. Hawapati kura tena hata waibeje. Huyo Tume ya Uchaguzi wakithubutu watachomwa moto hai..

Salva na Ikulu, njooni muanze kutoa mapovu, kwamba Lipumba ni Muhongo !.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom