The Stig
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,113
- 1,106
Kauli hii ya Lipumba ni ushahidi tosha kuwa haiwezekani kupatikana kwa manufaa yeyote ya maana kwa watu wa dini moja, eti kwa sababu raisi au watawala wa nchi ni wa dini hiyo.
Hata hii nchi apewe Sheikh Ilunga au Ponda au Basaleh awe raisi, tusitarajie kuwa ndio itakuwa pepo kwa waislamu. Hakuna atakachoweza kufanya zaidi ya Kikwete alivyofanya. Kama waislamu au wakristo wanataka waneemeke kutokana na utawala wa nchi, basi wachangue kiongozi mwenye uchungu na nchi hii, bila kujali imani yake.
Matatizo ya elimu duni, afya duni, barabara duni, usalama duni, kipato duni na mengine yote hayawapati waislamu tu, yanamla kila mmoja wetu.
Kwani Lipumba alitarajia Kikwete angejenda barabara, na shule na mahakama, na hospitali za waislamu peke yao? Kwani yeye anatarajia kuwa siku akiwa raisi atafanya hivyo? Anaposema waislamu wanaishi kama daraja la nne anamaanisha kuna ubaguzi mashuleni, mahospitalini, barabarani, mahakamani nk kwamba kama wewe ni muislamu kuna huduma unazuiwa kupata?
Kama ni kuteseka tunateseka wote tu, na kama kuna lolote linalowezwa kufanywa na dini basi ni kuhamasisha waumini wake wafanye bidii kujitafutia maendeleo, na kuisaidia na kuikosoa serikali pale inapobidi. Hayo ndiyo yanayofanyika na dini Tanzania, lakini kwa kauli na uhamasishaji wa watu kama akina Lipumba, siku hizi tunashuhudia dini zikihamasisha uhasama dhidi ya dini nyingine kwa mwamvuli wa siasa.
Mwaka 2015 sio mbali..., tutashuhudia kama huyo akina Lipumba wanamtaka akiingia madarakani ataweza kweli kutengeneza madaraja kwa wananchi kwa misingi ya dini, na kama ataweza kuwaweka waislamu katika hilo daraja la kwanza...
Umeeleza vizuri sana ukweli wa mambo yalivyo! Mara chache unapata mchangiaji anaongea pointi na kwa ufasaha wa hali kama ulivyofanya kwenye bandiko lako hili.