Elections 2010 Lipumba aiponda NEC mbele ya JK

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,285
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana aliungana na wanazuoni pamoja na wananchi kuiponda Tume ya Uchaguzi (Nec) kwa kushindwa kuhamasisha Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa takwimu za uchaguzi wa mwaka huu zilizotolewa jana na mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame wakati akitanzagza matokeo ya urais, ni asilimia 42.84 tu ya watu waliojiandikisha kupiga kura, ndio waliojitokeza kutumia haki hiyo ya kuchaguzi viongozi wao.
Kwa mujibu wa takwimu hizo kati ya watu 20,398,394 waliojiandikisha kupiga kura, ni watu 8,626,283 tu ndio waliojitokeza kupiga kura, rekodi ambazo zilimfanya Prof Lipumba kuhoji kama Nec ilitekeleza ipasavyo majukumu yake ya kutoa elimu ya uraia.

Katika hotuba yake baada ya kutangazwa kwa matokeo yaliyompa mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete ushindi wa kura milioni 5.3, Profesa Lipumba, ambaye alikuwa akizungumza kwa niaba ya wagombea walioshindwa baada ya mshindi wa pili, Dk Willibrod Slaa kutokuwepo, alisema kutojitokeza kwa watu wengi kiasi hicho ni "tishio kwa ukuaji wa demokrasia nchini".

"Ukichukua takwimu za idadi ya waliojiandikisha ambao ni kama milioni 20 na idadi ya kura alizopata mshindi, ni dhahiri kwamba amechaguliwa kwa asilimia 27 tu ya watu waliotakiwa kupiga kura. Hiki si kitu cha kujivunia... hii ni tishio kwa demokraisa," alisema Lipumba ambaye kielimu amebobea kwenye uchumi.

"Tume imetuangusha kwa kuwa imeshindwa kuwezesha wapigakura kushiriki katika uchaguzi."
Alisema ushiriki mdogo wa watu katika uchaguzi ni miongoni mwa kasoro zinazotokana na udhaifu wa Nec ambao wamekuwa wakiulalamikia kwa muda mrefu na hivyo kumtaka mteule huyo wa urais kushughulikia suala hilo atakapoanza kazi rasmi.
Lipumba, ambaye ni mwenyekiti wa CUF, alibainisha kuwa wadau wa masuala ya demokrasia, hasa vyama vya siasa, hawana imani na tume na kwamba upo umuhimu wa kufanya mabadiliko yatakayowezersha tume hiyo kuaminiwa.

Source: Mwananchi.
 
Katiba baba katiba mbovuuuuuu!!!!!!!

Katiba haisemi mshindi atapatikana na asilimia 51 ya colum ya waliojiandikisha kupiga kura, bali asilimia 51 ya kura zilizopigwa, haijalishi hata kama waliopiga kura wapo 500 ya idadi ya watu milioni 43.
 
Back
Top Bottom