Lipumba afafanua maana ya kuwaita CCM ''Intarahamwe"

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,433
Reaction score
6,352
Akiongea na Wazanzibari walio wengi katika viwanja vya Pemba jana May day Lipumba alisema"

"Sisi tumewaita CCM intarahamwe kutokana na lugha zao za kibaguzi dhidi ya makundi mbali mbali ambyo ndio iliyokuwa inatumiwa na jamaa hawa wa Intarahamwe ambayo baadae ikasababisha mauwaji makubwa.

"Ndugu zanguni maana ya Intarahamwe ni wanyaruwanda au warundi ambao wakifanya kazi pamoja ndio tafsiri yake. Sasa pana pana kundi la CCM limeamua kufanya kazi pamoja ili kuzuwia mawazo na maoni ya wananchi na kuanza kuleta lugha za kibaguzi kwa wananchi na katika jamii za kitanzania"

Akaendelea kusema "CCM walipokuwa wanachangia bungeni walikuwa wanatoa lugha za matusi na kibaguzi na wengine walikuwa wanafurahi kupiga makofi na kugonga meza bungeni kushadidia ubaguzi huo na matusi hayo. Ambapo alisema lazima atokee mtu awaeleze lugha za matusi na kibaguzi hazikubaliki.

"Hatutaki yaje yatokee mauaji na vurugu zilizosababishwa na Intarahamwe wa Rwanda. Hatuhitaji na Intarahamwe ya CCM kuja kusababisha vurugu na mauwaji hapa Tanzania."

Kwenu wadau,;
 
Lukuvi ndio kiongozi wa kundi hilo la Intarahamwe kwa Tanganyika na Asha Bakari ni kiongozi kwa kule Zanzibar, hawawezi kuacha kushonganisha utarahamwe wao hawa mana wanajaza matumbo yao.,
Bora kuitwa jina baya kwa matendo usiyofanya. Kuliko kuungana watu ambao wana matendo machafu kama ya Ushoga
 
mtafute Sitta akupatie hansad za lukuvi alivyothibitisha bungeni jinsi alivyofanya utarahamwe makanisani
 
Lipumba amesahau kuwa CCM ni chama Tawala na ndio walioifanya nchi hii kuwa na amani na utulivu.

nchi ina mauaji ya kimya kimya hii tusidanganyane hapa wanafiki wakubwa nyie hata maana ya aman na utulivu hamuijui .
 
Lipumba amesahau kuwa CCM ni chama Tawala na ndio walioifanya nchi hii kuwa na amani na utulivu.
Weweeee!! wamefanya "amani". Wananchi wa tanzania wameamua kuvumilia kuleta amani na utulivu!! katika ya dhulma za ufisadi, uporaji, wizi na ukandamizaji wa CCM!! CCM ni Nterahamwe!!
 
Lipumba amesahau kuwa CCM ni chama Tawala na ndio walioifanya nchi hii kuwa na amani na utulivu.
Hiyo ccm unayoisema ndio ile iliyosaidia ukombozi wa Waafrika, kupiga vita ujinga, kuondoa ukabila, kupiga vita rushwa na kikubwa kabisa ilileta Azimio la Arusha ma sio hii ya sasa!
 
Lipumba amesahau kuwa CCM ni chama Tawala na ndio walioifanya nchi hii kuwa na amani na utulivu.

Watanzania tunapenda sana kuimbishwa nyimbo za wanasiasa kama kasuku. Hivi una amani gani wakati upo katika kiwango cha juu kabisa cha umaskini kama walivyo wananchi wengi nchini? Utulivu tunaoushuhudia unachangiwa na ujinga na umaskini tulionao. Na yote yamesababishwa na mfumo mbaya wa CCM kupitia serikali zake. Think out of the box!!! Nenda vijijini ukaone wananchi walivyopigika huenda hutaamini kama huko pia kuna serikali na hicho chama chao.
 
Akiongea na Wazanzibari walio wengi katika viwanja vya Pemba jana May day Lipumba alisema"

"Sisi tumewaita CCM intarahamwe kutokana na lugha zao za kibaguzi dhidi ya makundi mbali mbali ambyo ndio iliyokuwa inatumiwa na jamaa hawa wa Intarahamwe ambayo baadae ikasababisha mauwaji makubwa.

"Ndugu zanguni maana ya Intarahamwe ni wanyaruwanda au warundi ambao wakifanya kazi pamoja ndio tafsiri yake. Sasa pana pana kundi la CCM limeamua kufanya kazi pamoja ili kuzuwia mawazo na maoni ya wananchi na kuanza kuleta lugha za kibaguzi kwa wananchi na katika jamii za kitanzania"
Akaendelea kusema "CCM walipokuwa wanachangia bungeni walikuwa wanatoa lugha za matusi na kibaguzi na wengine walikuwa wanafurahi kupiga makofi na kugonga meza bungeni kushadidia ubaguzi huo na matusi hayo. Ambapo alisema lazima atokee mtu awaeleze lugha za matusi na kibaguzi hazikubaliki.

"Hatutaki yaje yatokee mauaji na vurugu zilizosababishwa na Intarahamwe wa Rwanda. Hatuhitaji na Intarahamwe ya CCM kuja kusababisha vuruagu na mauwaji hapa Tanzania."

Kwenu wadau,;

Kitendeo alichokifanya Prof Lipuma akilingani na heshima anayopewa na jamii achilia mbali kuwa wasomi wanamtegemea sana katika fani ya Uchumi na masuala mengine kwani ni mingoni mwa watu makini ambao maandiko na matamshi yake vyaweza tumiwa na wasomi kwenye tafiti za kitaaluma. Kama ni kweli ni yeye ametoa ufafanuzi kwa kile alichomaanisha kuwaita wajumbe wenzake ma Intarahamwe na kukimbia vikao vya Bunge bado hajakidhi vigezo vinavyoweza kumrudishia hadhi yake. Haiingii akilini Profesa tunayemuamini kulikimbia Bunge linaloweza kujadili mambo na kufikia maamuzi yanayokubalika kikatiba badala yake anajiunga na kundi lililosheheni ushabiki kwenda mitaani na kufanya mikutano inayohamasisha hisia nje ya Bunge la Katiba ambavo kwa vyovyote matokeo yake hayatumiki kwenye Bunge.

Ni ushauri tu kwamba Prof aombe tu samahani kwamba ilikuwa slip of tongue na awashauri wenzake warudi Bungeni tuendelee kupata michango na hoja makini kutoka kwa watu makini.
 
Kuna wakati chama serikali inabidi iendeshe nchi kidikteta / kibabe ili watu watofautishe kati ya kuwa huru na kutokuwa huru.
 
'Interahamwe'....ili ni kundi kubwa la wahutu wa kinyarwanda lililoongoza mauaji ya kimbali nchini Rwanda mwaka 1994. Ni kundi lililo nia mamoja (kubaka, kufanya mauaji ya kinyama) dhidi ya watutsi. Kwa mauaji hayo yalivyokuwa, nidhairi wahusika hawakuwa na chembe yoyote ya ubinadamu. Walijawa chuki iliyokithiri mipaka.

Kwa hali ilivyoonekana katika mijadara ya bunge la katiba mpya, ni dhairi, wachangiaji wengi kutoka kundi la 'waliowengi' dhidi ya 'wachache' lilionesha chuki iliyokithiri na uchochezi ambao haujawai tokea Tanzania. Walistahili kuitwa 'Interahamwe'. Hata hivyo chembe chembe za unterahamwe ktk kundi ilo la 'waliowengi' zilionekana mapema. Ukichimbua michango yangu hapa JF neno hilo nimelitumia sana kuonesha nchi ilikokuwa inaelekea.

Kwa maana nyingine Interahamwe ni kundi kubwa ambalo linaweza endeshwa na watu wachache wenye madaraka na fedha kufanya maagamizi ya kimbali pasipo hata wao ku-reason kwa nini wafanye ivyo. Hatutegemei Tanzania yetu ifikie huko, japo dalili zinaonesha.
 
Kitendeo alichokifanya Prof Lipuma akilingani na heshima anayopewa na jamii achilia mbali kuwa wasomi wanamtegemea sana katika fani ya Uchumi na masuala mengine kwani ni mingoni mwa watu makini ambao maandiko na matamshi yake vyaweza tumiwa na wasomi kwenye tafiti za kitaaluma. Kama ni kweli ni yeye ametoa ufafanuzi kwa kile alichomaanisha kuwaita wajumbe wenzake ma Intarahamwe na kukimbia vikao vya Bunge bado hajakidhi vigezo vinavyoweza kumrudishia hadhi yake. Haiingii akilini Profesa tunayemuamini kulikimbia Bunge linaloweza kujadili mambo na kufikia maamuzi yanayokubalika kikatiba badala yake anajiunga na kundi lililosheheni ushabiki kwenda mitaani na kufanya mikutano inayohamasisha hisia nje ya Bunge la Katiba ambavo kwa vyovyote matokeo yake hayatumiki kwenye Bunge.

Ni ushauri tu kwamba Prof aombe tu samahani kwamba ilikuwa slip of tongue na awashauri wenzake warudi Bungeni tuendelee kupata michango na hoja makini kutoka kwa watu makini.

Unafatilia kwa karibu michango ya wabunge wako CCM? Naona hata JF mara chache unapatembelea, you might be far from the reality!
 
Hakuna cha ajabu kwa Lipumbafu askafurulah.... ni mekosea ni Lipumba, Kuwaita wenzake Interahamwe na kuleta tafasri ya kibabaishaji! Lipumba ni mbaguzi, Gaidi na mnafiki. Mbona alipoitwa Shoga na mliberali hakutoka bungeni? mbona hakwenda Zanzibar kuitisha mkutano wa hadhara na kutoa tafasri? .Achana na Prof. kilaza.
 
Kitendeo alichokifanya Prof Lipuma akilingani na heshima anayopewa na jamii achilia mbali kuwa wasomi wanamtegemea sana katika fani ya Uchumi na masuala mengine kwani ni mingoni mwa watu makini ambao maandiko na matamshi yake vyaweza tumiwa na wasomi kwenye tafiti za kitaaluma. Kama ni kweli ni yeye ametoa ufafanuzi kwa kile alichomaanisha kuwaita wajumbe wenzake ma Intarahamwe na kukimbia vikao vya Bunge bado hajakidhi vigezo vinavyoweza kumrudishia hadhi yake. Haiingii akilini Profesa tunayemuamini kulikimbia Bunge linaloweza kujadili mambo na kufikia maamuzi yanayokubalika kikatiba badala yake anajiunga na kundi lililosheheni ushabiki kwenda mitaani na kufanya mikutano inayohamasisha hisia nje ya Bunge la Katiba ambavo kwa vyovyote matokeo yake hayatumiki kwenye Bunge.

Ni ushauri tu kwamba Prof aombe tu samahani kwamba ilikuwa slip of tongue na awashauri wenzake warudi Bungeni tuendelee kupata michango na hoja makini kutoka kwa watu makini.

Prof. Lipumba ndye MSOMI wa kwel kwan usimamia kwel hyo. Achana na Shivj, Mwakyembe na wengineo wasomi uchara wasakatonge mapumbafu hayo manafiki yanayokimbia kivili chao kwa kpndsha ukwel na kuugeuza kuwa uongo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom