Lipi jema

Kwa kweli mmenifungua sana macho yangu katika huu ulimwengu wa mapenzi. So huwa ni hadithi za kijiweni tu kuwa ... usimwonyeshe mwanamke kuwa umempenda sana ....atakutawala eh?
Salaam,
Mapenzi sio kama project flani ambayo unaweza kuweka indicators of success, huwezi kusema wivu ni indicator ya love, NAKATAA...inaweza kuwa indicator ya infiriority complex, huwezi kusema kuangalia simu ya mwenza wako ni indicator ya insecurity.....inaweza ikawa ndo style yake ya kulinda mali yake........na ana-define kama LOVE...strange eeh!!!

Kuonyesha kuwa unampenda mtu...maana yake ni nini? mtu kujisikia au kuona anapendwa sana maana yake ni nini??
Mimi binafsi nafikiri....na labda naamini, BUSARA ni muhimu katika kila jambo. definitions za mapenzi zinakuwa influenced na mambo mengi sana e.g. tamthilia, hadithi za kusadikika, stories kutoka kwa marafiki, nakathalika)

Need I say more??!!
 
hapo utanidai bia tatu!...please!umeongea kitu fulani OUTSTANDING
.....umekosea.............valuu tatu!! I mean, hivi zile savana si zimefanana na valuu, au zimefanana na cocakola!! mi sijuagi vinywaji venye rangi bana!!!
 
Unajua swala hapa sio kuonyesha au kutoonyesha mapenzi. Ukweli ni kwmaba mapenzi nikitu natural, kinatoka ndani ya mtu biola yeye mwenyewe kuhusisha ufahamu wake. Hizi ni hisia asilia. Mtu hawezi kuanzisha "initiate love feelings", bali zinakuja naturally kulingana na mazingira husika. Ila kitu mtu anachoweza kujaribu kufanya nikuzuia kidogo," suppress them".

So Kulingana na mtazamo huo, kama hisia za mapenzi zimejijenga kuhusu mtu fulani na hisia hizo ni genuine, mhusika hawezi kuzuia zisijionyehse wazi kwa muhusika na hata kwa watu wanao wazunguka. Mapenzi ya kweli ambayo misingi yake haitokani "WHAT I AM but rather WHO I AM", ni natural na yanajiachia bila muhusika kujitambua.

Tatizo linajitokeza pale mtu, the other side, anapokuwa hana mapenzi ya kweli kwako then there is no balance. Anakutumia na kukutesa. Na huu ni ujinga mkubwa na ulimbukeni wa kimapenzi.

kumpenda mtu sio kosa na kumwonyesha kuwa unampenda sio hiari bali nihitaji la kimapenzi. We just have to learn how to appreciate love that is being offered to us.
 
kwa kweli ni ngumu kupretend..Sidhani kama inawezekana watu huwa tunaongea tu midomoni lakin practically haiwezekani ila kupretend unapenda hilo linawezekana ingawa ukiwa makini itajua tu kama huyu mtu anapretend ama la.
 
What??? nipe AK47 yangu.....haya niambie ni wakina nani wamehusika!!

lakini ina maana umekuwa hard-core!!

B here u come!!!!! hahaaaaaaaaaaaaaaaaa lol!!

yaani kwa maneno mengine nunda au sio?? sasa hito AK47 tena ndo unataka kuangamiza au....
utakua hujanisaidia bana hebu tafuta msaada mwingine basi B!!!......can we finish wat we started???
 
Love deeply and affectionately. You may get hurt but its the only way to live life completely!!!
 
Kwa kweli mmenifungua sana macho yangu katika huu ulimwengu wa mapenzi. So huwa ni hadithi za kijiweni tu kuwa ... usimwonyeshe mwanamke kuwa umempenda sana ....atakutawala eh?

...ki ukweli hizo hadithi za kijiweni zipo nami nishazisikia sana. Ukichunguza kwa makini, wanaokwambia hayo hawakutakii furaha maishani mwako. Naamini kuna tofauti ya wanaopendana na kujali, na 'wanaonyesha' upendo (kwa matarajio fulani)

Wanaopenda na kujali hawana haja ya 'kuonyesha watu' kiasi gani wanavyopendana. Maisha yao yamekamilika, maelewano, masikilizano nk ni kawaida.
Mashaka ni kwa wale ambao hupenda kwa matarajio fulani... hao ndio wale ambao (kama ni mke/mume) atatumia 'gharama' zote aziwezavyo 'kuwaonyesha' walimwengu wanaowazunguka jinsi gani anavyompenda mwenza wake, ilhali nyumbani kwao hakuna amani, mapenzi wala masikilizano.

Mila, desturi pia zinachangia suala la 'kuonyesha' upendo. Kushikana mauno, na mabusu hadharani kwa jamii nyingi za kiafrika bado halipendezi, mke akianza kelele kwanini humpendi kama 'wanavyoonyeshana' Upendo wacheza sinema wa kwenye 'Isidingo', ujue kuna walakini mkubwa kwenye IQ yake.
 
Love deeply and affectionately. You may get hurt but its the only way to live life completely!!!

Thank you! bht you are in the zone. Nafananisha wale ambao wameamua kutowaambia jinsi wanavyowapenda wapenzi wao kiasi gani kwa kuogopa kuumizwa kimapenzi na jamaa mmoja ambaye amekataa kataa kujifunza kuendesha gari eti kwa kuwa kuna ajali nyingi za magari na anaogopa kufa au kupata kilema cha maisha.
 
asikwambie mtu ndugu yangu, hakuna mtu anayependeza kama anayekuambia jinsi anavyojisikia akiwa na wewe au ukiwa mbali naye.... love without expression is like a car without wheels

kwenye hii kesi nadhani MJ1 has all rights to express herself, it comes as a reflex na pia inaleta raha ya pekee
 
MJ1,

Kupenda robo-robo au nusu-nusu, haiwezekani!

Onyesha pendo lako 100%: whether yule mpendwa anapendeka au hapendeki: mwachie Mungu - Amri Kuu ni hii "pendaneni kama nilivyowapenda"
 
Huwezi kupretent love ..penzi likiingia moyoni ni kama kikohozi lazima ukohoe ..
haya mengineyo sijui niseme nini mie
 
JS thanx am fine mydia ninamshukuru MUNGU.

Ndio hapo sasa nashindwa kuelewa... kuna baadhi ya wanaume huwa wanasemaga eti ukumwonyesha mwanamke unampenda sana atakuchezea sasa nashindwa kuelewa ina maana wao wanauwezo wa kuficha?? au ndo usanii tena?
Inawezekana kabisa kuficha mapenzi MJ1. Mimi mwenyewe nina hakika ninampenda my gal kuliko ninavyomuonesha.
 
Ni kweli The Boss nakubaliana na wewe kabisa kuwa kama umeumizwa itakuchukua muda kuonyesha mapenzi ya kweli kwa mwenzi wako. But ni ngumu kwa mtu ambaye hajawahi kuumizwa lets say ndo mpenzi wa kwanza huyo. Mimi nadhani kuumizwa kwenye mapenzi ni bahati ya mtu- si kitu ambacho unawezapanga kuwa nitahakikisha mapenzini siumizwi na ni jambo la kumshukuru MUNGU au?
Mi nadhani kinachotokea cyo kwamba unaficha bali kutokana na kumbukumbu za kuumizwa unakuwa bado hujamkubali mpenzi wako mpya 100%. Kwa kifupi anakuwa bado hajakuingia kumtima mzima mzima.
 
Mj1 shkang!

Huwezi kuplan kumwonyesha mtu kama unampenda au laa. Hivi vitu vinatokea nachurale. We unaweza fikiri humwonyeshi kama unampenda kumbe ndiyo unamwonyesha mpaka ndugu, jamaa, marafiki na maadui wanaona.

So; kama unapenda mjukuu wangu MJ1, there is no way, mpenzio atajua tu. And otherwise of course.
Mkuu hapo kwenye red umenipa angle muhimu sana ya kuangalia hili suala.
 
...sweetheart, kwani unamuonyeshaje mtu kuwa unampenda? nadhani kumpenda mtu ni 'natural' tu wala haihitajiki kumuonyesha unampenda as if maisha ni Isidingo.
What I mean is, huna haja ya "kumuonyesha" mtu kuwa unampenda, wewe mpende tu mwenyewe atatafsiri anapendwa au la.

...or, did i miss your point swhr?
Hapa mimi naona ni lugha tu ndio zinagongana ila kinachoongelewa ni kitu kilekile. Yaani unaposema we mpende tu, kwani kumpenda mtu hadi ajue unampenda maana yake ni nini. Kuna vitu unakuwa unafanya kwa umpendaye ndio vinavyofanya apendwaye ajue kuwa anapendwa na kwa kufanya vitu hvyo ndio tunasema anayependwa anaoneshwa kuwa anapendwa. Otherwise kama utasema we mpende tu halafu hakuna mabadiliko yeyote sina hakika sana kama hilo penzi litakuwa na maana yeyote kwa apendwaye.
 
swala la kupenda linatokea automatically na huwezi kulicontrol,na ndio maana huwezi kuamua kuonyesha au kutokuonyesha hisia hiyo,itakuja tu na utashangaa hata mama yako anakwambia, 'i know you are in love...'
Mama anaweza kusema you are in love kwa sababu anakujua vizuri pengine kuliko hata unavyojijua wewe mwenyewe. kwa hiyo mama yako ku-detect hiyo situation haina maana kuwa hata unayempenda ameweza kuliona hilo.
 
.....umekosea.............valuu tatu!! I mean, hivi zile savana si zimefanana na valuu, au zimefanana na cocakola!! mi sijuagi vinywaji venye rangi bana!!!
hehehehe!nilisema bia nikimaanisha VALUU!
 
Kwa kweli mmenifungua sana macho yangu katika huu ulimwengu wa mapenzi. So huwa ni hadithi za kijiweni tu kuwa ... usimwonyeshe mwanamke kuwa umempenda sana ....atakutawala eh?
Be careful kuna uwezekano mkubwa wengi walioongea hapa wana mtazamo unaofanana kwa sababu ya mazingira yao or may be coincidence au sijui nini. kwanza ni watu wangapi walio-respond. Ukianza kuwahesaba sidhani kama wanazidi kumi. Sidhani kama ni busara kutumia maoni ya watu kumi ku-generalize hii ishu. Pata maoni kutoka kada mbalimbali kwanza na sio watu wenye access na JF peke yao. Ni angalizo tu.
 
Kwa kweli mmenifungua sana macho yangu katika huu ulimwengu wa mapenzi. So huwa ni hadithi za kijiweni tu kuwa ... usimwonyeshe mwanamke kuwa umempenda sana ....atakutawala eh?

Nasikia kuna msemo kwamba "To be happy with a man, you must understand him a lot and love him a little. To be happy with a woman, you must love her a lot and not try to understand her at all"

 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom