Linux,unix etc

martial arts

Senior Member
Jun 26, 2014
191
99
Habarini za muda wakuu,kama ilivyo ada ningependa kufahamu au kupata maelezo kuhusu linux,kali linux na unux.
Karibuni!
 
kuwa specific kidogo.

unataka kujua maana yake?
jeunataka kujua namna ya upatikanaji wake?
auunataka maelezo ya namna ya kutumia?
 
Linux and Kali Linux all the same, ni a penetration and vulnerability testing OS which unaweza tumia in many ways so all you bruh
 
Linux ni kernel (ni software ambayo ipo level ya mwisho inayo-interact na hardware) ilitengenezwa na linus torvad kwa ushirikiano na ma-developer 100 kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Ina mizizi kutoka UNIX (hapa apple pia os zake ni unix type os).

Linus amechukua muunganiko wa jina lake na unix kupata linux.

Hivyo linux kernel ndio hutumika kutengeneza operating system za linux ambazo hujulikana kama linux distros.

Mifano ya operating zinazotumia linux kernel ni android, ubuntu, kali linux, linux mint, debian, fedora,tizen, red star os (north korea), kubuntu, cent os na nyinginezo.

Linux kernel na operating system zake huwa ni open source hivyo unaweza kuchukua source codes za os yoyote na ukamodify na ikibidi ukaipa jina lako.

Ila sharti na ww utapaswa source code utapaswa kuziweka public.

Linux os zinasifika kwa usalama lakini hivi karibuni kuna wahuni walitengeneza virus ajulikanae kama crossRat aliye na uwezo wa kuatack windows, linux na mac os ya apple.

Servers nyingi hutumia linux kutokana na usalama na uwezo wa ku-customize.

Ila developers wengi hasa watengeneza magemu hawapendelei kuunda software za linux oses kutokana na open sources software users hupendelea vya bure na pia linux market share ni ndogo kulinganisha na windows au mac os.

Mimi ni ubuntu user, linux os huwa nzuri kwa ajili ya kujifunza.

Ila pia mambo ya ku-type commands sudo apt-get install software haya yanachosha watu.

Kwa layman linux huwapa wakati mgumu kutumia ila huwa kuna guide books huwa zina commands zote.
 
Natumia Mint linux kwenye ki laptop kidogo, about 500 GB HDD, 8 GB RAM, specifically kwa ajili ya ku download podcasts kwenye Gpodder, halafu na backup podcasts kwenye external drive ya 5 TB. Halafu backup naipeleka kwenye NAS shared folder.

It works pretty good.
 
Back
Top Bottom