SI KWELI Link inayosambaa ya kazi za TRC

SI KWELI Link inayosambaa ya kazi za TRC

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Je kuna uhalali wowote kuhusu link inayosambaa whatapp ambayo inamfanano na site ya TRC,Ikijumuisha nafasi mbalimbali za kazi katika shirika la TRC ususani SGR.
Screenshot 2025-03-27 125537.png
 
Tunachokijua
Shirika la reli Tanzania (TRC) ni shirika lililoundwa chini ya Sheria ya Reli Namba 10 ya mwaka 2017 kwa lengo kuu la kutoa huduma ya usafiri bora na uhakika wa reli, Kusimamia, kuendeleza na kuhakikisha ulinzi na usalama wa miundombinu ya reli nchini Tanzania.

Madai

Mdau wa JamiiCheck.com amehitaji kupata uhalisia wa taarifa inayosambaa na kiungo (link) inayodaiwa kuwa ni ya shirika la Reli Tanzania kuhusu nafasi za kazi kwa mwaka 2025. Nafasi zilizotajwa ni wahudumu ndani ya treni (kiume na kike), wafanya usafi, wapakiaji mizigo, watoaji mizigo na wakatishaji tiketi vituoni. Taarifa hiyo inaendelea kueleza kuwa mwisho wa kutuma maombi hayo ni mwezi wa 5 tarehe 10, 2025.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli. Ujumbe huo unaonekana kuwa umetengenezwa na watu wenye nia ya kufanya ulaghai kwa wananchi.

Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo haijatolewa na shirika la reli Tanzania (TRC), na kiungo (link) kinachotumika si cha shirika la reli Tanzania. Shirika la reli Tanzania na taasisi nyingine za serikali zinatumia kikoa (domain) ya .go.tz ama .co.tz lakini kiungo kilichoambatanishwa kwenye ujumbe potoshi haina kikoa hicho.

Hata hivyo ukifungua kiungo kilichoambatanishwa kwenye taaraifa potoshi inafunguka tovuti ambayo si ya shirika la Reli Tanzania.

Shirika la Reli Tanzania pia limekana kuhusika na taarifa hiyo inayohusu kutoa ajira mbalimbali kama zinavyoonekana kwenye Tangazo potoshi. Tazama hapa

Attachments

  • Screenshot 2025-03-27 125641.png
    Screenshot 2025-03-27 125641.png
    241.8 KB · Views: 29
  • Screenshot 2025-03-27 125717.png
    Screenshot 2025-03-27 125717.png
    225.6 KB · Views: 33
  • Screenshot 2025-03-27 125735.png
    Screenshot 2025-03-27 125735.png
    210.9 KB · Views: 25
  • Screenshot 2025-03-27 125756.png
    Screenshot 2025-03-27 125756.png
    18.3 KB · Views: 32
Back
Top Bottom