Lini vyama pinzani vitachukua madaraka?

Lini vyama pinzani vitachukua madaraka?

Kijana kijana

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2018
Posts
2,546
Reaction score
2,625
Toka nizaliwe wakuu nyerere yupo hai na kuna chama kilikuwa kinaongoza Nchi hii mpaka hivi leo.

Sasa najiuliza tu kwamba ni kweli wananchi bado hawajaamka miaka yote tokea tanzania ianze ?

Kimeshindikana nini miaka yote hii vyama pinzani visiingie madarakani?

Kama watu hawajaamka basi ni bora kuachana na siasa tu mana itakuwa huongei na watu bali wanyama,tokea pale bado tu hawajaskia?

Hivi kuna haja ya kujifanya mzalendo wa chama fulani kkuwapigania wananchi wakati huo unaweka maisha yako hatarini kwa watu ambao tokea enzi hizo wanaambiwa hivyo hivyo tuwatoe towatoe?

Tatizo nini wakuu,kuna haja ya kujiingiza kwenye siasa kwa ajili ya kuoindua chama ikiwa miaka mingi zaidi imepita haijawezekana?
 
Chama unachotaka kitolewe kimejichanganya na vyombo vya dola na vya maamuzi .

Kukitoa inatakiwa kujitoa mhanga .
Ni swala la kufa na kupona .
Hivi ni kweli kuna haja ya kupaza sauti kwa kuhatarisha maisha yako na familia kwa ajili ya mtanzania ambae tokea miaka ya 90 hajaweza kumtoa madarakani yule ambae anamuamini ni mbaya wake?
 
Nadhani vitachukua kuanzia 3018 - Miaka 1000 kutoka sasa, baada ya hawa wanaoviongoza vyama vya upinzani kwa kuangalia maslahi yao kuondoka.
 
Nadhani vitachukua kuanzia 3018 - Miaka 1000 kutoka sasa, baada ya hawa wanaoviongoza vyama vya upinzani kwa kuangalia maslahi yao kuondoka.
Mana sijawahi kuona rais mzuri upande wa wapinzani
 
Hivi ni kweli kuna haja ya kupaza sauti kwa kuhatarisha maisha yako na familia kwa ajili ya mtanzania ambae tokea miaka ya 90 hajaweza kumtoa madarakani yule ambae anamuamini ni mbaya wake?
Kwanini umetumia neno kuhatarisha maisha ktk hoja hii, kama kweli kuna nia njema ya ushindani wa kisiasa ?!
Manaake hao unaotaka watolewe hawajawahi kuwa na nia njema ktk ushindani wa kisiasa
 
Siku shida zikizidi sana hapo ndio utakuwa mwnzo
 
Kwanini umetumia neno kuhatarisha maisha ktk hoja hii, kama kweli kuna nia njema ya ushindani wa kisiasa ?!
Manaake hao unaotaka watolewe hawajawahi kuwa na nia njema ktk ushindani wa kisiasa
Hiyo kauli lazima itumike tu mkuu,sikuona kauli ingine ya kuweka.

Mimi sijataka watolewe mkuu,
 
Siku wazungu wakikatiwa mirija yao ya unyonyaji ndiyo utakuwa mwisho wachama kilicho madarakani. Na upinzani kupewa madaraka
 
Wapinzani watashika dola baada ya Tanzania kufikisha miaka 70 ya uhuru.
 
Back
Top Bottom