Lini Umewahi kusema"Ipo Siku" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lini Umewahi kusema"Ipo Siku"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magulumangu, Apr 10, 2010.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wakulu nimekuwa najiuliza kila mara kuhusu hili lakini no answer sijui na wenzangu mumewahi tokewa?Lini umekasirishwa na mwenza wako na kudiriki kumwambia wewe ngoja tu siku yako inakuja...mie nimewahi baada ya kupigwa mswaki wiki nzima madai yake kachoka na kazi,ilinibidi kusema vile kutikisa kiberiti lakini wapi mwendo ule ule tu ikabidi nitumie uzoefu lakini ngoma ikawa no way..sasa wazee hebu nisaidieni hapo..
   
 2. m

  mimi-soso Senior Member

  #2
  Apr 10, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  fafanua tafadhali, maana hii ipo siku nifahamuvyo mimi inasema katika mazingira mengi sana. Je wewe unazungumzia ya mazingira gani?
   
 3. K

  Kaseka Member

  #3
  Apr 10, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  " Ipo siku" na kauli zingine kama "we ngoja tu", "utanitambua siku moja" n.k. Nikauli zinazoashiria kuporomoka kwa hisia juu ya jambo fulani. Bila shaka unakumbuka kile kisa cha sungura na ndizi mbivu. Alianza kwa mbwembwe nyingi akizirukia na kuamini atazifikia. kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kuporomoka katika hisia zake juu ya ndizi. Mwisho kabisa alipotambua kwamba hawezi kuzifikai akasema " sizitaki mbichi hizi"

  Awali aliziona mbivu, baada ya kushindwa kuzipata akapoteza hamu na kutoa kauli ya kushindwa akiwa ameporomoka kihisia akatoa hiyo kauli. Kisa hakikuendelea, lakini kingendelea labda angefikia hatua ya kulia na hata kutoa machozi.

  Wewe baada ya kukutana na tatizo hilo uliangalia " a tip of the ice-berg" ukakivamia kama Titanic ukiamini utafanikiwa kukisogeza kumbe chini yake kuna tatizo kubwa sana ambalo huna budi kuliangalia. " Ipo siku" ni kauli inayo onyesha hisia uliyonayo juu ya mwenza wako, na hata akipona tatizo lake si ajabu likahamia kwako. kwani tayari umefikia ile hali ya kutaka kuadhibu, kutia maumivu ili ufanikishe mahitaji yako bila kujali anaye toa huduma hiyo.

  Pole sana Mkulu, inawezekana tatizo likawa si la mkeo bali ni lako na lina jionyesha kwa mkeo. Mwaka 2007 wakati nampeleka mke wangu kujifingua baada yakutoka nchini Kenya nilikokuwa kikazi. Hakika nilikuwa nimechoka sana kwani nilitumia usafiri wa basi. Ile nafika nyumbani tu namkuta mke wangu ananisubiri, nilichofanya ni kubadili nguo tu na kumpeleka hospitali. Tunafika pale Sinza, manesi wanasema presha ya mke wangu iko juu. Kwa sababu ninauelewa wa maumbile ya kihisia na kiakili ya binadamu, nilipinga hilo. Mke wangu hakuwa na historia hiyo, ila mimi ninayo. Nikatoa nje nikasimama chini ya mti na kuhesbu mapigo yangu ya moyo, ukweli ni kwamba presha yangu ndo ilikuwa juu. Nikaanza zoezi ya kuishusah nilipojiridhisha nikaludi ndani na kushauri wampime tena mke wangu kwani inwezekana walikosea........ Aaaa walistaajabu, saa tatu kasorobo usiku ule nikapata binti mwingine. Mambo ya maumbile ni mazito. Tafuta suluhisho kauli za NAMNA HIYO HAZITIBU KITU
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hili tatizo jamani mbona limekuwa kubwa mno! kila mtu ana lalama
  wasi wasi wangu ni wanaume kudhani kuwa mwanamke ndo chanzo cha tatizo na kushindwa kujitathmini yeye mwenyewe kwanza.
   
Loading...