Elections 2010 Lini Mrithi wa nyerere atapatikana?

segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Namkubali sana Nyerere kutokana na jinsi alivyokuwa kiongozi shupavu mwenye kuweza kumnyamazisha na kumpotezea yeyote yule,kipindi chake nidhamu ilikuwepo bwana.Watu walikuwa wapigwa ban za kutosafiri nje ya vijiji walivyozaliwa.Akikutaa hata ulikuwa unagombea cheo chochote cha kisiasa usingepata kama angekuwekea vigingi.Nilibahatika kusikia habari moja toka kwa rafiki yangu mmoja ambaye anatoka kijiji kimoja na JKN.Alisema kukuwepo na uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji hapo BUTIAMA.Wagombea walikuwa Mjeshi Msuguri na mwl wa shule ya msingi hapo kijijini.Nyerere alikuwa anataka Msuguri apate hiyo nafasi lakini alikuwa anafahamu kuwa hawezi akashinda kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki.Uchaguzi ulipokaribia JKN akasema uchaguzi utafanyika kisomi zaidi kura zitahesabiwa na kompyuta toka mjini.Siku ya uchaguzi msuguri akashinda kwa kishindo kwa mjibu wa kompyuta na Mwalimu akapata kura sita.Watu washangaa kwa sababu watu waliosema wamempigia kura yule mwalimu walizidi ile idadi.Nyerere akawambia wanaobisha kwamba yule mjeshi hakushinda,Mnabishana na kompyuta?? watu wakanywea.
Nyerere alituchagulia mwinyi kuwa rais,Mwinyi akachemka vibaya mpaka Nyerere mwenyewe kuingilia kati alipoona mambo yanaenda ndivyo sivyo.
Nyerere alituchagulia Mkapa,yeye mwenyewe akisema Mr.Clean,Kilichotokea kwa huyu mr clean ni kufanya biashara akiwa ndani ya magogoni ambapo ni kinyume kabisa cha katiba pamoja na kashfa nyingine zinazotutafuna hadi leo hii.
Kwa misingi hiyo Nyerere hakuwa na uwezo wa kupridict kuwa kiongozi anayemtaka angetimiza aliyokuwa amepenga.
Nani atamrithi Nyerere?
Ya kwangu ndo hayo kazi kwenu wanajamvi
 
Back
Top Bottom