tanga kwetu
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 2,193
- 1,434
kuna siku nilikuta Magufuli anaitwa Dr., sikubisha wala sikukubali bali nilishangaa maana 'no data no speaking' lakini nikafuatilia na kugundua jamaa kasota miaka minne pale UDSM na kupata PhD yake katika mambo ya chemical engineering. Siku za hivi karibuni vyombo vya habari (nime-notice hasa hasa ITV), zinamtambulisha Kikwete kama Dk. Kikwete (Pia Karume). Nimejaribu kufuatilia wapi kapata hicho cheti cha PhD au MD au BVM/DVM (Bachelor of Veterinary Medicine/Doctor of Veterinary Medicine) inaonekana ni Dr. ya vinginevyo. Naomba mwenye taarifa juu ya hili anijuze. Recently, wimbi la watu kujiita madokta limekuwa kubwa sana huko Tanzania. Inauma kama mtu hajasota kama ma-real Drs wanvyousotea kuupata u-Dr. halafu mtu anajipachika tu. Tena watu kama hao usipomwita Dr. anakasirika. Wenzetu huku Ulaya hawapendi kuitwa ovyo ovyo Dr....you just call him/her jina lake la kupewa utotoni...Condoleze Rice etc.