Afrika imewahi kuwa na mshindi mmoja tu wa Ballon d'Or, na huenda ikasubiri zaidi kuona mchezaji mwingine akifuata nyayo za George Weah baada ya orodha ya mwaka huu kutangazwa.
Nahodha wa Morocco, Achraf Hakimi, na mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane, ndio wachezaji wawili pekee kutoka Afrika walio kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo hiyo mwaka 2026.
Wachezaji hao wawili wamewahi kumaliza katika nafasi sita bora za Ballon d'Or, lakini baada ya mwaka ambao Hispania ilitwaa Kombe la Dunia la Fifa na Kylian Mbappe kufunga mabao 10 na kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya mashindano hayo, nafasi za Hakimi au Mane kutwaa tuzo hiyo zinaonekana kuwa ndogo.
Lakini Afrika imewahi kusubiri muda mrefu kabla ya kuona nyota wake akifikia kilele cha tuzo hiyo. Je, mwaka huu unaweza kuwa mwanzo wa sura mpya?
Hatuna shida nayo wao wawe wanatulipa vizuri tuu ili tuwatoe wadogo zetu Africa tuwapeleke kwao wajifunze soka mwisho wa siku tuje tutawale soka lao vizuri
Kama hawakupata Kina Drogba, Samwel Etoo na Tou're basi hawa wa sasa hawawezi hata kuwa nominated ijapokuwa majina yao yanawekwa kwa malengo fulani ya waandaaji wa Tuzo.