Lindi: Watatu wafariki kutokana na mapigano ya wakulima na wafugaji

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Watu watatu wamefariki dunia baada ya kutokea mapigano ya wakulima na wafungaji katika Kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa.

Tukio hilo limetoka juzi majira ya saa saba mchana baada ya mkulima Chande Magoma kumkuta mfugaji shambani kwake akilisha ngo'mbe mahindi yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutoa Kwa tukio hilo.

“Nikweli tuna tukio Kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa watu wawili, mkulima na mfugaji walipigana wakajeruliana hadi kupelekea vifo vyao wote wawili.”

“Leo (jana) asubuhi kundi la wanakijiji wakalipiza kisasi kwa kumuua kijana mmoja ambaye waliamini anatoka kwenye jamii ya wafugaji, tuna washikilia watuhumia zaidi ya hamsini kuhusiana na matukio hayo, hata hivyo kuna utulivu, baada ya viongozi ngazi ya mkoa na wilaya kufanya mkutano na wananchi,” alisema Kitinkwi.

Mwananchi
 
Wakiambiwa wafuge kisasa hawataki
Suruhisho ya hili Jambo Ni Kodi ya kila mfugo,Hawa ng'ombe wakitozwa shilingi 5,000/- kwa kila ngombe kwa mwezi ,wafugaji watalazimika kupunguza mifugo yao.

Ni ukweli usiopingika kuwa wafugaji Ni watu wabaya Sana,natokea jamii ya wafugaji but I hate them,Ni watu wa vurugu na viburi sana
 
Unajua athari ya kuongeza kodi? Kama vile wewe haitokuhusu?. Kwanini useme wafugaji ni wakorofi bila ya kujua changamoto za wafungaji nchi nzima?. Sera ya mifugo imeelekeza kila wilaya kutenga nyanda za malisho. Je Wilaya hiyo imefuata maelekezo hayo. Halafu Wakulima muda mwingi sana wanakuwa na wivu kwa wafugaji sababu ni chuki ya kipato.
 
Ccm hawana akili hata ukimwelewesha hawezi kukuelewa. Anakuambia ng'ombe watozwe kodi halafu kesho akienda buchani akakuta kilo ya nyama ni 20,000/- ataanza kubwabwaja.
 
Back
Top Bottom