LINDI MANISPAA: Tangazo la nafasi za kazi za Watendaji wa Mtaa Daraja la III, Deadline Mei 21, 2018

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
3,346
4,614
TANGAZO LA AJIRA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi anapenda kuwatangazia Wananchi kuhusu uwepo wa nafasi ya ajira ya Mtendaji wa Mtaa Daraja la III

MTENDAJI WA MTAA (NAFASI 11)

SIFA ZA MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III

i. Awe na Elimu ya kidato cha nne (iv) au sita (vi) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha , Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA

i. Afisa masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa
ii. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala bora katika Mtaa
iii. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Mtaa
iv. Katibu wa mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Mtaa
v. Kutasfiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
vi. Kuandaa Taarifa za utekelezaj wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji wa mali
vii. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Mtaa
viii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Mtaa.


NGAZI YA MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni TGS B

UTARATIBU WA MAOMBI
Maombi yote yaletwe yakiwa na nakala za vyeti halisi vya Elimu na Taaluma pamoja na
wasifu wamwombaji (CV).Pia maombi yaambatanishwe na namba za simu za mkononi
pamoja na picha ndogo mbili (Passport Size za rangi ) za hivi karibuni.

MUHIMU
Maombi yote yatakayoambatanishwa na Matokeo ya Kidato cha NNE (Result Slip)
hayatafanyiwa kazi.

Mamombi yote yatume kwa Anuani Ifuatayo

Mkurugenzi waManispaa,
S.L.P 1070,
LINDI.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe tarehe 21/05/2018


Satura, J.M
Mkurugenzi wa Manispaa
LINDI.


Kuona tangazo halisi pakua nyaraka ifuatayo
 

Attachments

  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA MTAA-MANISPAA YA LINDI.pdf
    101.7 KB · Views: 139

Similar Discussions

Back
Top Bottom