NDOTO KAVU
JF-Expert Member
- Feb 15, 2011
- 1,513
- 1,120
Kwa hiyo mzee unasubiri hadi akuharishie? duh kweli wanaume mna uvumilivu!!Ndugu zangu wanajf. Ninapenda kuwasilimia wote mabibi na mabwana. Nimefurahishwa sana na ushauri na mawazo manayotoa kwa kweli ni ya kujenga sio kubomoa. Shukrani.
Mimi ni kijana ambae nilibahatuka kumpenda binti mmoja na nilibahatika kuzaa nae mtoto mmoja tukiwa tunaishi nae pamoja kama miaka mitatu. Lakini baada ya kupata mtoto nikamwona bibie anabadilika kwa sababu dada zake wanauwezo. Mimi nilivumilia mambo mengi sana kiasi kwamba ilifikia kipindi ikawa tunasemana chumbani na kuombana msamaha yanaisha. Mimi mwenzio ninaumia kumbe yeye anapata raha tu na nikimuuliza hivi anajisikiaje labda anavyuniona kama ananipenda anajibu kama chizi ninakupenda kumbe ananingonga huku nyuma. Haya mambo ya simu ni historia ndefu sana kwangu na yeye kuhusu kijana mmoja tulie kuwa tumepanga nae nyumba moja. Na hili la simu nimelifuma mwenyewe live bila kuambiwa na mtu yeyote. Kama ni chakula cha mtoto alikuwa anapata kila siku isipokuwa siku ambazo anakua. Lakini tamaa inaendelea kumzidi. Ninasikia anachukuliwa na rafiki yangu mzee ambaye alifiwa na mke wakati sija toka huko Tz. Na mimi ninamwita ni baba kwa sababu mtu akisha kuzidi miaka 30 ni lazima umuheshimu. Na nilimweshimu kwa sababu alikuwa ni jirani yangu. Sina ukoo nae wala sio kabila langu.
Ubinafsi:
1. Amefuga mifugo kwa mtu bila kuniambia, na nimemuuliza akasema ni kweli alikuwa nazo hata kabla sijatoka huko na hela alipata kwa dada yake.
2. Amejenga nyumba bila kuniambia walipomuuliza wenzake ya kuwa baba watoto anajua alisema hataki nijue ni nyumba yake atapangisha kwa sababu anajua nitajenga nyumba na tutakaa. Baada ya kujua nimeshajua ndio akaaza kuniomba hela za kuchimba choo na kuanza kunieleza ameamua kujenga nyumba sijuii sababu haziishi. Nilipo muuliza amepata wapi hela anajitetea ametumia hela nilizokuwa ninampa za matumizi. Kweli nilishikwa na hasira nikampeleka mwanagu boding japo ni mdogo wa miaka 7.
3. Ana majibu kama kuku ambaye anaharisha.
4. Hapendi kusikia ninawasaidi ndugu zangu kabisa ilifikia kipindi kabla sijaja huku kawakejeli wazazi wangu, nikimwomba embu wasaidie kitu fulani anasema si uwasaidie wewe si wazazi wako, anasema sijamuowa kwa ajili wa wazazi au ndugu. Lakini ninashukuru mungu hakuna mtu yeyote anajua adha ninayoipata, sija wahikuwaambia hata wazazi. Ninasema hivyo kwa sababu anzia nimetoka huko mama yangu alikuwa anaumwa lakini alifika nyumbani kwao akawa anajificha mpaka akaondoka hakuwasalimia wazazi wangu kabisa.
Ninaomba ushauri ndugu zangu nifanye nini? Na mimi ndio nimemaliza masomo ninataka kurudi nyumbani, nianzie wapi maisha? Dada zangu wote wameshaolewa nimebaki na mdogo wangu wa kiume ambaye yupo sekondari.
Umeishi nae kwa muda wa miaka 3 hujaweka msimamo wa kufunga nae ndoa, ndio maana ameamua kufanya mambo yake bila kukushirikisha
pole sana, umefunga ndoa? kama umefunga ndoa vumilia, lakini kama hujafunga ndoa, hapo huna mke, tafuta mwingine.....atakuja akuchinje ukizipata huyo ili arithi..ametoka wapi kwanza, machame au mkuu?daa mkuu fasta shukuru Mungu bado unaishi naye kama mchumba wako(Kidini) kama umegundua hayo mapema mkuuu usifunge naye ndoa kabisaa, kuvunja uchumba si zambi!
Pole sand ndugu yetu. Mimi nitakushauri kama ifuatavyo; kwanza kabisa mwenza wako siyo mwaminifu; hili ni tatizo kubwa sana ambalo nafikiri liko juu ya uwezo wako. Huyu mtu bila maombi hawezi badilika kamwe ni kitu kiko damuni. 2. Kajenga nyumba bila kukwambia, hiyo inaashiria kwamba anahitaji nafasi ya kuishi maisha yake mwenyewe bila wewe. 3. Ana jeuri kwa umalaya wake, inawezekana wewe unachompa ni kidogo kwa kutumia mwili wake anaongezea pale ulipoishia wewe. 4. hana mapenzi na ndugu zako, ubinafsi mbaya sana ambao ki ukweli wale wote wenye roho hizo na wako kwenye ndoa huwa hawabadiliki. Mazingira waliyokulia ni ya kimaskini sana kiasi kwamba kila kitu kwake ni lulu, though kuna wengine ni tajiri wa mali na maskini wa roho.
Mimi nakushauri mwache tu aende zake, omba mtoto wako akue katiika mazingira mazuri, Mungu atakupa mke mwema. Kuanza maisha peke yako sidhani kama ni kitu kigumu unless wewe ukifanye kuwa kigumu. Make sure una muda na mtoto wako, usiingie kwenye mambo yanaitwa mapenzi kabla ya hujajua hata huyo utakayekuwa nae kama atampenda mwanao. Siku hizi mambo ni magumu, mtu anakubali kumpenda mwanao kwa sababu anataka aingie kweye ndoa akishaingia vimbwanga vinaanza. Simama katika imani huku ukiomba mungu kukupa hekima na busara za kulea mwanao.[/Q
Kaka umetoa ushauri mzuri sana .......hawa dada zetu wana matatizo sana kuna jamaa yangu mwaka jana kuja kushtuka nyumba imeshaisha ila aliachana na mkewe baadae