Hata mimi nimelea watoto bila mama lakini sikuwa nawabeba hivyo. Hapo amezidisha. Kwani mtoto ni lazima abebwe hivyo pamoja na mfuko wa akina mama mkononi? Mbona mwanaume akiigiza kusema au kutembea au kujiremba kama mwanamke tunamcheka?
Shida sio kubeba mtoto shida ni jinsi alivyobeba mtoto, wewe kama unabeba mwanao hivyo OK, hiyo ni wewe, lakini sio sahihi kwa mwanaume kubeba hivyo PERIOD.
siku hizi haki ni sawa.... sio ooh mwanaume suruali hana hela (sawa wababa nao wanafanya kazi zilizo dhaniwa ni za kina mama, na kina mama nao wafanye kazi wanazo dhani ni za kina baba )
Hheheheheee sorry, ila akili yangu imewaza kazi wanayofanya kina baba ni kutia watu mimba..... ambayo kina mama ndo waifanye au kukupa mzigo na kukususia nao na kuukataa au kuukana kama ni wake...