Limbu abwagwa tena Mahakama Kuu

Limbu abwagwa tena Mahakama Kuu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoketi leo chini ya Mtukufu Jaji Lugano Mwandambo imeahirisha kusikilizwa kwa maombi ya zuio la muda dhidi ya Mwigamba na wenzake na kupanga kusikilizwa kwa kesi ya msingi mnamo tarehe 15/4/2015. Kimsingi, Mwigamba na wenzake wataendelea na shughuli zote za chama hadi tarehe ya kusikilizwa kwa shauri hilo.


Kesi ya msingi ni kati ya Kadawi L. Limbu, Leopold Lucas Mahona na Grayson Manyori Nyakarungu dhidi ya Samson Mwigamba, Peter Mwambuja na Mohamed Masaga. Ni kesi ya madai nambari 17 ya 2015. Wadai waliwasilisha Maombi madogo nambari 21/2015 yakiomba, pamoja na mambo mengine, zuio la muda dhidi ya Wadaiwa-akina Mwigamba kutojihusisha na shughuli za ACT-Tanzania hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kuamuliwa. Maombi hayo madogo yaliondolewa (were struck out) kutokana na upande wa Wadaiwa kukubali kuwa Maombi yao yalikuwa na mapungfu ya kisheria hasa katika kuifanya Mahakama itoe kinachmbwa (to move the court).

Wadai-akina Limbu waliwasilisha maombi madogo tena nambari 129/2015 wakiomba zuio la muda dhidi ya Mwigamba na wenzake na wateule wao hadi kumalizika kesi ya msingi. Maombi hayo madogo mapya yalipangwa kusikilizwa leo. Mawakili wa Mwigamba wakiongozwa na Wakili Msomi Mwandamizi John Mnaku B. Mhozya, pamoja na kupokea maombi hayo leo,walidokeza mapungufu mengine ya kisheria katika maombi madogo mapya na kupingwa kusikilizwa kwa maombi hayo madogo mapya leo.

Jaji Mwandambo amekubaliana na hoja za Mawakili wa Wadaiwa na ameamua kuwa kesi ya msingi itatajwa tarehe 15/4/2015 na hoja za kisheria kupokelewa siku hiyo. Hivyobasi,Mwigamba na wenzake ambao ni Wadaiwa/Wajibu Maombi watendelea kujihusisha na ACT-Tanzania hadi itaapoamriwa vinginevyo.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoketi leo chini ya Mtukufu Jaji Lugano Mwandambo imeahirisha kusikilizwa kwa maombi ya zuio la muda dhidi ya Mwigamba na wenzake na kupanga kusikilizwa kwa kesi ya msingi mnamo tarehe 15/4/2015. Kimsingi, Mwigamba na wenzake wataendelea na shughuli zote za chama hadi tarehe ya kusikilizwa kwa shauri hilo.

Itaendelea.....
....Limbu alitumika tu kuaanzisha chama lakini wenye chama walipotaka chama chao akakataa kuwakabidhi ndio kesi hiyo.tUPO NDANI YA act tutajua wanapenya wapi,wanapitia wapi.
 
chama cha wasaliti na waliofukuzwa,viongozi wake wote watakuwa waliofukuzwa,sasa tuone wasaliti watajiongozaje?
 
limbu huna lako hapo!!! cha ni chakina zitto na mwigamba...acha kushika mapembe!!!
 
John MnakumbMhozya mgombea ubunge mtegemewa WA jumbo la Chalinze kupitia Chadema siyo❔➖eti PETRO E.Mselewa
 
Last edited by a moderator:
Amicu,joni naye ameingia huku?narudi "Kwa Kipofu"

Magwangala,

Mimi nimehusika kwenye hilo shauri kama wakili tu na si vinginevyo. Mwigamba na wenzake walikuja ofisini kwetu wakatupatia instructions za kuwawakilisha,nasi tumefanya hivyo kwa niaba ya wateja wetu na tunashukuru wameridhika na huduma na representation tuliyowapatia kama ofisi (Fortis Attorneys)
 
😁😂😁😁😁😁
 
Mayenga,

Mimi nimehusika kama wakili tu wa akina Mwigamba,si vinginevyo mkuu. Kama wakili ninapopata mteja tukielewana "fees" wajibu wangu ni kumuwakilisha mahakamani kwa kutetea kesi yake au kesi dhidi yake
 
Mayenga,

Mimi nimehusika kama wakili tu wa akina Mwigamba,si vinginevyo mkuu. Kama wakili ninapopata mteja tukielewana "fees" wajibu wangu ni kumuwakilisha mahakamani kwa kutetea kesi yake au kesi dhidi yake

Utafuata nyayo za Msando very soon kiongozi maana na yeye alijitetea hivihivi.

Ku-deal na watu wenye uelewa mdogo ni kazi sana,wanadhani maisha ni siasa tu yaani ukatae pesa kisa mteja wako amewahi kuwa na mgogoro na chama chako.
 
Ushauri wa bure kwa Kadawi L. Limbu, Leopold Lucas Mahona na Grayson Manyori Nyakarungu tulieni mjenge chama , msitoe njaa tumboni kupeleka kichwani mtaallibu akili.
 
Back
Top Bottom