Limao (ndimu) husaidia mwili kutengeneza damu

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Kwa mujibu wa USDA, limao (ndimu) huwa na mjumuiko wa nishati, protini, wanga, nyuzilishe, madini ya calcium, magnesium, phosphorus, potassium, sodium, zinc, copper, selenium na kiasi kidogo cha sukari.

8FC69B06-9A48-41B3-A48E-2C1B8618AC4B.jpeg


Aidha, huwa na vitamini C, citric acid, vitamini B12, folate pamoja na viondoa sumu vya carotene, vitamini E, lutein na zeaxanthin.

Utengenezwaji wa Damu
Madini ya chuma, folate na vitamini B12 hufanya kazi kwa pamoja katika kuwezesha utengenezwaji wa damu mwilini.

Aidha, vitamini C na citric acid huhitajika kwenye kuzuia tatizo la Anemia linaloweza kutokea baada ya mwili kushindwa kufyonza madini ya chuma yanayopatikana kwenye mlo kisha kusababisha upungufu wa damu.

Virutubisho hivi vyote unaweza kuvipata kwenye limao (ndimu) hivyo tofauti na jinsi inavyoamikika mitaani, matunda haya hayakaushi damu, bali huusaidia mwili kutengeneza damu pamoja na kuzuia upungufu wake.

Ni matunda mazuri kwa kila mtu, lakini zaidi kwa wale wenye changamoto ya upungufu wa damu mwilini.

Chanzo: United States Department of Agriculture (USDA)
 
Ukiingiza malaria (ambayo ipo nyingi tu mtaani) katika mlinganyo ndio unaweza kuona jinsi limao limekuja kuhusishwa na upungufu wa damu.

Ni kwa sababu linaishusha homa na linapambana mdogomdoogo sana na malaria hivyo matokeo yake mtu anapungukiwa damu kwa kukaa na malaria 'kiduchu' ndani ya damu kwa muda mrefu.

Je hii ni afya au sio afya ni jambo linabaki wazi kwa majadiliano
 
Back
Top Bottom