Like mother like daughter?

Like mother like daughter?

Noor

Senior Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
146
Reaction score
49
Mimi ni mkaka mwenye miaka 27 nilikutana na mdada mwenye miaka 24 facebook tukaanza kuchat na hatimaye tukafikia uamuzi wa kua wapenzi. Aliniambia hakuna kwenye mahusiano kama nilivyokua mimi. Siku aliyokuja kwangu kulala alikuja kwenye saa tatu usiku, nikamuuliza leo imekuaje hadi amepata muda wa kuja kulala kwangu akaniambia baba yake amesafiri, nikamuuliza kuhusu mama yake akanambia nae ameenda kwa marafiki zake. Nikawa na swali linaumiza kichwa kua paka akitoka panya anajitawala? Tukiwa bado tunaendelea na maongezi ya hapa na pale mama yake akampigia simu kuwa amuandalie nguo kwa ajili ya kesho kazini, atazipitia saa kumi na mbili wakati anaenda kazini. Nikamuuliza kwa hiyo mama harudi nyumbani leo akanijibu ndio maana yake, hawezi kurudi kwa sababu baba hayupo. Ilibidi aondoke usiku huo huo maana alikua hana jinsi ya kulala wakati mama yake atapita mapema.

Je huyo anafaa kua mke maana toka nilivyojua tabia ya mama yake na yeye sihitaji hata kumuona. naomba mnishauri nifanyeje?
 
mmmmmhh, ngoja kwanza nadhani hii haijatulia inafaa kuanza nayo asubuhi nikiwa na akili iliyochangamka, nitarejea kaka
 
Inaelekea anasapoti ujinga anaofanya mama yake na ni rahis yeye pia kufanya hivo..
 
Mimi ni mkaka mwenye miaka 27 nilikutana na mdada mwenye miaka 24 facebook tukaanza kuchat na hatimaye tukafikia uamuzi wa kua wapenzi. Aliniambia hakuna kwenye mahusiano kama nilivyokua mimi. Siku aliyokuja kwangu kulala alikuja kwenye saa tatu usiku, nikamuuliza leo imekuaje hadi amepata muda wa kuja kulala kwangu akaniambia baba yake amesafiri, nikamuuliza kuhusu mama yake akanambia nae ameenda kwa marafiki zake. Nikawa na swali linaumiza kichwa kua paka akitoka panya anajitawala? Tukiwa bado tunaendelea na maongezi ya hapa na pale mama yake akampigia simu kuwa amuandalie nguo kwa ajili ya kesho kazini, atazipitia saa kumi na mbili wakati anaenda kazini. Nikamuuliza kwa hiyo mama harudi nyumbani leo akanijibu ndio maana yake, hawezi kurudi kwa sababu baba hayupo. Ilibidi aondoke usiku huo huo maana alikua hana jinsi ya kulala wakati mama yake atapita mapema.

Je huyo anafaa kua mke maana toka nilivyojua tabia ya mama yake na yeye sihitaji hata kumuona. naomba mnishauri nifanyeje?

Hiyo ndiyo tabia yake halisi, kazi ni kwako!

Msichana yeyote mwenye tabia nzuri asingeondoka nyumbani usiku kwa lengo la kulala kwa mpenzi kwa kutoroka kwa kuwa mama yake hayupo nyumbani. Atakapokuwa mkeo hatashindwa kwenda kwingine kama mama yake anavyofanya. Kusanya vilago, kimbiaaaa!
 
homa huanza na dalili nahizo ndo dalili.......
 
An ounce of prevention is worth a pound of cure...
Wewe mwenyewe ushamuona like mother like daughter unategemea nini hapo??....
Every picture tells a story..chukua hatua!!
 
Malezi yanatoa picha ya tabia mtu...huu wala sio utabiri...ni hali halisi. ..
 
Nahisi hafai ndio maana nimeuliza ili nipate mchango wenu ili nifanye maamuzi sahihi
 
Ina maana baba akiondoka mama nae anaondoka na pia mtoto nae anaondoka, sasa siku ukimuweka ndani ukiondoka wewe na yeye anaondoka na pia binti yenu anaondoka du changanya na zakwako hapo maana mtoto wa nyoka ni nyoka tu
 
duh,hivi kumbe kuna watu wana tongozana facebook?
 
Hiyo ndiyo tabia yake halisi, kazi ni kwako!

Msichana yeyote mwenye tabia nzuri asingeondoka nyumbani usiku kwa lengo la kulala kwa mpenzi kwa kutoroka kwa kuwa mama yake hayupo nyumbani. Atakapokuwa mkeo hatashindwa kwenda kwingine kama mama yake anavyofanya. Kusanya vilago, kimbiaaaa!

kweli jf kila mtu ni mtakatifu ,hizi ishu za kutoroka nyumbani na kulala kwa wanaume mbona ni common sana kwa watoto wa kike kila wapatapo nafasi.
 
Duu huyo baba angejua yan akiondoka mama anaondoka,bint anaondoka probably hata kaka anaondoka
Tupa kuleeee

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Naona umejipa jibu mwenyewe!

Unaweza fanyiwa kama anavyo fanyiwa baba yake!

Nahisi hafai ndio maana nimeuliza ili nipate mchango wenu ili nifanye maamuzi sahihi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom