Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 257
Kuna mambo yanashangaza sana katika soka letu. Inashangaza kwa sababu, wakati dunia ya sasa ikimulika zaidi mafanikio katika mifumo ya kisayansi, sisi tumebaki kule kule.
Wenzetu wamejitahidi kuifanya dunia kuwa kama kijiji, wamefanikiwa. Sasa wanapiga hatua zaidi za kuifanya dunia bali mtaa. Sisi wala hatushtuki, tunataka mambo yale yale ya zamani. Mawasiliano ya barua, karatasi, stempu na kalamu. Tunataka kuona barua tunayoiandika leo na kuituma Mwanza, basi ifike baada ya siku saba.
Tunazidi kujikita kwenye sayansi ya giza. Tunataka mafanikio ya haraka kupitia usafiri wa ungo. Kifaa hiki ndicho tunakiona kinaweza kutufikisha tunapotaka kwenda kwa kasi kubwa kuliko ndege.
Nilisema inashangaza, kweli inasikitisha. Hivi hadi leo hii kuna timu zinasaka ushindi kwa njia ya kuloga? Yaani, viongozi, makocha na wachezaji wanategemea matokeo kupitia ushirikina?
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwishoni mwa wiki iliyopita lilitangaza kuzipiga faini timu za Simba na Coastal Union kwa sababu ya kushiriki vitendo vya ushirikina muda mfupi kabla ya mechi ya Ligi Kuu.
Timu hizo zinadaiwa kufanya matendo hayo kwenye vyumba vya kubadilisha nguo kwa kumwaga maji kama sehemu ya dawa ya kufanikisha kile kinachoonekana kuwa ni ushindi wa kishirikina. Nilichoshangaa zaidi ni kwamba, sijasikia kiongozi yeyote wa timu hizo akipinga adhabu hiyo. Maana yake, wamekubali kushiriki ushirikina ili kupata ushindi.
Ila ajabu ni kwamba, Coastal Union wamelalamika TFF wakidai kufanyiwa vitendo vya ushirikina katika mchezo wao dhidi ya Mbeya City na kufungwa bao 1-0. Hawajapinga tuhuma kama hizo dhidi ya Simba.
Hivi kweli bado tuko kwenye dunia, ambayo tunaendelea kudhani ushindi uwanjani hauwezi kupatikana bila kuloga?
Niliwahi kuandika wakati fulani kwamba soka la nchi yetu linauawa kutokana na kuendelea kuwapa nafasi viongozi wabovu na wasiokuwa na ubunifu wa kisayansi kama ilivyo kwa wenzetu.
Ni hao hao wanaotumia fedha nyingi na muda pia kwenda kwa waganga kutafuta njia za mkato za ushindi kupitia ushirikina. Kama klabu hizo zinaamini ushindi ni lazima kuloga, kwa nini sasa zilitumia fedha nyingi kusajili wachezaji wazuri?
Adhabu ya Sh500,000 kwa timu zinazoshiriki mambo ya ushirikina haitoshi, nadhani TFF ingewafungia kushiriki soka viongozi wa klabu watakaobainika kushiriki vitendo hivyo.
Naamini na nitaendelea kuamini kwamba, ni kizazi kipya tu cha viongozi wenye mwanga wa mafanikio kisayansi, ndicho kitakachotutoa kwenye utamaduni huu wa aibu. Ligi ya ushirikina hutoa matokeo ya kishirikina.
Mwananchi