Ligi Kuu Bara : Simba SC vs Azam FC

Danny greeny

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,856
1,645
Leo ni muendelezo wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba na Azam FC utakaopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa. Live update zote utazipata hapa hapa jf kupitia uzi huu. sembo, Katavi, Crashwise, Mdakuzi, Cynic tuwe pamoja kwa muda wote mwanzo mpaka mwisho wa mchezo.
***************************************
FULL TIME : SIMBA SC 0 - 0 AZAM FC

Dk 87, Majegwa anapoteza nafasi nzuri kwa Simba, badala ya kutoa krosi, anampa mikononi kipa Manula

Dk 86, Tchetche anajaribu shuti lakini Agbani anadaka kwa ulaini kabisa

Dk 84, Nimubona anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliokuwa unakwenda langoni mwake na kuwa wa kurushwa

Dk 80, nafasi nyingine Simba wanapoteza kwa papara baada ya beki wake Nimubona kupiga shuti kubwa wakati angeweza kutuliza na kutoa pasi ndani

DK 79 Azam wanapata kona, inachongwa na Mcha lakini inakuwa ni moja ya kona zisizo na madhara ambazo Azam FC wamepiga mpaka sasa

Dk 78, Awadhi Juma anaweka vizuri mpira, akiwa katika nafasi nzuri anaachia shuti ambalo halina madhara yoyote

SUB Dk 76, Azam FC wanamtoa Mugiraneza na nafasi yake inachukuliwa na Bolou Tchetche

Dk 75 bado Mugiraneza na Agbani wako wanatibiwa

SUB Dk 73, Simba wanamtoa Juuko na nafasi yake inachukuliwa na Brian Majegwa

Dk 71, Mudathiri anaachia shuti kali lakini Agbani anadaka kwa umahiri mkubwa.

Dk 70, Bocco tena, anawapiga chenga mabeki watatu wa Simba, anapiga shuti safi kabisa, Agbani anapangua

Dk 67 Bocco tena, yeye na kipa wa Simba, anauchop mpira lakini unatoka nje kidogo

Dk 66, Nimubona anaokoa shuti la Bocco lililokuwa linajaa wavuni. Kona, inachongwa lakini haina lolote

Dk 55 zinaibuka vurugu baada ya Kiiza kumpiga teke Sure Boy naye naye akamkanyaga akiwa pale chini


Dk 52, Manula anafanya maajabu yake tena, anapangua faulo maridadi kabisa Tshabalala na kuwa kona ambayo haina madhara kwa Azam

SUB Dk 51, Hijja Ugando anaingia kuchukua nafasi ya Daniel Lyanga ambaye Ameumia

SUB : Mudathiri Yahaya anaingia kuchukua nafasi ya Singano 'Messi' ambaye hakuonekana kabisa kipindi cha kwanza

Dk 47, Bocco anajaribu lakini kwa mara nyingine Agbani anakuwa makini
Dk 46, Azam FC wanaanza kwa kasi zaidi lakini Simba wanaonekana wako makini na hilo


HALF TIME : SIMBA SC 0 - 0 AZAM FC

Dk 42, Manula anafanya kazi nyingine ya ziada na kudaka mpira kichwani mwa Kiiza

Dk 41, MWantika anafanya kosa, Kiiza anauwahi lakini Manula anakuwa na spidi zaidi anaokoa unakuwa wa kurushwa

KADI Dk 36, Aggrey analambwa kadi ya njano kwa kumrukia kwa makusudi Kiiza

Dk 33, Mwamuzi Akrama anamuonya kwa maneno nahodha wa Simba Jonas Mkude kwa kumwangusha Kipre tchetche

Dk 29 Mwalyanzi anamwangusha Aggrey Morris, mwamuzi Mathew Akrama anamfuata akitaka kumpa kadi ya njano, lakini anagundua amesahau. Analazimika kwenda kuifuata kwa mwamuzi msaidizi, anarudi katika dakika ya 30 na kumlamba Mwalyanzi kadi hiyo ya njano

Dk 28, Simba ndiyo zaidi wanamiliki mpira na zaidi ni katikati ya uwanja. Washambuliaji wake na viungo kama Mwalyanzi na Lyanga wanaonekana hawako makini kama utalinganisha na wale wa Azam FC wanaoonekana wana njaa ya mabao

Dk 25 sasa, Simba wamepiga kama pasi 28 hivi lakini mwisho wameishia kwa shuti dhaifu la Awadhi Juma

Dk 22, MWantika analazimika kulala na kuutoa mpira usimfikie Mwalyanzi, inakuwa kona. Inapigwa lakini haina faida kwa Simba

Dk 21 sasa, Azam FC ndiyo wamefika langoni mwa Simba mara nyingi zaidi. Lakini hawako makini katika umaliziaji

DK 19, Mwantika anafanya kosa kubwa, Kiiza anauiba mpira lakini kipa Manula anauwahi na kuokoa hatari ktk lango la Azam

Dk 15, kiungo Sure Boy wa Azam FC anaonekana kuwa na mwendo mzuri na kuifanya Azam FC kutawala mchezo zaidi hasa katikati

Dk 11, nafasi nyingine kwa Azam FC lakini Bocco tena anapiga kichwa dhaifu kama kile cha kwanza

Dk 8, Azam FC wanaendelea kushambulia, Bocco anapokea krosi safi lakini anapiga kichwa fyongo

Dk 7, Mcha anabaki yeye na kipa Agbani wa Simba, lakini anampa mikononi

Dk 2, Lyanga amapiga shuti Manula anapangua na kuwa kona, inachongwa Kiiza anapiga kichwa lakini Manula anapangua tena

Dk 1 mechi imeanza taratibu huku kila timu ikionekana iko makini na Azam FC inacheza zaidi katika eneo lake, Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Azam FC lakini ni goal kick.
***************************************
FULL TIME: Simba SC 0 - 0 Azam FC
 
Asante sana mkuu kwa kuanzisha Uzi Na natumaini utatushushia updates pamoja Na wadau wengine watakaokuwa wanaona laivu mechi.

#ubingwamsimbazi ushindi Leo lazima.......:D:D
 
Kikosi cha Simba dhidi ya Azam FC leo...
1. Vincent Agban
2. Emery Nimuboma
3. Mohammed Tshabalala
4. Juuko Murshid
5. Novart Lufunga
6. Justise Majabvi
7. Awadh Juma
8. Jonas Mkude
9. Hamis Kiiza
10. Danny Lyanga
11. Peter Mwalyanzi

BENCHI:

Peter Manyika
Mohammed Fakhi
Hassan Ishaka
Brian Majwega
Mussa Mgosi
Raphael Kiongera
 
DONDOO ZA AZAM FC

Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Majimaji ya Songea (2-0) mabao yote yakifungwa na kiungo Mudathir Yahya.

Azam FC itawakosa wachezaji wengine kama kiungo Frank Domayo, Allan Wanga, Racine Diouf, Shomari Kapombe, ambao ni wagonjwa huku Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, akiendelea kukosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata wakati timu hiyo ikiichapa Mtibwa Sugar bao 1-0.

Mchezo wa kwanza baina ya Azam FC na Simba SC katika mzunguko wa kwanza uliisha kwa sare ya mabao 2-2, Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ akifunga mabao yote, wakati Ibrahim Hajibu alifunga ya Simba mabao.

Huo utakuwa mchezo wa 16 kuzikutanisha timu hizo kwenye ligi tangu Azam FC ipande msimu wa 2008/2009, Azam ikishinda nne, Simba saba na kutoka sare mara nne.
 
Back
Top Bottom