Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Niko 77 na ndiyo kwanza kunakucha huniambii kitu ng'wanawane 😁💪

Hizi ni perception za jamii tu ili pengine kuwatia hamasa na kuwaasa walioko huku nyuma wasikakawane kwenye nira za ujana bali wamakinikie zaidi kuanza maandalizi mapema maana ukifika huko 40+ hata process nyingi za mwili zinaanza kukuwashia indiketa kuwa sasa tunahama kwenye msimbo wa ujana na tunaingia kwenye utu uzima sasa.

Hii ni sawa tu na ile perception kwamba eti binti akivuka miaka 30 hajaolewa basi jua lake jema na lililong'aa sana hapo nyuma sasa linaingia machweoni. Na kuna mabinti wasiojitambua ambao kweli wakivuka 30 na bado hawajaolewa wala kuwa na familia wanapaniki badala ya kutulia na kuwekeza katika wao kama wao. Hata katika hili wapo wengi tu wanaofikia hiyo 40+ huku ramani za maisha bado zipo zigzag wanapata sonona hasa wakijilinganisha na baadhi ya waliosoma nao ambao wanakuwa wameshapiga hatua kubwa.

Binafsi kama ningeambiwa leo hii muda urudishwe nirudi huko kwenye 40s kitu pekee ambacho ningekirekebisha ni kuutunza mwili na kujali afya yangu sana. Nisingekunywa mipombe kupindukia na minyama choma hii. Japo ukiwa kijana huwezi kuona madhara yake, ukivuka 45 huku ndiyo sasa utaona kosa ulilofanya - na hapo kama una bahati hujapata presha, kisukari, matatizo ya figo, magonjwa ya moyo na ishu zingine kibao.

Miaka ya 40....kijana linda sana afya yako. Kila kitu kifanye in moderation (ikiwemo ulaji wa mbususu na hata CHAPUTA). Mengine yote ni madogo tu hasa kama unajitambua.

Hint: Usijilinganishe na classmates wako. Hypertension itakuhusu ufe mapema uache makorokocho yako yote uliyoyahangaikia kwa kujinyima sana 😁😁🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🖐

 
Asiwadanganye mtu wanangu. Maisha yanakuja jinsi yalivyo na hakuna wa kujua kesho. Hiyo 40 kama utafika ni uwezo wake Mola kwa wanaoamini hili

Wengi mna bahati kwa sasa kupata nasaha na kushauriwa humu, wengine wamekula maisha bila kujua
Wengine pia hata umshauri vipi bado atakula Bata bila kuwaza kuwekeza

Mimi sikuwa mtu wa starehe bali ni mtu wa kusafiri sana na kuiona Dunia, yaani ndio hobby yangu ila sasa nimepunguza kiasi ingawa bado nasafiri.

Vijana kuweka akiba ni muhimu sana na 40 isiwatishe kwani nina over 60 na bado napiga kazi sana
Nani kawaambia ukifika 46 umezeeka sio kweli.

Pigeni kazi sana mkiwa vijana ili msiwe watu wa kuomba omba baadae.
 
Kwa Tanzania hiyo principle haifanyi kazi.

Mtu anamaliza chuo at 30.

Anapata kazi at 35.

Anaoa at 36

Hiyo forty inakuwaje?
 
Mi naona Life begins at 25, ukifika miaka 25 akili zote za utoto zinakuwa zimeisha huwazi tena kupiga picha kali, kucheza games, kama ramani hazijakaa sawa na una akili timamu hata usingizi huwa unakata katkat ya usiku wa manane.

Na ukiendekeza mitandao ya kijamii unaona vijana wa umri wako wametoboa unaweza kujikuta hata furaha unakosa kabisa, ni umri mgumu sana vijana wengi wanajitoa uhai hapa 25-35, kwasababu changamoto za maisha zimeanza rasmi.
 
At 25 career wise bado, family bado, maendeleo bado, huenda hata shule bado kumaliza.
 
Sijasema at 46 umezeeka, ila wanasema umri huo upo katikati ya lifespan yako, nguvu na akili zipo kwenye peak yake.

Tatizo ni kujipanga hasa ukiwa kijana, kuna vitu vya msingi mtu anatakiwa kuviangalia ili mambo yasije kuwa mengi katika umri fulani.
 
Tofauti utaiona ukiwa apeche alolo, majukumu ni mengi yanakuangalia huna jinsi ya kusolve unajiona hopeless...ukiwa na ukwasi 40 is just a number.
 
Wewe subiri kidogo, wanasema wakati unaapproach 40 unapata stress za uzee, imewahi kukutokea? Au ndio vile maokoto sio haba huna stress?
Frankly speaking Sina stress hata kidogo za uzee wala sioni aibu kusema nikaapproch 40....Nina stress mambo yangu ya pesa yakienda ndivyo sivyo only that!
40 ni poa sana Eroni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…