Ila Mkuu, kutunza hela ni moja kati ya njia rahisi kabisa ya kuwa maskini.Tunza kibunda chako.
Kwa nini??Ila Mkuu, kutunza hela ni moja kati ya njia rahisi kabisa ya kuwa maskini.
...hivi miaka 40 bado ni kijana?
Kwamba mtu akiwa 40+ awe tayari amewekeza na pesa zinamfuata tu mkuu? Sasa mbona wengi wetu ndio tunaanza kujitafuta, tulichelewa either kusoma, kupata watoto, kuwekeza...Tafuta hela ukiwa kijana, ikifika 40+ maisha yaanze kwa kutumia ulichochuma...
Sababu pesa ni chombo cha kufanyia kazi kiuchumi, sasa kukiweka ndani ni kuzuia kufanya kazi hivyo ni sawa na kuwa na shamba usilolimaKwa nini??
Miaka 40+ wanasema umefikia peak ya graph ya maisha.Kuna kuishi na kuishia, nafikiri ukifika 40 unaianza safari ya kuishia duniani. Ila ukifika 30 unatakiwa kuwa umeanza kufanya kilichokuleta duniani.
Na ukiwa 20-29/30 hapo unatakiwa kuishi, huna stress, unazo nguvu zakutosha kuzurura, una uwezo wa kupata furaha kwa jambo dogo (mizuka).
Japo hii sio kwa wote maana kuna watu wana muaka 16 na wana stress zakutosha plus majukumu, ila kwa wengi au standard ya kidunia huo nivumri wa kuishi yaani kufurahia uwepo wako hapa duniani bila stress kali.
Ukifika 45 watoto wako watakuwa na umri gani mkuu.?Ni kweli Maisha yanaanza 40, umri huo unategemewa uwe umejiandaa na uzee, umeshawekeza, unamalizia malizia vitu vidogo vidogo ili ukifika 50 upumzike ule mafao, uenjoy maisha yaliyobaki, ujiandae na magonjwa na jinsi ya kupambana nayo,
Ukifika 40, bado huna ramani lazima hofu ikuingie, uwe depressed na wengi huanza kukata tamaa kwa kujihisi ndio basi, kumbe 40 inakupa last chance ya kupambania kujiandalia 50 yako,
Wito wangu kwa vijana tupige kazi bila kuchoka, fainali uzeeni.