Lifahamu jeshi la Israel na MOSAD

Lifahamu jeshi la Israel na MOSAD

Tanzanite klm

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
478
Reaction score
411
HISTORIA YA TAIFA LA ISRAEL TANGU 1948 NA VITA VITA KUU ILIZOPIGANA.

UTANGULIZI

Katika karne ya 19 idadi kubwa ya Wayahudi waliishi katika maeneo kadhaa ya Milki ya Urusi yaliyotwaliwa na milki hiyo mnamo 1800.

Uadui dhidi ya Wayahudi ulitokea katika utawala wa Kirusi. Kuanzia mwaka 1880 kulitokea ghasia mbalimbali ambako Wayahudi walishambuliwa katika miji ya Urusi. Wimbi la pili la ghasia hizo zilizoitwa pogromu zilikatokea mwaka 1905, ambapo Wayahudi zaidi ya 2000 waliuawa mjini Odessa .

Wakati ule Wayahudi wa Urusi walianza kuhamia nje: wengi wao walikwenda Marekani, lakini wachache walielekea Palestina.
Mapogromu yalikuwa pia chanzo cha harakati mpya ya Uzayuni (Zionism) kati ya Wayahudi wa Ulaya. Uzayuni ulilenga kuwapa Wayahudi eneo maalum ili wapate kujenga upya taifa katika dola lao wenyewe, ambako wangekuwa wenyeji, si kundi la pekee katikati ya watu waliowadharau.

Mwaka 1896 Theodor Herzl (1860-1904) aliandika kitabu "Dola la Wayahudi" alimodai kuundwa dola la pekee kwa ajili ya Wayahudi. Mkutano wa kwanza wa wafuasi wake ulichagua jina la "zion" ambalo lilikuwa jina asilia la mlima wa hekalu mjini Yerusalemu; wakachagua jina hilo kwa sababu linataja mahali patakatifu zaidi pa Uyahudi.

Mkutano huo uliazimia kuwa "Uzayuni unalenga kuunda makazi salama yaliyokubaliwa rasmi kwa ajili ya taifa la Kiyahudi katika nchi ya Palestina".

Wazayuni walikusanya pesa kote Ulaya wakanunua ardhi katika Palestina na kuanzisha vijiji kwa ajili ya Wayahudi waliohima huko.
Palestina katika Milki ya Ottoman mwaka 1914

Vita ya Kwanza ya Dunia ilikwamisha mipango yote kwa sababu Palestina ilikuwa sehemu ya Milki ya Ottoman iliyoshiriki katika vita pamoja na Ujerumani na Austria dhidi ya Urusi, Ufaransa na Uingereza.

Mwaka 1917 wakati ambapo jeshi la Uingereza lilifaulu kusogea mbele kutoka Misri na kuingia Palestina, waziri wa mambo ya nje Arthur James Balfour alitoa tamko la Balfour yaani tamko rasmi kuwa Uingereza inataka kusaidia mipango ya kuanzisha makazi ya Kiyahudi katika Palestina. Wakati uleule Waingereza waliwaahidi Waarabu kuundwa kwa dola la Kiarabu kwenye maeneo yaliyokaliwa nao katika Milki ya Ottoman. Lakini wakati huohuo walipatana na Ufaransa kuhusu ugawaji wa maeneo ya Kiarabu ya Milki ya Ottoman.

Kwenye mkutano wa amani wa Paris wa mwaka 1919, ulioandaa Mkataba wa Versailles, mwakilishi wa Waarabu, Faisal bin Hussein bin Ali al-Hashimi, alipatana na mwakilishi wa Wazayuni, Chaim Weizmann, kuwa anakubali uhamisho wa Wayahudi kuja Palestina, na Palestina kuwa eneo la pekee tofauti na Dola la Waarabu ambayo Faisal alilenga kujenga Uarabuni pamoja na Syria na Irak. Haki za wakazi Waarabu zilitakiwa kulindwa na maendeleo ya pamoja kati ya wakazi Waarabu na Wayahudi kujengwa.

Karibu inbox tukuunge na telegram group kwa simulizi za sauti
 
Back
Top Bottom