Katika Sony Tv inayopatikana katika visimbuzi vya dstv kuna Tv show inaitwa Trisha. Miongoni mwa yanayojadiliwa katika kipindi hicho ni hasa mambo yahusuyo familia kama vile watu kusingiziwa watoto kuwa wa kwao ilhali sio. Usaliti katika ndoa na mambo yanayofanana na hayo.
Kilichonifanya niandike thread hii ni namna wanavyomgundua msaliti wa ndoa au mtu yeyote anayetoa taarifa za uongo. kinachofanyika mtuhumiwa wa kutoa taarifa za uongo anavishwa nyaya kadhaa kifuani mikononi na kichwani na nyaya hizo huingizwa katika kompyuta yenye software maalum yenye uwezo wa kugundua kama kinachosemwa ni uongo au ni kweli "Lie detector software" Hivi utaalam kama huu ukija huku kwetu bongo watu wengi si wataumbuka?Wake za watu, waume za watu, viongozi wanaoomba kura kupitia kampeni zao za kimagumashi si wataaibika au mnalionaje hili Great thinkers?