Mpendwa, nakubali kabisa ni vema kutafakari kabla ya kupindua utaratibu kama tunataka kweli yale yanayofuata na tukibomoa utaratibu - je kuna mpango wa baadaye?
Ila tu picha yako ya Paradiso Libia chini ya Gadafi inaoekana ni tofauti na Walibia wengi. Ajabu? Nchi ilijaa watu maskini kutoka nchi za Afrika (waliokuwa na maisha mabaya) ilhali asilimia ya vijana wake wenyewe walijaribu kwenda nje.
Kufuatana na factsheet ya world bank
http://siteresources.worldbank.org/INTPROSPECTS/Resources/334934-1199807908806/Libya.pdf kabla ya mapinduzi walikuwa Walibia 110,000 walioondoka nchini mwaka 2010. Hawakuenda UAE bali nchi nyingine zinazotajwa.
Je umeshauliza kama labda wakati wa Gadafi serikali ya UAE haikutaka Walibia kutokana na uhusiano mbaya kati ya Gadafi na Waarabu wengine?
Ilhali sasa mlango umefunguliwa ?