flulanga
JF-Expert Member
- Jul 1, 2016
- 4,861
- 6,342
Habarini ndugu zangu,
Mimi nina goli la huduma za kipesa kama M-Pesa, Tigo na Airtel Money. Hapo awali nilikuwa kwa mwezi naingiza sio chini ya laki 5 ila kwa sasa biashara sio nzuri nimeshuka hadi laki 4 mpaka 380.
Na yote hii imechangiwa na kuongezeka kwa watoa huduma kama yangu hapa jirani maana kwa haraka haraka nimepata majirani sio chini ya watano ndani ya muda mfupi.
Sasa ninachokiona kwa kipato hiki nisipojiongeza nitachelewa sana kufikia malengo yangu.
Kwa hiyo sasa najiuliza nifungue goli jingine kama hili au nifungue library (kuuza CD na kuingiza nyimbo na movie kwenye flash).
Hii biashara sina uzoefu nayo na wala sina mtu ninayemfahamu anafanya hii biashara zaidi huwa nawaonaga tu.
Mtaji wangu nilionao wa kuanzia ni shilingi Milion 1 ila uwezekano wakuongeza japo kidogo upo.
Ninaomba wenye uzoefu wa hii biashara ya library watiririke ili nipime kati ya hii nayoifanya maana hii nayoifanya nina uzoefu nayo kwa asilimia kubwa maana ndio biashara yangu ya kwanza katika maisha yangu.
Karibuni
Sent using Jamii Forums mobile app