LHRC yalaani polisi kumdhalilisha mwanamke Igunga

  • Thread starter Ng'wanza Madaso
  • Start date

Ng'wanza Madaso

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Messages
2,278
Likes
100
Points
160
Ng'wanza Madaso

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2008
2,278 100 160
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimelaani kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi nchini cha kumdhalilisha mwanamke mmoja ambaye alikuwa akifanya maandamano ya kushinikiza kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, mkoani Tabora.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Ofisa Ueleweshaji Umma, Jinsia na Watoto wa LHRC, Edna Lushaka, alisema kitendo kilichofanywa na polisi wanaume ni cha udhalilishaji, kinyama na kinyume na kanuni za adhabu.

Alisema kisheria polisi wana uwezo wa kuwakamata wananchi, lakini sio kwa kutumia nguvu ya ziada na kwamba sheria inaruhusu polisi wa jinsia inayofanana na mtuhumiwa kumpekua endapo anatuhumiwa.


"Kitendo cha polisi wa kiume kumbeba juujuu na kumweka kwenye gari mwanamke yule, ni udhalilishaji wa haki za binadamu na si sahihi," alisema.

Naye Mkuu wa Huduma za Polisi Jamii, Isaya Mngulu, alikiri kuwa si sahihi kwa polisi wa kiume kumnyanyua mtuhumiwa mwanamke na kwamba kitendo hicho kilifanywa baada ya kutokuwepo polisi wanawake katika eneo hilo la tukio.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, alishangazwa na kitendo cha Baraza Kuu la Kiislamu nchini (BAKWATA), kukaa kimya bila kuzungumzia tukio hilo wakati katika tukio la kudhalilishwa kwa Mkuu wa Wilaya, Fatma Kimario, walitoa tamko.


"Nilitegemea BAKWATA leo watatoa tamko kwa kuwa mwanamke amedhalilishwa. Hapo ndipo tutajua BAKWATA wanatetea haki za watu au walikuwa na ajenda yao nyingine. Huwezi kulinganisha kitendo cha jana na kile cha hijabu," alisema Dk. Slaa.Chanzo: HAPA
 
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
1,675
Likes
6
Points
0
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
1,675 6 0
Watoe tamko kwani kuna manufaa kwao au kwa Magamba?

Hawa si matarumbeta ya magamba haya na hakuna tarumbeta la kupiga kelele kinyume na anaelimiliki.........ni ndoto
 
K

Kakalende

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2006
Messages
3,256
Likes
46
Points
135
K

Kakalende

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2006
3,256 46 135
Msitake kumchomekea Dr Slaa, wale jamaa wakianza ugomvi wao hauishi!
 
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,249
Likes
4,678
Points
280
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,249 4,678 280
Thread imebadilishwa heading na posts zangu wamechakachua duu!!
 
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Likes
720
Points
280
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 720 280
Thread imebadilishwa heading na posts zangu wamechakachua duu!!
hujaonekana siku 3 humu vipi kulikoni? Hongera lakini kwa ushindi wa kuchakachua.
 

Forum statistics

Threads 1,236,300
Members 475,050
Posts 29,253,351