LHRC kuchunguza theluthi mbili ya Z’bar

LHRC kuchunguza theluthi mbili ya Z’bar

Huyo mama anataka kuchanganyikiwa, siyo bure achunguze nini? Mwambieni arudishe fedha za wazungu zitamtokea puani ameshiriki kuwadanganya wajerumani kuwa wao na ukawa eti ndo wenye uwezo wa kusababisha kupata katiba! Na ITV daima wamepeana vipindi mpaka wamechoka hakuna mabadiliko, ndo mjue watanzania runawajua upapeta wenu kwa wazungu

Mkuu umenena vema. Nilimstukia mapema sana kuwa ni pandikizi la wazungu kuleta unreast nchini kupitia chagadema katika mgongo wa UKAWA, lakini vyama vingine vimewabaini mapema!
 
wewe umechanganyikiwa nini, nani kasema kasema kura za siri lazima ziwe na ndiyo na hapana? hoja mfu sana hiyo.

Kwani kura za siri zina matokeo gani zaidi ya"ndio"au "hapa?"
 
Mkuu umenena vema. Nilimstukia mapema sana kuwa ni pandikizi la wazungu kuleta unreast nchini kupitia chagadema katika mgongo wa UKAWA, lakini vyama vingine vimewabaini mapema!

mkuu! Huyu mama ni janga la taifa amewaonyesha watanzania alivyo kiherehere wa wazungu, lkn kwenye swala la katiba tutamuondolea uvivu hatuwezi kumwaacha atuangamizie taifa letu
 
Jaribu kuhakikisha ule mchakato wa kuwapa ela (isomeke hela) hawa Wajumbe 3 Manake hali kwa sasa ni mbaya zile za siri (kura) wengi wamepiga hapana. Naomba tukutane ofisini kwangu nawajulisha Lukuvi, Wassira na Migiro.

SS (Sawel Sitta)

LOL!!!! Kweli Akidi imetimia!!!!


 
kijo bisimbaaaaa mbona migogoro ya wakulima na wafugaji hatumsikii huyu mama inabidi ashitakiwe kwa kuidharau serikali ipo sheria
 
mwanasheria mbumbumbuanapojitoa ufahamu utashangaa tumekwambia jenga nyumba manake Jakaya atakapo swagwa the Hague uwe na pakuishi, usijifanye komba munywa tui la Nazi kura idadi ya wajumbe wa katiba wameongezeka toka wapi wakati sita alitanganza namba nyingine,

Mkuu Lwesye huwa kuna wanasheria na kuna Bush Lawyers, jee huyu yuko kundi gani?
 
Last edited by a moderator:
kadri mchakato wa katiba unavyosonga mbele ndivyo sura halisi za wale waliokuwa wamejificha kwenye koti linaloitwa neutral zinaanza kujitokeza.

Wahenga walisema, mfa maji hakosi kutapatapa.

Ndugu zake wanaojiita ukawa walishauriwa warudi bungeni, lakini yeye na timu yake wakawajaza upepo na kuwaambia wasirudi kwa sababu 2/3 haiwezi kupatikana.

Bunge maalum lina haki na kinga kama zilivyoainishwa katika sehemu ya pili ya kanuni, ibara ya 4(1-7)

sawa lina haki tumekubali haya mwambie sitta ataje majina ya wanaukawa waliopiga kura mbona kimya na idadi mtuambie imeongezeka vp hapo tutamaliza utata na kwanini aseme liwalo na liwe kama unaakili vizuri kichwani mwako acha ushabiki kwenye mambo muhimu tutaona kama hii katiba znz itapita utarudi hapa we kichwa maji nafikiri uliupata ujumbe wa mwanasheria mkuu znz
"mungu ibariki tanganyika"
 
LHRC nawapongeza kwa kazi zenu! Ila kwa hili la uchunguzi halina tija inabidi mwelekeze nguvu kwenye kuwajengea wananchi uelewa wa katiba pendekezwa ili waweze kufanya uamuzi sahihi wakati wa upigaji wa kura! Mama Bisimba na Sungusia pamoja na Masanja and Co. Its time you guys mpishe watu wengine hapo ofcn hasa damu changa! Sio kwa ubaya ila mmekaa muda mrefu sana just take a break for a while mnaweza kwenda pumzika legal aid au mkaimarisha kitengo cha utafiti. Then baadaye mkarudi. Ushauri tu! Hilo la theluthi 2 zimepatikanaje haina tija cc tunajua si halali ila hata mkigundua then what?
 

Helen-Kijo-Bisimba.jpg


MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba, amesema watafanya uchunguzi kubaini mazingira yaliyowezesha kupatikana kwa theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Zanzibar.

Alisema ingawa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa imepitishwa, theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar haijulikani inatokana na kura gani, kwani toka awali hesabu zilionyesha kura za wajumbe kutoka visiwani zisingefikisha idadi inayotakiwa.

“Pamoja na kupitishwa hiyo rasimu, bado kuna utata wamepataje theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar, tutafuatilia tujue imetokea wapi, kwa hesabu tulizokuwa tunapiga kulikuwa hakuna uwezekano,” alisema Dk. Bisimba.

Aidha alisema hata hivyo bado wananchi wana nafasi ya kuchuja katika kura ya maoni kuangalia ni mambo yapi waliyatolea maoni waliyotoa yapo katika Rasimu ya Katiba hiyo inayopendekezwa na yapi yametolewa, na ndipo wafanye uamuzi.

“Wananchi waelewe kuwa kupitishwa kwa rasimu ya tatu si mwisho wa mchakato, bali tunawasubiri katika kura ya maoni,” alisema.

CHANZO: Mtanzania

Huyu mama namkubali anaweza kufuatilia.
 
Back
Top Bottom