LG Wazindua Simu Mpya Inayotumia Skirini (Screen) Mbili

CostantineC

Member
Dec 28, 2012
30
11
LG imezindua simu mpya ambayo skrini yake ni kubwa na ambayo inaweza kutumiwa njia tofauti kwa wakati mmoja.

Simu hiyo LG G6 ina mfumo wa 18:9 badala ya mfumo wa 16:9 ambao unatumiwa na simu nyingi.

Hii ina maana kuwa skrini hiyo inaonekana kubwa kuliko kawaida.

LG imekiri kuwa simu iliyozinduwa awali ya G5 ilishindwa kufikia malengo yake ya mauzo.

LG inasema kwa simu hiyo haiwezi kuathiriwa na maji wala vumbi
Simu hiyo ilizinduliwa mjini Barcelona kabla ya kuanza kwa mkutano wa simu za mkononi duniani.

Skrini ya LG G6 ina upana wa sentimita 14.5 ikilinganishwa na skrini ya sentimita 13.5 ya LG5.

Simu hiyo mya pia inawewa kuzamishwa ndani ya maji hadi muda wa nusu saa bila ya kukumbwa na tatizo lolote.
Skrini hiyo imetengenezwa kuonyesa sehemu mbili wakati mmoja
G6 ni ndogo kuliko G5 lakini skrini yake ni kubwa

Source: BBC swahili
 
inawezekana simu yenyewe ndio hii hapa
1a62c9f7de28f20eef05dda783e49807.jpg
8cf0927b5850d4040b55502c6f05f618.jpg
 
Back
Top Bottom