LG Nexus 5X!

Hio nexus ni ya zamani mkuu siku hizi simu za google zinaitwa pixel, ameachana na nexus.

Kwa budget yako unapata midrange nzuri tu kama
-samsung galaxy j7 pro
-xiaomi redmi note 5 pro
-Huawei honor 7x

Au ukienda used way flagship za 2016 simu kama
-galaxy s7
-lg v10
-xiaomi mi 5 etc zinapatikana kwa hio bei
 
Asante sana mkuu ushauri huu nimeuchukua,hii Huawei Honor nimeipenda sana ila naona bei yake itakuwa mtihani kwangu,unaweza kuijua bei yake japo kwa kukisia?

J7 Pro wanakomaa 650,000/= kaka Kama hii Huawei itafika hata 600K nitafunga macho tu.
 
Asante sana mkuu ushauri huu nimeuchukua,hii Huawei Honor nimeipenda sana ila naona bei yake itakuwa mtihani kwangu,unaweza kuijua bei yake japo kwa kukisia?

J7 Pro wanakomaa 650,000/= kaka Kama hii Huawei itafika hata 600K nitafunga macho tu.
Huko duniani hio Huawei inauzwa kama 300,000 ile configuration ndogo ya 4gb ram na 32gb internal na inazidi kidogo ikiwa ni 64gb internal. Ila sijajua bei ya Hapa kwetu

Mondiale Firmware Huawei Honor 7X Smartphone 5.93 "Vue Plein Écran 2160*1080 p Octa Core 2.4 ghz Double arrière Caméra 16MP D'empreintes Digitales de la boutique en ligne | Aliexpress mobile
 
Huku nilipo oppo ni kama zote hela yako tu, nafikilia niwe dealer wa oppo tu. Niwe nawatumia mjini huko.[/QUOTE

Upo sehemu gani mkuu bado sijapata uamuzi ninunue simu gani,nisaidie pia bei zake na uimara wa hizo simu kama hutojali.
 
Kwa iyo budget yako ni nzuri..
Nngeshauri uchukue S7
Au uagize kama hauna uhitaji wa haraka sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utunzaji wake wa charge uko vipi mkuu,nime-google inaonyesha battery yake ni 2700 mAh ulivyokuwa unaitumia upande huo ilikuwaje?pia kwa pesa hiyo nitaweza kuipata kweli?
Chaji hazikai sana ni kama Samsung vile sema hivi ukiingia kwenye internet huwa zinapata moto sana
 
simu ziko freshi sana, ni kama brands kubwa kubwa tu kama huawei, lg, samsung vile. Hata design zake sio cheap kama ma tecno, zinaendeana sana na iphone kwenye software!
Sir_Mimi
 
Nawashukuru sana wakuu Extrovert merengo90 na mkuu utakuja na wote mliojaribu kunipa ushauri wenu,hili zoezi nimeamua kuliahirisha kidogo natuliza akili nichambue ktk models walizonishauri wadau hapa jukwaani ili nijue ipi ni sahihi kwa matumizi yangu na nitakayoweza kudumu nayo.

Nina jiwe langu Nokia Lumia 625 nililifungia kabatini litanisukuma sukuma kidogo wakati nikitafuta chaguo sahihi.

Asanteni sana!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…