Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Good evening members.
Mimi niliwahi kusaidiwa na mtu niliyekuwa simjui au mtu baki mwaka 2003.
Huyu dada alikuwa ni askari police. Hata mimi nilishangaa sana kusaidiwa na police.
Nilikuwa ninatoka Kigoma sasa narudi dar. Baada ya kushuka kutoka katika bus pale Ubungo nikaenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala kusubiri gari za kunipeleka Kariakoo ili nipande tena gari za kuelekea Tandika.
Kwa bahati mbaya kabla hata sijapanda gari nikakuta pochi yangu pamoja na simu vyote havipo. Nikaenda straight mpaka kituo kidogo cha police mule ubungo bus terminal kutoa taarifa.
Nikaandikisha kila kitu mpaka vitambulisho vyote vilivyopotea kasoro pesa ambazo walisema kuwa hawawezi kuandika kwa maana huwa hazipatikanagi.
Nikamwambia yule dada wa mapokezi kuwa kwa kuwa nimeibiwa pochi yangu yote pamoja na pesa sikuwa hata na nauli ya kunifikisha tandika, yule dada kwa huruma yake akaingia mfukoni mwake akatoa shillings 5,000 akanipa kama nauli.
Nilimshukuru sana kwa maana bila vile nilikuwa ninadhalilika sana that night. Thanks to God I met that good Samaritan. Hayo ndio yalinikita mimi na mengine mengi tu.
Jamani tusidharau watu baki huwezi kujua kesho nani atakuja kukubeba akupeleke kwa hospital.
Kama na wewe uliwahi kusaidiwa na mtu baki kama ilivyonikuta mimi naomba tu shee hapa wakuu.
Ninawasilisha.
Karibuni sana.