Zuriel_cfc
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 4,092
- 9,055
Nakumbuka wakati nipo kidato cha nne nilikuwa suspended shuleni nikatakiwa kurudi nyumbani na kuleta mzazi wangu. Tulikuwa wawili na mwenzangu. Basi tukasafiri hadi iringa mjini. Tulipanga kupeleka mzazi bandia shuleni. Tulipofika mjini mwenzangu akaniambia wacha tulale hapa mjini kesho tutajua cha kufanya.
Basi tukaenda kwny nyumba moja (mwenzangu alikuwa mwenyeji maana walikuwa wanaishi hapo iringa mjini mie natokea Dar) tukaingia geto. Kumbe ni kwa boyfriend wake mi sina habar nikajua ndio nyumbani.
Ilipofika mida ya saa mbili usiku wakaja wakaka wawili, nikatambulishwa huyu ni shemeji yako na huyu rafiki yake! Tukaenda mgahawani kula baadae tukarudi pale geto. Kumbe bwana watu wana mipango yao mie sina hili wala lile, story story badae mwenzangu akaniita nje, ananiambia mie nalala hapa wewe ukatafute pa kulala, lol!
Nilidata kabisa duh, usiku huu mi naenda wapi jamani, akaniambia kama vp kalale kwa yule (yule rafiki sasa) nikasema hapana ntaenda kulala stendi. Nikaingia ndani nikachukua kibegi changu nikaaga huyo nikatoka, ilikuwa kama saa nne hv usiku.
Nikaanza kutembea sijui naenda wapi, nikawaza pa kwenda, hela sina zaidi ya nauli ya kurudia shuleni, nikaanza kulia njiani huku natembea. Kumbe yule kaka (rafiki) hakupenda nilichofanyiwa akawa ananifuata nyuma mie sijui. Nikatembea kufika barabarani nikaa pembeni sielewi cha kufanya. Akatokea yule kaka akaniuliza kwani yule sio rafiki yako? Nikamwambia nimwanafunzi mwenzangu tunasoma darasa moja. Akashangaa, sasa mbona hauko shule? Nikamweleza ukweli kama nimefukuzwa shule natakiwa nipeleke mzazi kwa sababu tulifanya mgomo shuleni.
Akaniuliza shule gani nasoma na kwa nini nisiende nyumbani sasa. Nikamwambia siwez kwenda nyumbani mama yangu atanikata masikio akijua nimefukuzwa shule. Akaniuliza sasa utafanyaje, nikamwambia itabidi nitafute mzazi bandia ndo niende nae. Yule kaka akaniambia nyanyuka twende mi nitakusaidia. Nikanyanyuka tukaenda hadi nyumbani kwake (chumba kimoja). Akanionesha choo nikaoge nikakataa, nilikuwa naogopa na natetemeka kama nimeshikwa na homa. Akaniambia usiogope mi sitakufanya chochote, kuwa na amani panda kitandani ulale. Duh!
Nikamuuliza wewe unalala wapi akasema ntalala chini,wee moyo unadunda hatari. Akasema niamini kweli sitakufanya chochote we lala tu kesho nitakusaidia kutafuta mama akupeleke shule. Nikapanda kitandani na jinsi,viatu, na kibegi changu mgongoni. Akanipa shuka jifunike baridi. Nikalala kwani usingizi ulikuja?? Yule kaka akalala chini,katandika shuka akaweka manguo kichwani kama mto akalala. Nikakaa nawaza mpaka nikapitiwa na usingizi. Kushtuka asbh yule kaka hayupo. Nikaa kitandani siamini kama nimelala salama salimini.
Kidogo akarudi akaniuliza umelala salama? Umejikagua uko salama? Ulikuwa unaogopa nini sasa? Nikatoa tabasam feki pale, nikamwambia asante kwa kunihifadhi. Akaniambia nenda kaoge nikupeleke ujanywe chai. Nikasema nataka nitafute mama wa kwenda nae shule kwanza akasema usijali si nimekwambia ntakusaidia? Basi nikaenda chooni kuoga nilipomaliza tukatoka nje, akanipeleka kwny stend ya kalenga kuna mama ntilie kibao, tukaingia kibanda kimoja cha mama wa kichaga kumbe alishaongea nae akamweleza shida yangu yule mama akakubali. Tumekunywa chai akanitambulisha kwa yule mama, kwamba ndo atanisaidia kwenda shule kama mzazi wangu, duh! Nimampanga yule mama vya kwenda kuongea shuleni akakubali. Akafunga biashara yake kaenda kujiandaa hao tukaenda stendi kuu kupanda gari za shuleni. Yule kaka alinipa na nauli yangu na ya yule mama aisee.
Nilimshukuru sana sana na kumuomba msamaha nilimfikiria vibaya usiku. Akaniambia kuwa na amani bado wanaume wastaarabu tupo. Nikarudi shuleni. Sikumtafuta tena yule kaka na sijui kama yuko tena, ila kati ya watu muhimu walionishika mkono kwny maisha yangu na yeye alikuwepo japo hata sikufanikiwa kumjua jina lake.
It is well with my Soul!