Lete ushahidi.!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lete ushahidi.!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chakochetu, Oct 30, 2012.

 1. c

  chakochetu Senior Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna jambo ambalo linasumbua kama kushindwa kukubali ukweli na kurekebisha tatizo.!!

  Sasa imekuwa ni suala linalosumbua jamii yetu,tukisema hapa Serikali ifanyie kazi kero mbalimbali utasikia majibu yasiyo na ufumbuzi wa tatizo eti "KAMA UNA USHAHIDI ULETE" tuufanyie kazi.

  Ebu niambie neno hili kama siyo la kujihami na kukwepa kuwajibika :

  [1].Mpenzi wako unasikia anafanya mapenzi na mtu mwingine na una uhakika,eti anakuambia neno hili NIPE USHAHIDI.[2].Tuna hakika viongozi wanahujumu uchumi unaambiwa eti ,kama una USHAHIDI ULETE tufanyie kazi.
  [3].
  [4].Kuna maofisa wa serikali wanashirikiana na wawekezaji katika kutengeneza mikataba mibovu,isiyokuwa na tija kwa Taifa,na mikataba mingi ni mibovu inastahili kufanyiwa marekebisho,eti hata hili unaambiwa LETE USHAHIDI
  [5].Kuna tatizo la vyama tawala barani Afrika KUIBA KURA KATIKA CHAGUZI KUU,eti hili nalo LETE USHAHIDI.
  [6].Maadili ya Taifa yanaporomoka na mustakabali wa Taifa unawekwa rehani,kwa viongozi kushindwa kusimamia kanuni,sheria na taratibu na kutozingatia misingi iliyowekwa na Viongozi waliotangulia,hamna kiongozi anayekubali bali wanajihami na kusema LETE USHAHIDI.
  [7].Serikali imeshindwa kuwadhibiti wafanyabiashara wameachwa wanapanga bei wanavyotaka wao,Serikali imeshindwa kudhibiti Mfumuko wa bei(inflation),eti hii nayo Watawala wanajitetea mpaka USHAHIDI,sasa mwananchi gani ataenda kuwapa ushahidi??
  [8].EWURA iondoe kipengele cha kupandisha bei kila baada ya wiki mbili,bei zipande mara moja kwa mwaka na hasa wakati wa Bajeti kama BIA,SIGARA na bidhaa nyinginezo ili kulinda mwenendo wa bei katika soko la tanzania.EWURA sijui wame copy and paste kutoka OPEC au soko la dunia???,EWURA na wafanya biashara wa bidhaa hii ndio wanayumbisha soko la petroli ,eti hili nalo watasema LETE USHAHIDI.!!!
  [5].Tulisema,na wengi dalili tuliziona miaka 5 inamtosha Mkuu wa Nchi kutawala, miaka 10 asingeweza na mambo yatamshinda,eti wakasema mbona wengine waliweza kwa nini yeye ashindwe,sasa TUNAONA ,eti hii nayo NILETE USHAHIDI.
  [6].Wazanzibari wengi hawataki kukubali ukweli,kwamba wengi wao walitokea BARA enzi ZILE za biashara ya mwarabu[kuwasafirisha binadamu kwenda Ulaya na Uarabuni] na soko lilikuwa Zanzibar,na hili linahitaji USHAHIDI MWINGINE?!!
  [7].Nchi nyingi za Afrika zinafanani,Ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji;ukiona matukio yanatokea yanafanana na matukio yanayotokea katika nchi za wenzetu,hili sijui tena Serikali itasema kama una ushahidi lete tuufanyie kazi.
  Orodha ni ndefu .....
   
 2. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Lete ushaidi,nimekubali wanafunzi hawajui kusoma...lete,walimu wamegoma kimyakimya..lete....wabunge wamepandishiwa mshahara na let....du huu nao ukweli mtupu
   
 3. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Serikali haijui kinachoendelea .... everyone is busy thieving/stealing.
  Ndio maana majibu yao kwa kila jambo ni "lete ushahidi"
   
 4. m

  mojaone Senior Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [Serikali haijui kinachoendelea .... everyone is busy thieving/stealing.
  Ndio maana majibu yao kwa kila jambo ni "lete ushahidi"

  Na wewe leta ushahidi
   
Loading...