Let Us Bring Balali Home

mwanatanu

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
851
127
Ndugu zangu wana JF, nawaombeni tusingoje serikali yetu imrudishe Balali. Na inawezekana wasifanye hivyo.

Naomba tuamzishe kampeni ya kumrudisha huyu mfisadi Bongo ili aweze kutoa nyaraka zote alizonazo.

Mawazo kwa Kampeni:
Kama mjuavyo, waandishi wetu wa magazeti Bongo ni wachanga, hivyo basi tuwatumie waandishi wa kigeni.

Kuna dada huyu wa Washington Post aliye stationed Nairobi anaitwa Stephanie McCrummen, huenda akaja Dar wakati Bush akija nchini.

Kuna jamaa huyu, Matti Huuhtanen wa Associated Press, na nahisi yupo Nairobi.

Nasema hivi kwa sababu kashfa ya BOT ni kubwa na haikupata uangalifu wowote kwenye mataifa tajiri.

Kama mjuavyo, kashfa hii ikipata kufichuliwa, bila shaka kutakuwa na shinikizo kwa serikali yetu iwajibike na hawa mafisadi.

Sipendelei ushawishi wa kigeni katika kutatua matatizo yetu, lakini inavyoonekana, serikali yetu inaonekana kubebana mno.

JF, tafadhali, tuachie tuifanye..."KURUDISHA BALALI NYUMBANI".
 
US Govt wameshatangaza kwamba wako tayari kusaidia katika kumrudisha Ballali. Siku zinakatika na msanii hajazungumza lolote kuhusiana kauli hiyo ya US. Halafu watu wanapoanza kufanya speculation anasema wananchi wasisikilize misleading information. Kunapokuwa na ukosefu wa habari toka kwa watendaji wakuu wa siri kali kuhusiana na habari muhimu za nchi kama hili sakata la BoT basi hali ndiyo huwa hivyo, na sioni dalili zozote za huyu jamaa kuhakikisha anaondoa hali hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom