Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,630
- 4,228
Wakuu,
Kulingana na hii statement ya Bw Rweyemamu nadhani
serikali haioni sababu za kumleta huyu bwana ajibu maswali
ya Wa-TZ.My opinion ni kwamba huyu bwana anamaswali ya
kujibu and that is why JK alimfuta kazi.
Kisha hii ishu ya EPA has a lot of pointers in it, such that its
only prudent serikali kujua alipo Balali na if anything asingeruhusiwa
kutoka ndani ya nchi isipokua while under Govt supervision.
Jamaa wanaleta densi na hii ishu just to buy time while thinking
watu watasahau.Huu ni uwizi wa hali ya juu and it is a lot of
diservice for Rweyemamu to callously say tukimtaka tutampata!!!
So tell me who is fooling who?Fat cats are getting away with murder
alafu tunaona magazetini eti trafiki kashikwa kwa sababu ya hongo...
hela yenyewe ukitizama ni mbuzi tu!!!
Aaah,....Jamani bongo!!!
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/9/habari21.php
na Irene Mark
SERIKALI imesema haimtafuti aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali, ambaye mapema mwaka huu alifutwa kazi na Rais Jakaya Kikwete kutokana na kubainika kwa wizi wa mamilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema kuwa serikali ina mkono mrefu na iwapo itafikia hatua ya kumtafuta gavana huyo wa zamani wa BoT, haitashindwa kamwe kumfikia alipo.
Alisema kutokuwepo nchini kwa Ballali, au kutojulikana alipo, si jambo linaloisumbua serikali kwa sasa, kwa sababu hivi sasa yeye ni raia wa kawaida, hivyo anao uhuru wa kuishi popote anapopenda.
"Serikali haimtafuti Ballali (kwa sasa), lakini ikiamua kufanya hivyo haitashindwa. Kwanza ni private citizen (raia huru) siyo mwajiriwa wa serikali tena," alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa, mkono wa serikali ni mrefu hautashindwa kumpata Ballali iwapo itamhitaji.
Akifafanua zaidi, alisema baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wake, serikali iliunda timu ya kuwachunguza watuhumiwa wa EPA, kuhakikisha fedha zilizoibwa zinarudi na kuwachukulia hatua waliohusika, akiwemo Ballali.
Alisema: "Ninachofahamu ni kwamba, timu iliyopewa kazi kuhusu ubadhirifu wa EPA inaendelea na kazi yake na tunaona jinsi fedha zinavyorudishwa." Mkurugenzi huyo pia alikiri kwamba serikali haifahamu hospitali aliyokuwa akitibiwa Ballali, licha ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kukaririwa akisema alimtafuta Ballali bila mafanikio alipokuwa jijini Washington, Marekani.
"Kwa kweli sifahamu hasa Ballali alikuwa akitibiwa katika hospitali gani, lakini najua alikuwa nchini Marekani katika Jimbo la Boston, ila hospitali kwa kweli siijui.
"Lakini huyu ni mtu huru, hivyo anaweza kuishi popote… huyu ana nyumba yake nchini Marekani… yupo huko anaishi na familia yake," alisisitiza Rweyemamu katika ufafanuzi wake.
Alisema mafanikio ya timu inayochunguza suala la EPA yanaonekana, hivyo aliwaomba Watanzania kusubiri ripoti itakayotolewa baada ya kukamilika kwa kazi hiyo.
Hivi karibuni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye pia ni kiongozi wa timu hiyo, alibainisha kuwa kazi ya timu hiyo inafanyika kwa siri na kwamba zaidi ya sh bilioni 67 zilikuwa zimerejeshwa na kampuni zilizodaiwa kujichotea fedha hizo kutoka EPA.
Kwa upande wake, mjumbe wa timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, aliwahi kukaririwa akisema aina ya uchunguzi unaofanywa dhidi wa kampuni na wamiliki hao haitakiwi kuwataja watuhumiwa wanaorudisha fedha hizo hadi watakapohitimisha kazi yao.
Timu hiyo ina wajumbe watatu ikihusisha pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).
Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, baada ya taarifa ya uchunguzi wa hesabu uliofanywa na Kampuni ya Ukaguzi ya Ernst & Young na kubaini ubadhirifu wa zaidi ya sh bilioni 133.
Taarifa hiyo ilibaini kuwapo kwa kampuni hewa 22 zilizolipwa mamilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti hiyo kati ya mwaka 2005 na 2006.
Hata hivyo, ilibainika kwamba, baadhi ya kampuni hizo zilidanganya kuhusu usajili na wamiliki wake huku nyingine zikimilikiwa na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wengine wakitumia nyaraka za kughushi kuiba mabilioni hayo.
Mbali na udanganyifu huo, fedha za EPA zinadaiwa kusaidia kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Kutokana na kashfa hiyo na nyingine zilizoikumba serikali ya awamu ya nne, nchi wahisani na washirika wa maendeleo walitishia kusitisha misaada yao katika bajeti ya serikali.
Tishio hilo la wahisani ambao mchango wao kwenye bajeti ya serikali ni asilimia 43, liliifanya serikali kuwaangukia kwa kuchukua hatua za haraka katika mapambano dhidi ya ufisadi.
Jitihada hizo za serikali zinaonekana kuzaa matunda kwani siku mbili zilizopita, wahisani hao wametangaza kuendelea kuchangia bajeti ya serikali baada ya kuridhishwa jinsi Rais Kikwete alivyoshughulikia suala la ufisadi nchini.
Hata hivyo, uamuzi huo wa wahisani uliingia doa juzi baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Wangwe kuutuhumu hadharani Umoja wa Ulaya (EU) akisema uamuzi wao wa kurejesha misaada unaonyesha kwamba umekuwa na ajenda ya siri ya kulinda ufisadi kwa ushirikiano na serikali.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/9/habari1.php

Trafiki kizimbani kwa rushwa
na Asha Bani
ASKARI wa Kikosi cha Usalama Barabarani, X WP 2846 CPL Sauda Habibu Kaijage, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akituhumiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh 3,000 kutoka kwa dereva wa daladala

Ikulu: Tukimtaka Ballali tutampata