Let it Go!

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Ex atabaki kuwa ex tu na sio maana nyingine yoyote. Kama ni wa maana, asingekuacha au asingekukosea adabu pindi mlipokuwa wote.

Kama Ex hakuwa na mchango wowote wa maana kwako wakati mkiwa pamoja, unafikiri kwa muda huu atakuwa na mchango gani wakati hamko pamoja?

Ndio, inawezekana ni mtu ambaye ulimpenda sana na huenda ndio alikuwa ni mpenzi wako wa kwanza, lakini inatakiwa ukubali tu kwamba, mlishamalizana na kila mtu akashika njia yake.

Njia yetu ya kupata furaha na amani, ni kutambua kwamba furaha yako haitakiwi umkabidhi mwingine kwa niaba yako.

Sio kwa sababu ameona siku hizi umenawili, unapendeza anaanza vitext vya 'Hi' na wewe ukaingia mkenge!

Kuwa na msimamo, na jali zaidi maisha yako, maumivu uliyopata awali yalikuwa yanatosha..

usikaribishe mengine!

Akija pasha kiporo kama ni kitamu kisha tembea mbele kama Mjeshi!! "Usawa wa kati, kwa mwendo wa haraka, mbeleeeeeeeee tembea!!!!"

Ataanza Kukumiss pale atakapokosa mbadala wako.

Ataanza kukumiss pale atakapoona uso wako umejaa tabasamu na muonekano wako ni bomba kuliko awali.

Ulifanikiwa kuchomoka, ukapona! Kuwa makini, usiangukie kwenye mikono yake tena!!
IMG-20191201-WA0017.jpeg
tapatalk_1571456657145.jpeg
 
moment za mahusiano ndo ngum zaid kusahaulika ktk maisha ya mwanadam na hisia za mapenz ndo zenye nguv zaid kwa mwanadam hivo wengi hujikuta tu kwa x bila kutarajia...
wanaoweza kumove on mazima wale walokua wanakidhi haja tu na si walopendana
 
Sio kila wanaoachana na wapenzi wao hao wapenzi wanakuwa hawana maana muda mwingine wanadamu tamaa tu na kukosa uvumilivi vinatuponza. Hivi hujawahi kusikia mtu anatamka 'tangu niachane na yule mwanaume/mwanamke sijabahatika tena kukutana nae kama yule?'
 
You cant fix a broken mirror
Sio kila wanaoachana na wapenzi wao hao wapenzi wanakuwa hawana maana muda mwingine wanadamu tamaa tu na kukosa uvumilivi vinatuponza. Hivi hujawahi kusikia mtu anatamka 'tangu niachane na yule mwanaume/mwanamke sijabahatika tena kukutana nae kama yule?'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom