LESENI ZA UDEREVA TRA NI WAZEMBE.

LESENI ZA UDEREVA TRA NI WAZEMBE.

Mimi tangia march 2018 hadi kesho nilipoenda mara kadhaa bila Mafanikio pale makubusho nami nikaachana nao life goes on
Lipo tatizo sugu la upewaji wa leseni za udereva kwa kisingizio cha uhaba wa kadi! Mimi binafsi muda wa leseni yangu kuisha ni mwezi wa sita, mwezi wa tatu nilikwenda TRA kulipia muendelezo wa leseni yangu nikaambiwa nitaipata baada ya wiki mbili, hata hivyo niliongeza zangu hivyo mwezi huu wa nne nikaenda TRA nikijua nitapata leseni yangu, hola! Niliambiwa nirudi baada ya wiki mbili kama watanijulisha kupitia ujumbe wa simu yangu! Nina mashaka kama TRA wanajua umuhimu wa leseni za udereva, inaelekea kwako kutupa leseni hizo ni hisani si lazima. Idadi ya madereva ni ndogo sana sana ni uzembe uliotukuka wanaposhindwa kuwa na kadi za kutosha.
 
Kumbuka kadi iliyokwisha muda kuwa muda mrefu inakufa na ukitaka kuifufua itabidi urudi mafunzoni tena.
Duuh mimi imeisha tangu mwezi wa pili na naona uvivu kweli kwenda kurenew sababu kila anaye enda lazima akae miez mpaka 6 ndio apate. Nikienda saiv si ndio mwanzo wa kupewa manual ya mwaka 47 kuendesha
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama una magari matatu inakulazimu kutoa copy 3. Dah!
Si unaweza kuwa una hama nacho au mnatumia watatu leseni moja?
risiti hiyo!!!!!?
Hivyo ndio nilivyofanya baada ya kuona walio renew kabla yangu usumbufu wanaopata.Nililipia mwezi wa 7 mwaka Jana nikapata leseni mwz wa 12 mwishoni KBS tena baada ya wao kunipigia simu kuwa iko tayari.
Yeah, hii njia ndio niliifanya baada ya trip 3 bila kuona matumaini ya kupewa. Wenyewe wakanicheki baadae.
Sikumbuki
Usitake tuvunje sheria, tueleze kifungu cha sheria kinachoruhusu karatasi ya malipo kuwa mbadala wa leseni ili nasi tukitumie.

Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi TRA msikilize alichosema hapo 👆
 
Back
Top Bottom