Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 23,277
- 28,437
Lipo tatizo sugu la upewaji wa leseni za udereva kwa kisingizio cha uhaba wa kadi! Mimi binafsi muda wa leseni yangu kuisha ni mwezi wa sita, mwezi wa tatu nilikwenda TRA kulipia muendelezo wa leseni yangu nikaambiwa nitaipata baada ya wiki mbili, hata hivyo niliongeza zangu hivyo mwezi huu wa nne nikaenda TRA nikijua nitapata leseni yangu, hola! Niliambiwa nirudi baada ya wiki mbili kama watanijulisha kupitia ujumbe wa simu yangu! Nina mashaka kama TRA wanajua umuhimu wa leseni za udereva, inaelekea kwako kutupa leseni hizo ni hisani si lazima. Idadi ya madereva ni ndogo sana sana ni uzembe uliotukuka wanaposhindwa kuwa na kadi za kutosha.