Leseni ya Biashara Kundi A, na Jinsi ya Kuipata

Leseni ya Biashara Kundi A, na Jinsi ya Kuipata

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,638
Reaction score
3,641

Njia rahisi za Kuomba Leseni ya Biashara Tanzania​

Je, unataka kuendesha biashara halali Tanzania? Kupata leseni ya biashara ni hatua ya lazima na sasa mchakato ni rahisi kuliko unavyofikiri. Fuata hatua hizi:
kundi A.png

  1. Tembelea tovuti rasmi: www.business.go.tz
  2. Bonyeza sehemu iliyoandikwa “Huduma”
  3. Chagua “Huduma za Leseni”
  4. Bonyeza hatua ya kwanza “Jisajili”
  5. Rudi tena kwenye “Huduma”
  6. Chagua tena “Huduma za Leseni”
  7. Hatua ya pili: Jaza taarifa za ombi lako la leseni
  8. Upload viambatisho muhimu (mfano TIN, mkataba wa pango, n.k.)
  9. Bonyeza “Tuma Ombi”
  10. Thibitisha na fanya malipo

Kumbuka​

Huu ni mfumo wa kidijitali, rahisi, wa haraka, unaopatikana popote.

Utoaji wa Leseni ya Biashara Kundi A Nani Anafaa, na Jinsi ya Kuipata​

Leseni ya Biashara si karatasi tu ni kibali halali kinachokupa mamlaka ya kuendesha biashara kisheria, kuaminika mbele ya taasisi za kifedha, na kupokea tenda kubwa!

Kundi A: Kwa Biashara Kubwa Zenye Uwekezaji Mkubwa​

  • Huduma za mawasiliano
  • Usafiri wa kimataifa
  • Benki, bima, utalii, bandari
  • Maduka ya kubadilishana fedha n.k.
Hutolewa na BRELA (Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni)

Kundi B: Kwa Biashara Ndogo na za Kati​

  • Migahawa, hoteli, biashara za ushauri, wakala wa bima, maduka ya rejareja n.k.
  • Hutolewa na halmashauri kupitia Afisa Biashara

Faida za Kuwa na Leseni Halali​

  1. Kufanya biashara kwa kutambulika kisheria
  2. Uaminifu kwa wateja na taasisi (mfano benki na mashirika ya fedha)
  3. Kupata fursa ya kushiriki tenda na zabuni
  4. Kutumia kama nyaraka ya kuomba mkopo
  5. Kukua kwa biashara yako bila usumbufu wa kufungiwa

Mimi na Timu Yangu Tupo Tayari Kukusaidia Kila Hatua​

Kuanzia usajili, maandalizi ya nyaraka, hadi kufuatilia leseni yako – tutakusaidia kwa haraka, kwa usahihi, na kwa weledi.
 
Back
Top Bottom