Leseni mpya za udereva kutolewa mwezi huu

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
a31ba6c174b28eb37e1e84dfa3def605.jpg

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu ucheleweshwaji wa kutoa leseni za udereva na kusema jambo hilo limesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa utoaji leseni ambao hivi sasa unaboreshwa ili leseni ziwe imara na kwamba kazi hiyo itakamilika kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Akizungumza na HabariLeo jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema ni kweli kumekuwa na ucheleweshaji wa kupewa leseni kwa madereva walioomba leseni kutokana mfumo wa sasa kubadilishwa. Aliongeza kuwa wataalamu hao wakandarasi wameshafika na wanaendelea kukamilisha kazi hiyo na kwamba ndani ya siku chache kuanzia sasa watakuwa wamemaliza na kuanza kutoa leseni kabla ya mwisho wa mwezi huu.

“Nia ya serikali na TRA ni kuboresha leseni zetu ili ziwe imara na tumekubaliana na Jeshi la Polisi kwa sasa madereva waendelee kutumia leseni za zamani ili mradi tu anaposimamishwa aoneshe risiti ya malipo aliyolipia leseni mpya,” alisema Kayombo. Alisema lengo la kuanzisha mfumo mpya wa kompyuta wa leseni ya kuendesha ni kuisaidia serikali kukusanya taarifa sahihi kuhusu dereva ambazo zitasaidia katika kufuatilia mienendo yao na kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato yake ya kutosha.

Alisema matarajio ya serikali ni kwamba mfumo huo mpya wa kutoa leseni utapunguza ajali za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na madereva ambao hawana sifa za kutosha za kuendesha magari. Kayombo aliwataka madereva ambao wamelipia leseni na hawajazipata kuwa watulivu kwani maboresho hayo yanayofanywa ni katika kuzifanya leseni hizo mpya kuwa imara na kwamba ndani ya wiki mbili kuanzia sasa zitaanza kutolewa. Alisema mfumo mpya wa leseni unachukua nafasi ya mfumo wa zamani ambao hakuweza kutofautisha kati ya aina ya leseni kwa ajili ya kuendesha gari na magari ya abiria ya uwezo tofauti.
 
Mwezi huu unakaribia kuisha, labda wangesema mwanzoni mwa mwezi ujao.
Wamepata tabu sana wale ambao leseni zao zimeisha na wanataka kuomba kazi, mwajiri anakwambia upeleke leseni iliyo hai.
 
Watu tume renew leseni toka mwezi wa tatu hadi leo kimya halafu mtu analeta siasa eti maboresho na upuuzi gani sijui, si aseme material yameisha mbona watumishi wa TRA ukiwauliza wanasema material yanasumbua tumuamini nani sasa??? Watu wanakosa ajira kisa tu hawana valid license nyie mnachukulia poa tuu.
 
Mbona Kiongozi Wa Tra Kasema Wameboresha Mifumo Yao Ila Siyo Leseni Mpya.
Wanaosema Mpya Ina Maana Zilizotolewa Ni Za Zamani
 
Sawia, Mimi nimehuisha leseni yangu tangu mwezi wa tano na nimeishakabidhiwa mpya, sijaona kama kwenye kadi kuna mabadiliko yoyote.
 
View attachment 838599
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu ucheleweshwaji wa kutoa leseni za udereva na kusema jambo hilo limesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa utoaji leseni ambao hivi sasa unaboreshwa ili leseni ziwe imara na kwamba kazi hiyo itakamilika kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Akizungumza na HabariLeo jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema ni kweli kumekuwa na ucheleweshaji wa kupewa leseni kwa madereva walioomba leseni kutokana mfumo wa sasa kubadilishwa. Aliongeza kuwa wataalamu hao wakandarasi wameshafika na wanaendelea kukamilisha kazi hiyo na kwamba ndani ya siku chache kuanzia sasa watakuwa wamemaliza na kuanza kutoa leseni kabla ya mwisho wa mwezi huu.

“Nia ya serikali na TRA ni kuboresha leseni zetu ili ziwe imara na tumekubaliana na Jeshi la Polisi kwa sasa madereva waendelee kutumia leseni za zamani ili mradi tu anaposimamishwa aoneshe risiti ya malipo aliyolipia leseni mpya,” alisema Kayombo. Alisema lengo la kuanzisha mfumo mpya wa kompyuta wa leseni ya kuendesha ni kuisaidia serikali kukusanya taarifa sahihi kuhusu dereva ambazo zitasaidia katika kufuatilia mienendo yao na kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato yake ya kutosha.

Alisema matarajio ya serikali ni kwamba mfumo huo mpya wa kutoa leseni utapunguza ajali za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na madereva ambao hawana sifa za kutosha za kuendesha magari. Kayombo aliwataka madereva ambao wamelipia leseni na hawajazipata kuwa watulivu kwani maboresho hayo yanayofanywa ni katika kuzifanya leseni hizo mpya kuwa imara na kwamba ndani ya wiki mbili kuanzia sasa zitaanza kutolewa. Alisema mfumo mpya wa leseni unachukua nafasi ya mfumo wa zamani ambao hakuweza kutofautisha kati ya aina ya leseni kwa ajili ya kuendesha gari na magari ya abiria ya uwezo tofauti.
Tumekalia politiki, kila mahali politiki raha wanaodanganywa ni wa GPA 32, huo uimara in wa zege au ribiti! Bora hats angesema mpya zitakuwa na chipu kama kadi za benki ili ziweze kuhifadhi kumbukumbu ya dereva angalau ningeelewa kuliko hili la kudumu muda mrefu wakati hizi tulizonazo zinadumu. Kila mtanzania ni politiki, politiki, politiki!
 
Yani politiki kila sehemu mkuu.
 
Sasa hawa jamaa hadi sasa mbona bado hawazitoi hizo leseni maana walituhadi kabla ya mwezi wa nane watakua wameshaanza kutoa lakini yangu wanayo toka mwezi wa sita
 
Vp zinatoka kwli? maana naingia wiki ya tatu sasa tokea niambiwe "utatumiwa message ikiwa tayari"
 
Mwezi wa pili sasa nasubiri msg kutoka TRA naona haifiki. Izi kadi kupata ni changamoto sana. Mh Raisi pengine wanahitaji na hili uliseme wewe.
 
Tanzania bwana wanahangaika mno na mambo ambayo mengi hayana hata msing. wala hayasaidii kutatua tatizo lililopo. Yaani kubadilisha mfumo wa kutoa leseni kutazuiaje ajali? Kwamba hao wanaopata ajali barabarani ni wale tu ambao hawana sifa za udereva au waliopata leseni kwa njia za mkato?

Hiyo mizinga ya kila wakati ya gari za serikali ilikuwa inapigwa na madereva wasio na sifa ambao hawakustahili kupata leseni?

Siku zote nawaambia watu, kwamba unapaswa kutofautisha kujua jinsi ya kuendesha gari na kufanya maamuzi ya haraka na hekima ukishajua kuendesha gari na kuwa barabarani. Hivi ni vitu viwili tofauti. Madereva wa mabasi hawaui watu kwa kuwa hawajui sheria au kuendesha mabasi. Mara nyingine ni uwezo wa mtu kufanya uamuzi wa busara akiwa barabarani Hilo huwezi ukamfundisha mtu.

Hilo hata kwa wasomi lipo. Raisi mzuri sio lazima awe yule aliesoma hadi PhD.
 
Shit. Hii ni December leseni bado zinasumbua kutolewa. Tumrudishe Kitilya mchapa kazi.
Arudishwe Kitilya muone mambo
 
Mwezi wa pili sasa nasubiri msg kutoka TRA naona haifiki. Izi kadi kupata ni changamoto sana. Mh Raisi pengine wanahitaji na hili uliseme wewe.
Mwezi wa pili tu?

Watu tangu mwezi wa 6 wanasubiri mkuu.
 
Back
Top Bottom