Leo tupike mkate wa nazi

Leo tupike mkate wa nazi

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,467
Reaction score
65,789
Hell

Hii leo sikuchukua picha hatua zote kwasababu ya umeme kukatika siku nzima ila haikuwa sababu ya mimi kuzuiwa kuja kuwafundisha na hiki pia

Hivi vitu una weza fanya nyumbani kwako ukiwa umetulia familia injoy kile ulicho kianda

Hatua ya kwanza utatafuta nazi yako mimi nilichukua nazi asili nilinunua sokoni kisha nikaaichuja vizuri na kuiweka pembeni

Baada ya hapo nika chukua ngano nikaichekecha kisha nika weka sukari, chumvi, amira, pamoja na blue band, nika changanya vizuri kisha nika chukua tui la nazi ile nilio chuja nikaweka pole pole yaani kidogo kidogo kumbuka nazi nimetumia tui lile la kwanza tu

Baada ya hapi nikaanza kukanda mpaka ngano ilipo kuwa tayari yaani ilikuwa ime lainika vizuri nika ifunika na kuiweka pembeni kwa mda furani ili ipoe kidogo kisha nikaichukua na kuanza kutengeneza maumbo ambayo mimi naya taka yawe

Baada ya hapo nikaacha ya umuke kwa mda fulani kisha nika chukua yai nikaanza kupaka juu ya mikate yangu hakikisha yai lina kolea vizuri sana na pia kama una ufuta unaweza weka kwa juu kuongeza mvuto wa mikate yako mimi nilikosa baada ya hapo nikaweka kwenye oveni kwa mda wa nusu saa moto ukiwa mdogo

Nikaja kutoa nikaona mikate yangu imekuwa vizuri nikapaka mafuta juu nika weka kwa mara ya mwisho na mikate yangu ipo vizuri kama unavyoona
1752676773436.jpeg

Tupo hapa kwa lengo la kujifunza so chukua darasa wengine wanajifunza kwa pesa mimi nimejitolea kwenu
1752676892608.jpeg

Tuzidi kujifunza mimi na wakubali sana wanangu
Kila mtu na maisha yake kila mtu ana pambana anavyojua mwenyewe ugai gai ………..
1752677136796.jpeg
 

Attachments

  • 1752676826035.jpeg
    1752676826035.jpeg
    311.6 KB · Views: 15

Similar Discussions

Back
Top Bottom