Leo tunakumbuka miaka 91 tangu Kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Mwalimu Nyerere alizaliwa tarehe 13 Aprili 1922. Leo ni miaka 91 tangu siku hiyo.

Nimeweka hapa documentary ya The Legacy of Mwalimu Nyerere, kama kumbukumbu ya siku hii.
 
Last edited by a moderator:
Nimeangalia video hii.

Nimefurahishwa na jinsi Mwalimu alivyokuwa akiongelea mambo ya matatizo ya Africa, na mfumo wa kiuchumi wa dunia na World Bank na IMF.

Hotuba yake kwenye bunge la Afrika ya Kusini iliwasisimua wabunge wa Africa ya Kusini.

Great son of Africa.
 
Video haifunguki, lakini naamini huyu mzee alikuwa anafanya kweli, japo yapo makosa aliyoyafanya kama binadamu, lakini kwa kiasi kikubwa alijitahidi sana kuijenga tz ya kujitegemea, alisema...NCHI HAIWEZI KUWA HURU KAMA BADO NI TEGEMEZI KIUCHUMI...na kweli leo ndio tunachokiona, tuna UHURU wa bendera tu, lakini kila kitu kinakuwa controlled kutoka mataifa makubwa, na rais wetu bila aibu, kutwa kucha kutembea kama YATIMA KUOMBA OMBA NCHI ZA NJE...ilihali tuna rasilimali chungu nzima....KIKWETE ANATUABISHA SANA KAMA TAIFA.
 
Subiri wenye kumpinga watakavyokuja na kejeli zao.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Alifanikiwa kutuimbisha wimbo wa Amani na Utulivu uliotufanya tuwe waoga wa kufanya maumuzi magumu na kuwa masiki mpaka leo,wajanja wanautumia wimbo huu kutpiga changa la macho.

Suluhisho la matatizo ya nchi hii ni kuuzika huu wimbo aliouasisi kama tulivyozika yeye mwenyewe baada ya hapo hawa wapiga porojo za kisiasa wataheshimu rasilimali zetu na watatuheshimu sisi wenyewe.

Nachukia sana hii nidhamu ya woga iliyojengwa na huye mzee, kuna watu walikuwa wanamuogopa huyu mzee zaidi ya wanavyomuogopa mungu
 
Alikuwa shujaa wa taifa lake na afrika kwa ujumla. watu waliokuwa na tabia za kupenda kuonea wenzao walikiona na wanamuogopa sana kwani alikuwa mkali. Kuna watu wanashindwa kutofautisha tui na maziwa kwa hiyo wameliwa na wajanja ambao humsingizia Kambarage Uwongo. Kambarage mbatizaji ameleta amani na utulivu na akawasha mwenge (nuru) wa uhuru (MASIHI) Ili wale mashetani wakikutwisha mzigo yeye akutue.
Kama wamekuhadaa usikate tamaa, muamini mungu.
 
Back
Top Bottom