hekimanyingi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2013
- 679
- 573
Nikiwa nyumbani mwanzo kabisa wa likizo yangu hapa nyumbani eneo la Maji ya Chai Wilaya ya Arumeru, Arusha. Wamekuja watoto wa kike watatu ambao wakiwa wameongozana na mama yao mzazi ambaye ni mlemavu wa kusikia na kuongea (bubu). Watu hao ni jamii ya kimasai wanasema wametokea maeneo yanayoitwa Ngabobo wilayani arumeru. Walikuwa wakiomba chakula. Baaada ya kuwahoji kwa muda niligundua ni kweli wanahiji msaada. Niliingia ndani nikawachotea wastani wa kilo 3 za unga wa mahindi nikawapa Tsh 5000/=
Kilichonihuzunisha sana na kufikia hatua ya kuandika uzi huu ni baada ya mabinti wale kuondoka hatua kadhaa kutoka nyumbani walianza kula ule unga wa mahindi mkavu kwa kunyang'anyana. Kwangu imekuwa ni jambo geni sana kwa mtu kula unga mkavu wa mahindi bila kupika.
Wakati mwingine kama wanadamu tunapata chakula na kubakiza hadi kutupa jalalani lakini wapo ambao wanakosa na kudiriki kula hata unga mkavu. Njaa ipo wadau tusaidie wanaokosa chakula badala ya kuwabeza.