Leo nimenusurika katika ajali ya gari

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
14,537
31,692
Wadau,

Leo nilikuwa katika safari zangu za kawaida katika rough road sasa leo mvua ilikuwa imenyesha na kukawa na uterezi. Nimefika kona fulani nikateleza, kutaka kurudi barabarani nikashindwa na nikavamia gema.

Hata sijui gari iligeuka vipi maana nashuka naona imegeukia nilikotoka huko huko kwenye gema.

Hakika Mungu ni mkuu, nimetoka salama kabisa miaka ya karibuni imani yangu imeyumba sana, ila kwa jaribu hili naamini Mungu anakusudi lake.

Wadau tuwe makini sana na haya magari, mimi nilikuwa nachukulia kawaida sana, kilichoniokoa leo ni mkanda, nisingefunga mkanda ilikuwa habari nyingine.
 
Mkuu ujembe umefika tusaidie hivi vitu road license, insurance, fire, stika ya wiki ya nenda kwa usalama, hongera sana.
 
Wadau leo nilikuwa katika safari zangu za kawaida katika rough road..sasa leo mvua ilikuwa imenyesha na kukawa na uterezi...
Nimefika kona fulani nikateleza, kutaka kurudi barabarani nikashindwa na nikavamia gema...

Hata sijui gari iligeuka vipi maana nashuka naona imegeukia nilikotoka huko huko kwenye gema...

Hakika Mungu ni mkuu, nimetoka salama kabisa..miaka ya karibuni imani yangu imeyumba sana, ila kwa jaribu hili naamini Mungu anakusudi lake!!

Wadau tuwe makini sana na haya magari, mi nilikuwa nachukulia kawaida sana, kilichoniokoa leo ni mkanda..nisingefunga mkanda ilikuwa habari nyingine!!
Pole sana Mkuu,
Seat belt ni muhimu sana.
 
Upeo wa Watanzania wengi ni tatizo sana, MTU anaelezea ajali halafu mwingine anasema hongera kwa kumiliki gari. Yaani MTU kuwa na gari mnaona bonge la dili. Umaskini ni tatizo sana na ndo maana wengi mnakuwa na roho mbaya
 
JF una watu mna inferiority complex iliyokubuhu....akili za kimaskini hizi...besides gari si lazima iwe yake..
Ndo hivyo mkuu..kuna watu kila kitu wanafikiri mtu anataka kujionesha..hata kama ni kujulisha watu namiliki gari ndo iwe JF tena na ID fake?
 
Wenye kuelewa tymeelewa achana na hao maboya pole na jirudi kwa Mungu
 
Ndo hivyo mkuu..kuna watu kila kitu wanafikiri mtu anataka kujionesha..hata kama ni kujulisha watu namiliki gari ndo iwe JF tena na ID fake?
Kuna wanafunzi humu....hawajui kuna watu tumeanza kazi wao wakiwa bado vidudu... gari kwao kitu cha ajabu
 
Back
Top Bottom