Leo nimekutana na agizo la kuwaombea viongozi kwenye Biblia, matokeo yake ni amani na utulivu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Katika Kutimiza matakwa ya imani kwamba angalau nipitie mistari kadhaa kabla sijaingia kwenye mapambano ya Maisha, nimejikuta nafunua bibilia nikakutana na...

1Timotheo 2:1-3.

Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote, 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 3 Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,

huwa sijui watu wanapata wapi ujasiri wa kutowaombea viongozi hata kama wanavyovifanya ni kinyume na matarajio yao. Hakuna kosa kubwa na baya ambalo litakufanya uhairishe jukumu hili...
 
jukumu letu ni kuomba uvivu ndio unaleta maneno mengi yasiyofaa ukiomba unaweka ulinzi wa Mungu kwa kiongozi na kwako pia...kelele nyingi ni dalili ya uvivu wa kupiga goti.
Kweli mkuu,
Bibilia inasema "Waombeeni wanowaudhi" leo anaibuka kiongozi wa dini anaamuru Mapepo yaende kwa kiongozi!!!

Kukosoa,Changamoto,Kuwa wakweli juu ya mambo ambayo wenda hayako sawa Hakuchukui nafasi ya Kumuombea Kiongozi.

Maana amani na Utulivu ni kwa faida ya Walemavu,watoto wachanga, wajawazito,Wawekezaji,Vikongwe, Kizazi cha kesho na Wenda amani na utulivu ikawa ni Daraja la kukufikisha kwa Kiongozi unaedhani ni bora zaidi hapo baadae...
 
ni kwa sababu hawalijui neno ingekuwa wanalijua nafikiri wangetenda sawasawa na jinsi neno linavyowaelekeza yapo mambo mengi sana viongozi wetu huyafanya alafu sisi tunabaki kulalamika hivi je umeshawai kwenda mbele za Mungu na kumueleza Mungu kwa ajili ya hilo unaloliona linafanyika kinyume hivi unajua kuwa maombi yako ni ya muhimu sana juu ya amani ya nchi maana hakuna mtu anayeweza kuja hapa akaniambia Amani tuliyonayo kwa sasa ni kwa uwezo wetu sisi wanadamu ila na jua kwa sababu ya wale wachache wanaokesha usiku na mchana wakiomba kwa ajili ya Amani ndio maana twaiyona hii tuliyonayo kwa hali unayoiyona jua wako watu wanaolia mbele za Mungu mchana na usiku wakiibeba nchi mbele za Mungu ni jukumu la kila mtu kuiombea nchi pamoja na viongozi wote aijalishi kuwa kiongozi kafanya nini wewe muombe tu maana Mungu ndie kamuweka pale na yeye ndie mwenye uwezo wa kummbadilisha .viongozi wanapoelewana wenyewe kwa wenyewe au wanapokuwa na ummoja basi matunda yake tutayaona hata kwa mwananci mmoja mmoja embu suala la kuiombea nchi na uongozi wa nchi uwe mzigo kwako kila upatapo nafasi.Mungu akubariki kwa hilo.
 
Katika Kutimiza matakwa ya imani kwamba angalau nipitie mistari kadhaa kabla sijaingia kwenye mapambano ya Maisha, nimejikuta nafunua bibilia nikakutana na...

1Timotheo 2:1-3.

Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote, 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 3 Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,

huwa sijui watu wanapata wapi ujasiri wa kutowaombea viongozi hata kama wanavyovifanya ni kinyume na matarajio yao. Hakuna kosa kubwa na baya ambalo litakufanya uhairishe jukumu hili...
binafsi sijawahi kumuombea rais wala kiongozi yeyote yule. sioni kama ni jambo akili. nafikiri cha kufanya katika maisha yangu ni kumwomba Mungu anipiganie na kunitetea tu ili waovu na waonezi wasiniumize tu basi. waovu wanaweza kuwa rais, mawaziri, wala rushwa na kadhalika. huwa sichelei kumwombea kiongozi yeyote kwasababu nina uhakika wakati mimi naomba kwa Mungu aliye hai, Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, yeye anakusanya kundi la waganga, wachawi, wasoma nyota, wakuu wa anga, wakuu wa giza, falme na mamlaka na majeshi ya pepo wabaya wamlinde na kumpigania kwenye uongozi wake.ni viongozi wachache sana duniani hawamwabudu shetani either kupitia waganga wa dunia, au free masons etc. naweza kusema kama si wachache basi hawapo kabisa wanaoishi kwa kumtegemea Mungu per se.

sasa kama mtu anatumainia wachawi na waganga wa kienyeji, mizimu na mashetani kumlinda na kumpigania, kwanini mimi nisumbuke kumwombea? kwani Mungu anachangamana na mashetani na wachawi/waganga? sasa kama mambo yakienda vizuri tujue aliyesaidia ni Mungu au hao wachawi/waganga wake? wakati wewe unasugua goti, wenzio wanatapanya hela na mafuta ya magari kwenda kusomba vizee vichawi huko maporini. Mungu hachangamani, na siwezi kupoteza muda kama huo kumwombea mtu. nisije kuomba mashambulizi dhidi ya nguvu za giza na yeye akashambuliwa pamoja nayo.

jambo pekee nitakalofanya ni kuiombea nchi, Mungu aitetee nchi yetu, atetee wanyonge wasio kuwa na mtetezi, awasaidie wasio kuwa na uchumi mzuri ili wenye uchumi mzuri wasiwaonee, Mungu atokee kuwatetea. siwezi kuwaombea viongozi...niwaombee kwa lipi? kwamba Mungu awapatie uchumi mzuri?...hahaha, wakati wameiba, wamekula rushwa na wanaishi kwa pesa za udhalimu?

niwaombee nini yaani? ulinzi? wakati wanalindwa na mashetani, waganga na wachawi pamoja na majeshi yote ya Tanzania....cha maana ni kuomba Mungu atutetee wasituonee tu. 100% ni waovu, wachawi na hawamwamini Mungu na siku zote hata kama hawasemi, mioyoni mwao ni wapinga kristo, wanapinga mambo ya kimungu kwasababu roho iliyo ndani yao ni roho ya mpinga kristo inayotawala dunia hii.

ninachoomba pekee, kama wakiwa wanatuonea, wanatudhalilisha bila haki, Mungu awafutilie mbali, Mungu atume radi na moto, na upanga ukatao kuwili dhidi yao akawafyeke mara moja na kumbukumbu lao lisionekane tena, ili tuweke watu wanaomhofu Mungu watutawale. ili tuweke watu wasio wachawi, wasoma nyota na waganga watutawale, ili mapinga kristo yasitutawale tena. Kwa Jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.Amin.
 
ni kwa sababu hawalijui neno ingekuwa wanalijua nafikiri wangetenda sawasawa na jinsi neno linavyowaelekeza yapo mambo mengi sana viongozi wetu huyafanya alafu sisi tunabaki kulalamika hivi je umeshawai kwenda mbele za Mungu na kumueleza Mungu kwa ajili ya hilo unaloliona linafanyika kinyume hivi unajua kuwa maombi yako ni ya muhimu sana juu ya amani ya nchi maana hakuna mtu anayeweza kuja hapa akaniambia Amani tuliyonayo kwa sasa ni kwa uwezo wetu sisi wanadamu ila na jua kwa sababu ya wale wachache wanaokesha usiku na mchana wakiomba kwa ajili ya Amani ndio maana twaiyona hii tuliyonayo kwa hali unayoiyona jua wako watu wanaolia mbele za Mungu mchana na usiku wakiibeba nchi mbele za Mungu ni jukumu la kila mtu kuiombea nchi pamoja na viongozi wote aijalishi kuwa kiongozi kafanya nini wewe muombe tu maana Mungu ndie kamuweka pale na yeye ndie mwenye uwezo wa kummbadilisha .viongozi wanapoelewana wenyewe kwa wenyewe au wanapokuwa na ummoja basi matunda yake tutayaona hata kwa mwananci mmoja mmoja embu suala la kuiombea nchi na uongozi wa nchi uwe mzigo kwako kila upatapo nafasi.Mungu akubariki kwa hilo.
Kwenye bibilia kuna mifano mingi Jinsi maombi ya wananchi yalivyogeuza hatari kuwa amani na Utulivu
1:Ninawi waliomba mji haukuharibiwa...
 
Katika Kutimiza matakwa ya imani kwamba angalau nipitie mistari kadhaa kabla sijaingia kwenye mapambano ya Maisha, nimejikuta nafunua bibilia nikakutana na...

1Timotheo 2:1-3.

Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote, 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 3 Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,

huwa sijui watu wanapata wapi ujasiri wa kutowaombea viongozi hata kama wanavyovifanya ni kinyume na matarajio yao. Hakuna kosa kubwa na baya ambalo litakufanya uhairishe jukumu hili...
Kwanini tusitumie muda wetu kumuombea shetani aache kuwafanya viongozi wetu kuwa na majivuno, kibri na kukurupuka
Nijuavyo mm huyo kiumbe shetani ni chanzo cha hayo yote
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Ukiona kiongozi wa dini anahubiri CHUKI kwa viongozi wa kisiasa, au Muumini anakuwa na Munkari na chuki kwa kiongozi
na kukata tamaa jua anakwepa wajibu huu aliopewa.

NI JAMBO JEMA NA LAMPENDEZA MUNGU...
kaka umesahau kuwa hao waliokuwa wanaombewa kwenye huo mstari, walikuwa wafalme wa enzi zile, sio hawa wa sasa. sio kina bashite na kina pombe. ni walee? inawezekana kabisa behaviours za wafalme na watawala wa kipindi kile ni tofauti na hizi za sasa. inawezekana kabisa wale wa kipindi kile walistahili kuombewa na pengine hawa hawastahili. kila jambo linatakiwa litathiminiwe kwa wakati wake.

unakumbuka kipindi cha Paulo/saulo, na enzi zote za mitume, unakumbuka pia kipindi cha herode aliyejiinua na kutukuzwa na wanadamu, jinsi Mungu alivyomsambaratisha kwa chango akafa na kudhalilika mbele ya kadamnasi. wapo viongozi wengi tu wa dunia hii ambao hakika walikua maadui wa Mungu, na Mungu aliwashughulikia. hivyo, sio kila kiongozi unatakiwa kumsikiliza, kuna wengine unatakiwa kuomba Mungu awasaidie, na kuna wengine unatakiwa kuomba Mungu ashuke amshambulie ili watoto wake tupone. ninasema amshambulie kwasababu hapa duniani kuna wanadamu wa aina nyingi sana, kuna wengine tunaishi nao ni wanadamu wa kawaida tu na marafiki wa Mungu, ila kuna viongozi wengine au wanadamu wengine ni maajenti wa shetani, na wanaishi wakijua wao ni maajenti wa shetani, wameingia mkataba na shetani, wanakula nyama za watu, wanauwa watu wanafanya uovu wa kila aina. mtu kama huyo naye ambaye ni ajenti anaenda kuripoti kabisa kwa shetani naye anaweza kuwa kiongozi. hivyo huyo naye unatakiwa kumwombea wakati kazi yake anakuvizia kuua kuchinja na kuharibu? si kuomba Mungu atukomboe toka mkonini mwake?

sasa watu kama hao ndio wamejaa kwenye uongozi wa nchi za africa na dunia nzima. hata ukiona wanajifanya kwenda church ni unafiki tu. hata bashite (kama ndio wewe uliyeandika hapa) kujifanya unaenda kanisani ni unafiki tu, umeshakuwa ajenti na siku ya anguko lako ipo na inakuja. mwombe Mungu akubadilishe, uache kiburi kama cha herode hicho, uache kiburi kama na nebukadreza kabla Mungu hakakusambaratisha au kukubadilisha iyo akili ukawa chizi ukala majani kama ng'ombe miaka 7 kama alivyosambaratishwa nebukadreza mfalme wa baabeli akala majani ya mwitu na kuota nywele kama hayawani/mnyama wa porini. mmeshakuwa maajenti ndio maana mnajifungia chumbani masaa hata 7, mnajadili nini? au mnaenda kuzimu? siku ya anguko lenu ipo na inakuja. Mungu amewainue, mlivyoona mpo juu, mkamtupa kule mkamwacha hata aliyewainua toka kwenye umasikini na kuonewa. yeye aliye juu anawaonya, badilisheni njia zenu, kucheka kwenu kubadilike kuwa kulia, sauti zenu za sherehe na ziwe maombolezo yamkini hasira yake itapungua dhidi yenu. Mungu akusaidie.
 
Uelewa wako ni finyu sana
 
Uelewa wako ni finyu sana
kipimo gani umetumia? vyovyote utakavyosema, huwezi kumchanganya Mungu na wachawi na wanaotegemea waganga wa kienyeji. nitakachoomba Mungu hapo mimi ni kuwasambaratisha ili waondoke madarakani tupate wapya wanaomjua Mungu. huwezi kumwombea mtu anayetumainia waganga wa kienyeji, Mungu hawezi kuchangamana na mashetani kufanya jambo. hivyo ninyi mlioamua kupoteza muda kuwaombea hao jamaa, endeleeni, ni muda wenu. sisi wengine katu hatuna muda wa kupoteza kama huo.
 
Ndio maana nikakwambia hujui chochote juu ya kumuombea mtu.
 
ndio kanuni ya ukristo ilivyo katika kila ibada zetu za juma lazima kiongozi wa nchi wa wakati huo aombewe na waumini wote bila kujalisha itikadi zao,pia maombi ndio njia pekee kwa mwanadamu kuwasiliana na Mungu aliye mkuu aketiye mahali patakatifu ndio maana wa kristo tunaagizwa kuwaombea hata wale watutendeao mabaya
 
Ndio maana nikakwambia hujui chochote juu ya kumuombea mtu.
wewe unayejua unaelewa nini? tatizo mnakariri, hata Mungu hamumjui. tuambie wewe uelewa wako ukoje kwenye kuwaombea hao wanaoenda kwa waganga wa kienyeji? kuwaombea waokoke wasiende tena au kuwaombea Mungu aambatane na nguvu zao za giza katika kuwalinda?
 
Back
Top Bottom