Leo ni Siku ya Valentine: Je unafahamu asili na maana yake?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Maalum kwa wale ambao bado hawafahamu

*Mtakatifu Valentino*
Mtakatifu Valentino alikuwa ni padre wa Roma (Italia) ambaye aliishi kwa kuishuhudia imani ya kikristo kati ya mwaka 197 na 273. Kanisa linamtambua kuwa ni shahidi wa imani kwa kuwa alitoa uhai wake kwa kuilinda, kuitetea na kuitangaza imani ya kikristo. Lakini pia Mtakatifu Valentino anajulikana duniani kote kuwa ni mtakatifu wa wapendanao. Kwa hiyo utakatifu wake katika historia ya Kanisa na umaarufu wake duniani kote ni mambo mawili yanayojikitika katika jambo moja la msingi kwa maisha ya mtu wa dini yeyote na mahali popote; jambo hilo ni imani.

Valentino aliongoka katika ujana wake na kubatizwa mnamo mwaka 197 na baadae akawa Padri kwa kuiishi imani ya kikristo mpaka mwaka 273 alipouawa kwa ajili ya kuitetea imani. Imani hiyo ya kikristo aliishi si tu kwa maneno bali pia kwa vitendo kwani wakati ule kuwa mkristo ilikuwa ni jambo gumu sana. Ugumu huo ulitokana na ukweli kwamba watawala wa Kirumi wa nyakati hizo walikuwa bado hawajaipokea imani ya kikristo. Valentino aliishi imani ya kikristo nyakati za mfalme Claudio ambaye mara kadhaa alimtesa na kumfunga gerezani na baadae aliuawa kwa amri ya mfalme Aureliano. Utakatifu wake Mtakatifu Valentino anatambulika na wengi duniani pote kwa sababu ya upendo wake kwa watu. Tabia yake ya kupenda watu ilijikita katika imani yake kwa Neno la Yesu, “Amri yangu ndiyo hii: Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yoh. 15:12-13).

Mtakatifu Valentino alitumia muda wake mwingi kuwasaidia watu wa ndoa na vijana wachumba kwa kuwafundisha juu ya upendo. Aliwafundisha kuwa upendo ni fadhila kuu ya kikristo na kiutu, kwa hiyo alisisitiza kuwa upendo ni kielelezo cha imani na utu. Watu wa ndoa aliwafundisha kuwa upendo wao hujionesha katika mambo makuu mawili: uaminifu na umoja. Uaminifu wa viapo vya ndoa katika kupendana na kuheshimiana siku zote na kwa hali zote. Umoja katika kutambua kuwa ndoa ni kati ya mume mmoja na mke mmoja. Mtakatifu Valentino aliishi nyakati ambazo ndoa za mume mmoja na wake wengi zilikuwa ni kama jambo la kawaida. Wanawake walinyimwa upendo ndani ya ndoa zao na wakawa wanyonge mbele za waume zao. Yeye alikemea jambo hilo bila kujali mtu yeyote; watawala kwa mfano, walikuwa pia na tabia hiyo ya kukosa uaminifu kwa ndoa zao. Polepole watu wengi walianza kujirekebisha na upendo ukaanza kurudi ndani ya ndoa. Hata hivyo mfalme Claudio alimchukia Valentino na kumfunga gerezani.

Wachumba aliwafundisha kuwa upendo wa kweli wa wapendanao hujidhihirisha katika kufunga ndoa mbele ya Mwenyezi Mungu. Hivyo basi aliwakemea bila woga vijana wengi waliokuwa wanaishi maisha ya unyumba. Vijana wengi waliongoka na kufunga ndoa takatifu kanisani. Jambo hili pia lilimkera sana mfalme kuona kwamba watu wengi wanaingia katika dini ya kikristo. Pia aliwatetea vijana waliokuwa jeshini ambao walikatazwa kwa sheria ya mfalme wasifunge ndoa. Sheria hiyo iliwanyima wanajeshi maisha ya ndoa kwa imani kuwa askari hodari hawatakiwi kuishi maisha ya ndoa.

Mtakatifu Valentino alipigania haki ya hao askari na kuwataka watawala waibatirishe sheria hiyo potovu. Katika kuwasaidia watu wautambue utakatifu wa ndoa, Mtakatifu Valentino alifanikiwa kuwafungisha ndoa wachumba wawili (mmoja mkristo na mwingine alikuwa mpagani) ambao wazazi wao walikuwa wamewawekea vikwazo. Mchumba wa kike ambaye ni mkristo alikuwa mgonjwa na yule wa kiume ambaye ni mpagani alikuwa ni askari. Askari aliwaambie eti si vizuri aoe kwani maisha yake yamo daima hatarini na hasa wakati wa vita na hivyo atamwacha mkewe kuwa mjane.

Na yule binti pia aliambiwa asiolewe eti kwa kuwa yeye ni mdhaifu na hivyo anaugua mara nyingi itakuwa ni vigumu kwake kutimiza wajibu wake wa nyumbani. Mtakatifu Valentino aliingilia kati na kuwafundisha wazazi wa vijana hao kuwa upendo hauna mipaka wala ubaguzi. Na pia wale wachumba akawafundisha kuwa katika ndoa ni lazima kupendana katika taabu na raha, afya na magonjwa, na kuheshimiana daima. Mtakatifu Valentino alifaulu kumbatiza askari na kumfungisha ndoa kwa yule binti ambaye alikuwa taabani mgonjwa kitandani.
Ushahidi wake Mnamo mwaka 269 mfalme Aureliano alimkataza rasmi Valentino kuhubiri, kuwaongoa na kuwafungisha ndoa takatifu. Mtakatifu Valentino aliendelea kumshuhudia Kristo bila woga na akawa tayari kwa lolote ila tu upendo wa Kristo uhubiriwe. Mwaka 270 mfalme alimhukumu Valentino adhabu ya kufungwa gerezani kwa miaka mitatu.

Urithi wake

Mtakatifu Valentino ametuachia urithi mkubwa wa imani. Mtakatifu Valentino anatufundisha kuwa fadhira ya upendo ni kielelezo cha imani. Mtu yeyote mwenye imani humpenda Mungu na huwapenda wenzake. Kipimo cha imani na kipimo cha utu ni upendo. Dunia inahitaji sana upendo ili mambo mengine mazuri yawezekane.
Mtakatifu Valentino alitambua kuwa watu wa familia wanapopendana jamii yote itapendana na kuishi kwa amani. Anatufundisha kuwa upendo huanzia nyumbani, yaani kati ya wanafamilia.
Ndiyo maana aliwataka watu wa ndoa wapendane katika misingi ya imani na wafunge ndoa takatifu.

Leo hii watu wengi duniani pote wanaikumbuka tarehe ya 14 februari kuwa ni siku ya wapendanao. Je, wanatambua kwa nini Valentino alitoa uhai wake siku hiyo?

Tunatakiwa tupendane kwa upendo wenye msingi katika imani kama alivyofundisha mtakatifu Valentino. Siku ya Mtakatifu Valentino ni siku ya wapendanao katika misingi ya imani na utu.
Kwa bahati mbaya watu wengi katika maisha ya leo tunapendana katika misingi ya tamaa za kimwili na kimapato. Leo hii kuna watu wengi wa ndoa ambao wana nyumba ndogo lakini nao wanasema eti leo ni siku yao ya WAPENDANAO. Ni upendo gani huo wenye nyumba kubwa na ndogo?
Je, Valentino hakufa kwa kupinga jambo hilo? Vijana wengi leo wanaishi uchumba sugu bila kufunga ndoa. Lakini wao pia wanasema eti leo ni siku yao ya wapendanao. Ni upendo gani huo pasipo msingi wa imani. Je, valentino hakutoa uhai wake ili kuwafundisha na kuwapigania vijana wafunge ndoa takatifu? Ni ajabu kuwa siku ya Mtakatifu Valentino uovu mwingi dhidi ya upendo ndiyo hufanyika. Ni vema siku hii iwe kwa ajili ya kujikumbusha maana halisi ya upendo. Wakati ule Mtakatifu Valentino alikwazika sana kuona watu wanaishi pamoja bila kufunga ndoa, alikwazika kuona vijana watu wa ndoa wanakosa uaminifu katika ndoa zao. Na alisikitika kuona hata vijana wanakosa haki za kuuishi upendo wa ndoa. Lakini akija leo hii, mtakatifu Valentino atashindwa hata kushangaa kuona jinsi upendo ulivyogeuzwa kuwa ni starehe ya kimwili badala ya kuwa ni fadhila ya kimungu.

Na mbaya zaidi atakutana na watu wa jinsia moja (ushoga na usagaji) wanaodai eti wanapendana na wana haki ya kufunga ndoa. Katika siku hiyo Mtakatifu Valentino anatukumbusha tena kuwa upendo ni fadhila ya kimungu na sio starehe ya kimwili.
IMG-20200213-WA0113.jpeg


Jr

Maswali fikirishi
Je Valentine day ni sikukuu ya kiimani/kidini?
Je Valentine day ni mojawapo ya kielelezo kuwa mfumo Kristo unatawala dunia?
Je kwanini siku hii imetekwa na imani zote kwa baadhi ya nchi na kuigeuza siku ya ngono na ufuska?
Je kwanini siku hii inazidi kupoteza mvuto mwaka hadi mwaka?
 
Naomba unikosoe kwa heshima na kwa hoja.. Kama unaona nimeandika uongo nikosoe kwa kuandika ukweli... Siandiki kila kitu ila kwakuwa unapenda kunifuatilia maandishi yangu ndio maana unadhani naandika kitu ambapo pia unadanganya kwakuwa huwezi kutoa ushahidi wa mimi kuandika kila kitu... Labda uniambie tuna tafsiri tofauti ya KILA KITU
umendika uwongo usipende sana kila kitu uandike hata kama huna ujuzi au elimu nacho we andika kuhusu majini na mapepo machafu vingime vinahitaji kina cha elimu hapa umedanganya rudi deep then andika tena

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Ingekua watu wakifanya mapenzi inatoka milio ya risasi, basi leo hali ingekua kama siku za vita ya pili ya dunia! Leo hakuna kimasihara, ni full kudhamiriana!
 
Huyo mtakatifu alitafutiwa tu kupachikwa hapo tu ili kuficha ukweli. Kuna sehem inasema alizaliwa au alikufa au alifungisha ndoa tar 14 Feb? Ukweli wengi tusioujua ni huu:



Mwezi wa pili yaani February ni jina la mungu wa Ki-roma ambapo kwa wakati huo walimwita kama Februus yaani god of purification wakiwa na maana kwamba mungu wa Utakaso,walikuwa wanamtegemea katika kila kitu na ndiyo maana sherehe zao nyingi zilifanyika mwezi wa Pili yaani February uku jina la February ni jina la mungu wao na baada waliamua kuita mwezi wa pili kama February maana ni jina a mungu wao na hivyo Kwa nini Valentine day inasherekewa mwezi wa pili ni katika mwendelezo wa kumuenzi mungu wa kiroma aliyekuwa anafahamika kama Februus na ikumbukwe kwamba wakati huo bado hakuna dini yoyote ile watu walikuwa na miungu yao binafsi hivyo neno february ni jina la Mungu wa kiroma miaka 5000 ilyopita.

MPAKA kesho hata kalenda tunazotumia majumbani kwetu Ni majina ya watu na miungu wa zamani,unaposherekea sikukuu ya Valentine's ambayo haitambuliki na nchi yoyote Ile bali Imepewa nguvu na makampuni na Midea ili wapige hela ww uendelee kubaki KUWA masikini ,Mwezi FEBRUARY Ni JINA la Mungu wa Kiroma aliyefahamika Kama Februus ama Februa .
Naomba unikosoe kwa heshima na kwa hoja.. Kama unaona nimeandika uongo nikosoe kwa kuandika ukweli... Siandiki kila kitu ila kwakuwa unapenda kunifuatilia maandishi yangu ndio maana unadhani naandika kitu ambapo pia unadanganya kwakuwa huwezi kutoa ushahidi wa mimi kuandika kila kitu... Labda uniambie tuna tafsiri tofauti ya KILA KITU

Jr
Soma vizuri uelewe


VALENTINE DAY ZILIKUWA NI SHEREHE ZA WAPAGANI WAKIWAENZI MIUNGU YAO ENZI ZA MFALME JULIUS CAESAR,MWEZI FEBRUARY LILIKUWA JINA LA MUNGU WA UTAKASO KATIKA UTAWALA WA KIRUMI.

Mpoki Buyah Kaminah (Sehemu ya I).

Miaka ya nyuma Waromani walikuwa na tamaduni zao na sikukuu zao pia,Kila baada ya mda fulani,Mara nyingi walikuwa wanasherekea baada ya Mavuno,na kulingana na Calenda yao (Pre Roman Calender) walifanya sherehe hiyo mwezi wa Pili yaani February ambapo kwa wakati huo mwezi february ulikuwa unajulikana kama Februarius kulingana na Romani Kalender ya wakati huo, kuanzia tarehe 13-14 na baadae tarehe hizo zilibadilika kulingana na mabadiliko ya Kalender yao wenyewe na ulikuwa ni utamaduni wa waroma kufanya sherehe nyingi ikiwemo kutambika na kutoa kafakara za wanyama kwa ajili ya kulinda mipaka yao na sherehe hizo zilianza kuenea na kubadilika majina na hata baada ya Dini sherehe hizo zilibadilishwaa jina lakini tarehe ilibaki pale pale yaani tarehe 15.

Mwezi wa pili ulikuwa ndiyo mwezi mfupi yaani Shortest month in Roman Calender lakini hata sasa mwezi huo ni mfupi kwa kuwa na siku 28,Hata hivyo Julius Caesar mtawala wa ngome kuu ya Roma ama Roman Empire alibadilisha Calender hiyo na sherehe hiyo kuanza kusherekewa february 15 hapa ilikuwa mwaka 46BC lengo kuu ni katika kumuenzi mungu wa utakaso ambaye alikuwa ndiyo Mungu wao, lakini hata hivyo miaka hiyo haikufahamika kama Valentine Day bali ilikuwa ni sherehe ya Mavuno pia yaani "Agricultural Celebration" huo ndiyo ulikuwa utamaduni wao japo sherehe hii imekuwa ikibadilika badilika kulingana na wakati na mpaka kufikia kuitwa Valentine Day kuna matukio mengi yamefanyika tofauti na Upotoshaji ambao umekuwa ikiandikwa juu Valentine Day.

Mbali na kwamba walikuwa wanasherekea juu ya Mavuno lakini pia Warumi walisherehekea siku hizo kwa lengo la kudumisha suala la uzazi kwa kutambikia wanyama na kutoa kafara kwa miungu yao,huo ulikuwa ni Utamaduni wao hata katika kipindi cha Caesar na baadae pia utamaduni huo ulikuwa anasambaa sana.Siku hizo ziliambatana matendo mbalimbali kama vile Wavulana kuvaa mikia ya wanyama na kujipaka damu ya wanyama wakiwa karibia nusu uchi wakiwakimbiza wasichana kwa kuwapiga mgongoni mtaani hiyo ilikuwa ni utamaduni wao,Matendo yao ya kuhusisha wanyama na mahusiano ulikuwa ni kumbukumbu ya muasisi Wa mji mkuu Wa Italy yaani Roma aliyefahamika kama Romulus kwa wakati huo ambaye inasadika Kuwa alinyonyeshwa na mbwa mwitu wakali akawa na ushupavu au ushujaa katika kuongoza nchi lakini ni miaka ya nyuma sana kabla ya Ujio wa Ukristo na ndiyo maana kuna ambao wanaona VALENTINE DAY ni sikukuu ya Wapagani (Paganism).

Kuna taarifa ambayo inaelezea kwa kina sana chimbuko la siku hii ya Valentine day,tunajaribu kutafiti ili kupata mtiririko sahihi lakini hata hivyo kuna mkanganyiko mkubwa sana na kulingana na mkanganyiko huu ndiyo hapo Valentine Day inaonekana kama sikukuu ya Wapagani.Okei twendeni mbele kidogo kuna kisa kingine hapa ambacho kinaonekana kama Chimbuko la Valentine Day,Katika miaka hiyo hiyo ya nyuma kabla ya Ujio wa Dini Waroma walikuwa wanaliwa sana na mbwa mwitu wenye hasira kali ambao walikuwa wanaishi porini na mida ya Usiku walikuwa wanashuka mtaani ama vijijini kuja kushambulia na kuuwa watu vijijini,Mbwa mwitu hao walikuwa wakali kuliko kawaida na kupelekea waroma kukosa amani na kuishi kwa wasi wasi mno.

Hata hivyo kulingana Waroma miaka hiyo ya 44BC walikuwa na Miungu yao maana hapa tunazungumzia kabla ya Ujio wa Dini hii ya kikristo ama dini nyingine yoyote ile hivyo waroma walikuwa wana miungu yao ambayo ilikuwa inawasaidia katika kutatua matatizo yao katika jamii zao,Sasa Waroma walianza kuwalilia miungu yao ili kuwafukuzuia mbali mbwa mwitu hao waliokuwa wanakula watu,Mungu wa Waroma kwa wakati huo alifahamika kama LUPERCUS na huyo ndio alikuwa Mungu wao na baada ya maombi yao na kumlilia Mungu wao huyo aliyejulikana kama Lupercus aliwajibu waroma na hatimae mbwa mwitu hao waliacha kuwashambulia Waroma na kuanzia hapo Waroma walianza kusherekea na kulingana na Kalenda yao ya zamani shere hiyo ilianza kufanyika katikati ya mwezi wa pili kuanzia tarehe 13,14 kwenda 15.

Huo ndiyo ukawa mwanzo wa waroma kuanza kusherekea Siku hiyo ambayo kwa wakati huo ilifahamika kama LUPERCALIA lakini baada sikukuu hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa Valentine Day kwa leo wanaita sikukuu ya Wapenda nao Duniani Kote.Hata hivyo Sikukuu hiyo pia iliambatana na kuwaomba mungu wao awaepushe na mikosi,njaa pamoja na magonjwa katika taifa lao,sherehe hizo zilifanyika karibia na viongozi wote wa Roma,hata hivyo lengo la sherehe hizo kufanyika mwezi wa pili ni katika kumuenzi mungu wao mwingine ambaye alikuwa anatumika ama kuabudiwa miaka mingi sana kipindi cha Julius Caesar na Viongozi wengine wa kiroma miaka hiyo,asili ya Valentine Day ni kwamba sikukuu hiyo inaonekana kuwa sikukuu ya wapagani kwa maana kwamba alianzishwa kabla ya dini kuja duniani.

Mwezi wa pili yaani February ni jina la mungu wa Ki-roma ambapo kwa wakati huo walimwita kama Februus yaani god of purification wakiwa na maana kwamba mungu wa Utakaso,walikuwa wanamtegemea katika kila kitu na ndiyo maana sherehe zao nyingi zilifanyika mwezi wa Pili yaani February uku jina la February ni jina la mungu wao na baada waliamua kuita mwezi wa pili kama February maana ni jina a mungu wao na hivyo Kwa nini Valentine day inasherekewa mwezi wa pili ni katika mwendelezo wa kumuenzi mungu wa kiroma aliyekuwa anafahamika kama Februus na ikumbukwe kwamba wakati huo bado hakuna dini yoyote ile watu walikuwa na miungu yao binafsi hivyo neno february ni jina la Mungu wa kiroma miaka 5000 ilyopita.

Mungu wa Julius Caesar ambaye pia alifahamika kama Februa ama Feburualia ndiyo mungu alikuwa anaabudiwa hakika karne nyingi sana miaka hiyo yaani miaka ya 44BC mungu Februus anambatanishwa sawa na mungu mwingine ambaye alifahamika kama Etruscans,miaka ya 44BB na kuendelea kama nilivyoelezea katika sehemu ya kwanza,hivyo na sikukuu hiyo iliyofahamika kama sikukuu ya utakaso yaani "Februa Festival of Purification" lakini pia waroma walikuwa na miungu wengi ambapo alikuwepo pia mungu wa mabonde,mungu wa mabonde misitu na tambalale ambaye aliitwa Faunus hivyo katika sherehe hizo waliwaunganisha miungu ya miwili yaani mungu faunusi na mungu februus na wote hawa waliwasherekea kwa pamoja mwezi wa pili (February/Februalia) na walitambika na kutoa sadaka wanyama na vitu vingine vingi na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kusherekea sikukuu hii mwezi wa pili kuanzia tarehe 13,14 mpaka 15 na ndiyo maana pia inatambukilika kama sikukuu ya wapagani.

Kuna hii nadharia pia ambayo watu wanajaribu kuifafanua juu ya kile kinachoitwa sikukuu ya wapenda nao yaani "Valentine day"ambapo jina Valentine ni jina la Mtumishi wa Mungu aliyokuwa anafanya kazi katika utawala wa "Roman empire" na hawa mapadre waliibuka baada ya kuanza kuenea kwa dini ya kikristo katika utawala wa roma ambapo taratibu walianza kuacha dini yao ya asili na kuanza kuukaribisha ukristo japo katika miaka hiyo Ukristo ulipata upinzani mkali sana kutoka Serikali ya roma ila baadae waliukubali na ndiyo ikawa dini ya kuu kwa sasa wanaita ukatoliki (Roman Catholic) lakini baadae watu wengi walikufa na wengine kufungwa kwa kosa la kueneza Dini hiyo ya Ukristo.Twende kwenye baadhi ya taarifa juu ya chimbuko la Valentine,Sherehe hizi zilikuwa ndani ya mafundisho ya Valentine aliyekuwa padre kuanzia mwaka 197 AD.

Baada ya Ukristo kuingia kwa warumi , Mfalme Claudius II alikuwa anahitaji Kuwa na taifa lenye Vijana shupavu,wakakamavu na wenye nguvu akiwataka Vijana wengi kujiunga na jeshi na aliwasisitiza wasije kujaribu kuoa maana kwa mtazamo wa mfalme Cloudius II hakutaka watu waliokuwa wameoa jeshini maana aliamini kwamba akioa anapoteza ule uhalisia wake na utendaji wa kazi unapungua jeshini na inakuwa raisi kushindwa vitani,Kulingana na utamaduni huo Vijana wengi walionekana kutopenda utaratibu huo, hawakuonesha mwitikio kwasababu hawakupenda kuacha familia zao nyumbani.Hapo ndipo historia nzima ya Valentine inapoanzia inasemekana kwamba Valentine alianza kumpinga mfalme Cloudius II,hakuunga mkono suala la Mfalme na Valentine aliendelea kuwafungisha ndoa vijana kwa Siri hata hivyo taarifa zilivyotapakaa Valentine alikamatawa na kuwekwa ndani.

Kwa kuwa Padr. Valentine alihukukiwa kwa kigezo hicho inasadikika alipata watu wengi waliokuwa wakienda kumuona gerezani kwa wakati huo Wakimpelekea maua kwa ishara ya upendo na umoja,Miongoni mwa watu wengi waliokuwa wakienda kumuona alikuwemo mtoto wa mkuu Wa gereza, kuna taarifa ambazo hazina uhakika wa moja wa moja bali ni kama upotoshaji tuu,taarifa hizi zindai kwamba Padre Valentine alijikuta anatembea na mtoto Wa mkuu huyo kwasababu yeye alikuwa anaruhusiwa kuingia ndani ya gereza pasipo mashariti ya askari wadogo wadogo kama unavyojua kwenye tawala za kifalme
taarifa zinadai kwamba Valentino alikuwa anafanya naye Mapenzi kwa Siri na mtoto huyo kwa siri , si tu kwa kumuogopa Mkuu Wa gereza.

Kabla muda wake Wa kunyongwa tarehe 14 /02/270AD Valentine,taarifa hizi ambazo haziaminiki sana zinadai kwamba aliandika barua kwa mtoto Wa mkuu Wa gereza ambaye alikuwa mpenzi wake ,Barua hiyo ilisainiwa kwa damu yake , alitia sahihi kwa damu iliyosomeka
"FROM YOUR VALENTINE" ,Baada ya hapo , Vijana wengi walianza kumuona Padre .Valentine kama shujaa Wa haki ya ndoa kwani ndicho chanzo cha kunyongwa kwake,na kutokana ushajaa huo watu wa nyakati hizo waliamua kuunganisha kumbukumbu za valentine katika sherehe zao za miaka yote ambazo zimekuwa zikifanyika kuanzia tarehe 13,14 kwenda mpaka tarehe 15 ya mwezi wa pili .Vijana waliokuwa wakimuenzi mtu huyo ( Mtetezi Wa haki ya ndoa ) ndipo mwaka 496 AD Siku hiyo ya tarehe 14 mwezi Wa pili ilitangazwa rasmi na Papa Gelasius kama Siku rasmi ya kumuenzi Padre Valentine lakini hata hivyo wakina Valentine walikuwa wengi sana kwa wakati huo,na shida nyingine waliamua kuunganisha sherehe hiyo katika sherehe zao za asili ambazo zilikuwa sherehe za matambiko kwa miungu yao waliokuwa wanaiabudu ndiyo maana siku hii ya Valentine ina utata mwingi kutokana na tarehe ya sherehe husika na hata hivyo hakijaonekana kukamilika kwani kuna upotoshaji mkubwa juu ya Padre Valentine.

Mwaka 1400 AD ikaanzishwa mahakama ya ndoa iliyosimamia haki za ndoa Kama mbadala Wa Padre.Sherehe hizi hufananishwa Kuwa chimbuko lake ni sherehe za kipagani kama ambavyo nimeeleza Kuwa awali kabla ya ukristo sherehe hizi zilikuwepo zikapotea baada ya ujio Wa ukristo licha ya kwamba mafunzo hayo yalienziwa na kufundishwa na Valentine. Lakini hiyo siyo hoja ya msingi ya kumfunya mtu asisherehekee Siku hiyo kwasababu hata kabla ya ujio Wa dini zetu sote ,tuliabudu miungu ambapo baadhi ya mambo tuliyokuwa tunafanya tulihama nayo baada ya ujio wa dini zetu na bado tunayaona matakatifu,pengine tatizo linawezekana lisiwe Sikuu ya Valentine day ila shida inaweza kuwa tarehe ya sherehe husika maana ina historia ngumuu juu ya miungu ya Kiroma kwa wakati huo hata hivyo sherehe imeanza kupoteza umaarufu wake katika baadhi ya mataifa japo maeneo mengine ndiyo inanoga haswa hususani Afrika na Marekani.

inaendelea sehemu ya II

Wako.
Mpoki Buyah Ndagasya
Email:mpokibuya@gmail.com
Email:Mpokibuyah@gmail.com
No. 0762155025
No.0624027362.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sundoka hizi habari kwa hakika ya uhalisia wake sote sisi hatuna ithibati nazo. Ni habari za kmapokeo tunasimuliwa tuu.. Kwa mfano iliyo maarufu ni hiyo niliyoweka mimi kwakuwa imekuwa ikijirudia kila mwaka..
Mkweli ni nani... Muongo ni nani? Hilo sijalitilia maanani.. Mimi mjadala wangu uko kwenye maswali niliyoweka mwishoni kwakuwa walau haya tunaweza kuyajadili kwa wakati tulio nao na uhalisia wake sundoka,

Jr
 
umendika uwongo usipende sana kila kitu uandike hata kama huna ujuzi au elimu nacho we andika kuhusu majini na mapepo machafu vingime vinahitaji kina cha elimu hapa umedanganya rudi deep then andika tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Kafanya kucopy na kupaste jamaa zwazwa sana wanao muamini humu ni misukule yake.
Kila kitu anataka aonekane anajua kumbe bwege mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa mmefanya kumshambulia mtoa mada na sio hoja yenyewe, angekuwa amecopy basi angetoa credit kwa mwandishi.
 
Back
Top Bottom